Nilidhani ukiingia mbuga ya wanyama Unaona wanyama kirahisi kumbe napo tabu tupu

Nilidhani ukiingia mbuga ya wanyama Unaona wanyama kirahisi kumbe napo tabu tupu

Hivi majuzi nilibahatika kufika ngorongoro national park eneo la crater; nikitarajia kuona wanyama wakubwa kwa ufasaha kama inavyosimuliwa kwenye movie mbalimbali za wanyama.

Niseme kwa dhati kabisa baada ya kuzungushwa mda mrefu niliambulia kuona nyati, kiboko,digidigi,punda na ndege flamingo. Lakini Tembo nilioneshwa miguu tu walipokanyaga sikuwaona, simba nao nilioneshwa kwa mbaali sana tena wawili tu wadogo kama mbwa, nikaoneshwa kichaka cha Faru wanamopenda kukaa lakini sikuona!

Kiufupi roho yangu haikuridhika kabisa bora ningeangalia movie tu!

matarajio yangu nilizani nitaona Faru, chui, twiga, Tembo na wanyama wengine kirahisi kumbe sio kazi rahisi kama nilivyotarajia.

Nifanyeje Next time ili niwaone wanyama kiufasaha kama tusimiliwavyo?
Nenda Serengeti kuna full ecosystem au utalii wa usiku utawaona wengi sababu wanakuwa wameshatoka kwenye mishe mishe zao.
 
Nenda Serengeti kuna full ecosystem au utalii wa usiku utawaona wengi sababu wanakuwa wameshatoka kwenye mishe mishe zao.
Yaani wanyama nao wana mishemishe?
Mimi nilijua mishemishe ni kula na kuzaliana tu...kwamba herbivorous wanakula mchana wakati carnivorous wanawinda vizuri usiku kwa sababu ya night vision advantage. Sasa kama unataka kuwaona carnivorous basi usiku ndio poa.
 
Mkuu,utalii uko hivi! Kwanza uwe na muda wa kutosha,pili pochi angalau iwe nene kiasi,mambo ni hivi,unamwambia guide unapenda kuona mnyama yupi,yeye anajua muda na mahali sahihi wanapopatikana(japo wakati mwingine wanaweza wasiwepo)ila bado guide ana second option! Muda ni jambo muhimu sana kwa utalii! Mfano mimi napenda kuingia hifadhini mapema sana kabla ya magari mengine hayajaingia,advantage yake ni kuwa tutaanza kuwaona wanyama adimu kuanzia karibu tu kabla hata hatujaingia huko ndani ndani maana kabla magari hayajaanza kuvuruga pori wanyama wengi huwa wanapenda kuja barabarani au karibu na barabara,sasa ikiwa umeingia hifadhini saa sita na ukatembezwa mbio kama Mwenge hutaona raha ya utalii,na pia kama mlienda na magari kama ya shule au wafanyakazi(in large group)na kibali chenu kinaisha saa kumi na mbili,ukute na guide anayewaongoza ameshawasoma na kujua hii kazi nnayoifanya haina Tip lazima awakimbize kama Mwenge ili akatege mingo za maana!!! Mzungu aje kutoka ulaya kuja kumuona Twiga live halafu arudi kwao hajamwona? Jipange mkuu! Ikiwa hujashinda Bingo haina maana kuwa Bingo hainaga mshindi! Hukucheza vya kutosha!!
 
Yaani wanyama nao wana mishemishe?
Mimi nilijua mishemishe ni kula na kuzaliana tu...kwamba herbivorous wanakula mchana wakati carnivorous wanawinda vizuri usiku kwa sababu ya night vision advantage. Sasa kama unataka kuwaona carnivorous basi usiku ndio poa.
Ndio wapo kam binadamu,nilipokuwa nawasoma wakat mwingine tulikuwa tukienda porini hatuwaoni,mfano lake manyara kuna simba wapanda juu ya mti ila sikuwai kumwona.
 
Pole Sana mkuu naona Ulikua na bahati mbaya,Mi nilienda mwaka juzi nilibahatika kuwaona Simba tena wanapandana kabisa,faru,Tembo na wengine I sikubahatika kumuona chuo tu.Kule crater hakuna Twiga but nje ya creator tulibahatika kuwaona coz wanasema wako wachache.Mwaka huu nilienda Mikumi Kule Twiga na Tembo ni wengi Sana na nilibahatika kuona Simba but faru na Chui si kuwaona.Simba nili muona kwa Karibu Sana kama mita 30 tu toka barabarani.
 
Nimetembelea Mbuga nyingi, moja ya sehemu unazoweza kuwaona wanyama kiurahisi ni hilo korongo la ngorongoro. Trust me. Nenda Saadani au Tarangire halafu ulinganishe na hapo, ngorongoro ipo juu....tatizo ni hiyo management tu...mambo ya C.A.G

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vizuri unapoenda mbugani. Nenda kwa ajili ya kutalii sana,yaani kurefresh akili tu,usifikirie sana kuona wanyama tu. Kwa sababu wanyama karibu wote hata kwa picha tayari unawafahamu. Nenda kurefresh tu,hata kufurahi mandhari tu. Sawa na unapoenda ufukweni iwe baharini au ziwani si lazima ukaogelee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi mm nina bahati au kampuni pengine ya utalii uliyoitumia, isije kua ulienda kwa coaster badala ya kutumia gari za kampuni za tours. Watu wa kampuni wanawasiliana kwa radio calls zao na kuelekezana wanyama walipo kwa signals zao mfano utasikia ndevu sehemu flani hapo ujue simba ndiko aliko sasa mtu ukienda na gari binafsi huwezi fahamu wanyama waliko labda uwaulize wale wa tours.
Mimi sijaona chui tu porini, niliwahi kumuona nikiwa mdogo sana pale Saanane kisiwani Mwanza akiwa kwenye cage ila mbuga nilizotembelea za Tarangire, Ngorongoro, Saadani, Mikumi na Arusha nimeona tembo kwa ukaribu mno, simba ndio kabisa walikuja kulala kwenye kivuli cha gari, nyati, faru, fisi, kiboko, twiga, nyumbu, pundamilia etc.

Few years from now you may wish you should have started today...
 
Hivi majuzi nilibahatika kufika ngorongoro national park eneo la crater; nikitarajia kuona wanyama wakubwa kwa ufasaha kama inavyosimuliwa kwenye movie mbalimbali za wanyama.

Niseme kwa dhati kabisa baada ya kuzungushwa mda mrefu niliambulia kuona nyati, kiboko,digidigi,punda na ndege flamingo. Lakini Tembo nilioneshwa miguu tu walipokanyaga sikuwaona, simba nao nilioneshwa kwa mbaali sana tena wawili tu wadogo kama mbwa, nikaoneshwa kichaka cha Faru wanamopenda kukaa lakini sikuona!

Kiufupi roho yangu haikuridhika kabisa bora ningeangalia movie tu!

matarajio yangu nilizani nitaona Faru, chui, twiga, Tembo na wanyama wengine kirahisi kumbe sio kazi rahisi kama nilivyotarajia.

Nifanyeje Next time ili niwaone wanyama kiufasaha kama tusimiliwavyo?
kwahiyo we uldhani mitembo na mifaru ikae inakusubiri wewe uwaone kw angle iliyokukalia poa kirahisi rahisi! na wao huwa wako bize na maisha yao.

ni sawa na mtu wa tunduma aje dar azunguke halafu ashangae mbona kafika dar hajamuona diamond wala wema wala makonda, wakati hao watu wako bize na mambo yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda siku hizi wametoweka...ila tulikuwa tunakesha nao hapo mamlaka siku nzima.

Zamani kidogo ilikuwa huwezi kutembea mwenyewe pale polisi kwenda nyumba za wafanyakazi mwenyewe. Umbali wa mita 100 tum
 
Kwahiyo kwa 5,000/- ulitaka uone wanyama wa mbuga nzima?kweli bado tuna safari ndefu...!

Back
Top Bottom