Mkuu,utalii uko hivi! Kwanza uwe na muda wa kutosha,pili pochi angalau iwe nene kiasi,mambo ni hivi,unamwambia guide unapenda kuona mnyama yupi,yeye anajua muda na mahali sahihi wanapopatikana(japo wakati mwingine wanaweza wasiwepo)ila bado guide ana second option! Muda ni jambo muhimu sana kwa utalii! Mfano mimi napenda kuingia hifadhini mapema sana kabla ya magari mengine hayajaingia,advantage yake ni kuwa tutaanza kuwaona wanyama adimu kuanzia karibu tu kabla hata hatujaingia huko ndani ndani maana kabla magari hayajaanza kuvuruga pori wanyama wengi huwa wanapenda kuja barabarani au karibu na barabara,sasa ikiwa umeingia hifadhini saa sita na ukatembezwa mbio kama Mwenge hutaona raha ya utalii,na pia kama mlienda na magari kama ya shule au wafanyakazi(in large group)na kibali chenu kinaisha saa kumi na mbili,ukute na guide anayewaongoza ameshawasoma na kujua hii kazi nnayoifanya haina Tip lazima awakimbize kama Mwenge ili akatege mingo za maana!!! Mzungu aje kutoka ulaya kuja kumuona Twiga live halafu arudi kwao hajamwona? Jipange mkuu! Ikiwa hujashinda Bingo haina maana kuwa Bingo hainaga mshindi! Hukucheza vya kutosha!!