Nilifadhaika sana kupata watoto wa kike tu

Nilifadhaika sana kupata watoto wa kike tu

mediaman

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2011
Posts
451
Reaction score
688
Hali hii hutokea katika ndoa nyingi. Mke anazaa watoto wa jinsia moja tu mfululizo, ama wa kike au wa kiume tu. Wazazi wengi huwa wanapenda wapate watoto wa jinsia zote. Kwa sababu hiyo inapotokea wanapata watoto wa kiume tu au wa kike tu huanza kutafuta njia ya kutatua 'tatizo' hilo. Wengine huenda kwa madaktari kutafuta ushauri wa kisayansi na kufanikiwa kupata mtoto wanayemtaka; lakini wengine ushauri wa kisayansi bado hauwasaidii kupata mtoto wa kiume au wa kike.

Wazazi wanapofikia hali hiyo wengine huenda kwa waganga wa kienyeji na huko huishia kuchanganyikiwa tu kutokana na masharti magumu wanayoambiwa na mganga. Jaribu kuwaza mtu anaambiwa apeleke kwa mganga kinyesi "fresh" cha tembo ndio apate dawa!

Nakumbuka mme fulani alisababisha mgogoro katika ndoa yake baada ya kumgombeza mke wake kwanini anazaa watoto wa kike tu. Na waume wengine huamua kuwaacha wake zao au kuoa mke wa pili ili wajaribu kama watapata watoto wanaowataka kwa njia hiyo. Njia zote hizo zinaposhindikana hubaki na huzuni isiyokoma.

Mimi pia nimepitia hali hiyo. Mara ya kwanza mke wangu alipata mtoto wa kike. Mara ya pili akajifungua tena mtoto wa kike. Tulikuwa tunajitahidi angalau tupate mtoto kila baada ya miaka miwili. Mara ya tatu mke wangu akazaa tena mtoto wa kike. Hee nikaanza kufadhaika, maana nilitamani na mimi niwe na mtoto wa kiume. Sikumlaumu wala kumgombeza mke wangu kwanini anazaa watoto wa kike tu kwa sababu najua kisayansi mwanaume ndiye anayehusika zaidi kufanya mtoto wa jinsia ipi azaliwe.

Katika kutafakari nifanyeje nikakumbuka yale maneno ya Mungu yasemayo "Ombeni nanyi mtapewa" Nikakumbuka pia habari za mama mmoja katika Biblia aliyekuwa hapati kabisa watoto lakini baada ya kumwomba Mungu akapata.

Kwa sababu hiyo na mimi nikaanza kumwomba Mungu kwa juhudi kwamba mke wangu atakapojifungua mtoto wa nne, awe wa kiume. Ndugu zangu, Mungu hana upendeleo, alisikia maombi yangu na kutupatia mtoto wa kiume. Kinachotakiwa tu ni kuhakikisha mahusiano yetu na Mungu ni mazuri na kuomba kwa imani, pasipo shaka. Yote yawezekana kwake aaminiye(Mk 9:23).
 
Hali hii hutokea katika ndoa nyingi. Mke anazaa watoto wa jinsia moja tu mfululizo, ama wa kike au wa kiume tu. Wazazi wengi huwa wanapenda wapate watoto wa jinsia zote. Kwa sababu hiyo inapotokea wanapata watoto wa kiume tu au wa kike tu huanza kutafuta njia ya kutatua 'tatizo' hilo. Wengine huenda kwa
Hongera mkuu, lakini kumbuka, mtoto ni mtoto tuu na ni zawadi toka kwa mwenyezi Mungu.
 
Back
Top Bottom