Nilidhani ukiingia mbuga ya wanyama Unaona wanyama kirahisi kumbe napo tabu tupu

Nilidhani ukiingia mbuga ya wanyama Unaona wanyama kirahisi kumbe napo tabu tupu

Vizuri unapoenda mbugani. Nenda kwa ajili ya kutalii sana,yaani kurefresh akili tu,usifikirie sana kuona wanyama tu. Kwa sababu wanyama karibu wote hata kwa picha tayari unawafahamu. Nenda kurefresh tu,hata kufurahi mandhari tu. Sawa na unapoenda ufukweni iwe baharini au ziwani si lazima ukaogelee

Sent using Jamii Forums mobile app
Sikuifurahia ile safari..... Nakumbuka kabisa. Nilijiona nimekwenda kuchoka zaidi.
 
Nimetembelea Mbuga nyingi, moja ya sehemu unazoweza kuwaona wanyama kiurahisi ni hilo korongo la ngorongoro. Trust me. Nenda Saadani au Tarangire halafu ulinganishe na hapo, ngorongoro ipo juu....tatizo ni hiyo management tu...mambo ya C.A.G

Sent using Jamii Forums mobile app
Saadani kule kwa wanaotaka kuona Twiga, Tembo na Ngiri hao wapo tele na vingedere. Pia kule mtoni kuna viboko na Mamba wanyama wengine ni shughuli kuwaona.
 
Hivi majuzi nilibahatika kufika ngorongoro national park eneo la crater; nikitarajia kuona wanyama wakubwa kwa ufasaha kama inavyosimuliwa kwenye movie mbalimbali za wanyama.

Niseme kwa dhati kabisa baada ya kuzungushwa mda mrefu niliambulia kuona nyati, kiboko,digidigi,punda na ndege flamingo. Lakini Tembo nilioneshwa miguu tu walipokanyaga sikuwaona, simba nao nilioneshwa kwa mbaali sana tena wawili tu wadogo kama mbwa, nikaoneshwa kichaka cha Faru wanamopenda kukaa lakini sikuona!

Kiufupi roho yangu haikuridhika kabisa bora ningeangalia movie tu!

matarajio yangu nilizani nitaona Faru, chui, twiga, Tembo na wanyama wengine kirahisi kumbe sio kazi rahisi kama nilivyotarajia.

Nifanyeje Next time ili niwaone wanyama kiufasaha kama tusimiliwavyo?
Mkuu labda ulikuwa na bahati mbaya tu siku hiyo... lakini kati ya mbuga zote nchi hii ngorongoro crater ndo mahala ambapo unapokwenda una uhakika kwa asilimia zaidi ya 90 wa kuona simba Tembo pamoja na faru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbuka unaenda kuangalia wanyama sio kumtembelea mtu ambaye atakaa kusubiri ujio wako kwa hiyo bajeti ya kutosha ni muhimu, sijui ni vyuma kukaza huko mbugani siku hizi ni ngumu kuwakuta wanyama wamejilaza tu wakisubiri watalii mje mpige picha
 
Hivi majuzi nilibahatika kufika ngorongoro national park eneo la crater; nikitarajia kuona wanyama wakubwa kwa ufasaha kama inavyosimuliwa kwenye movie mbalimbali za wanyama.

Niseme kwa dhati kabisa baada ya kuzungushwa mda mrefu niliambulia kuona nyati, kiboko,digidigi,punda na ndege flamingo. Lakini Tembo nilioneshwa miguu tu walipokanyaga sikuwaona, simba nao nilioneshwa kwa mbaali sana tena wawili tu wadogo kama mbwa, nikaoneshwa kichaka cha Faru wanamopenda kukaa lakini sikuona!

Kiufupi roho yangu haikuridhika kabisa bora ningeangalia movie tu!

matarajio yangu nilizani nitaona Faru, chui, twiga, Tembo na wanyama wengine kirahisi kumbe sio kazi rahisi kama nilivyotarajia.

Nifanyeje Next time ili niwaone wanyama kiufasaha kama tusimiliwavyo?
kweli Adventure is not for everyone ... usiende tena had ujue maana ya advnture

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom