Nilifadhaika sana kupata watoto wa kike tu

Nilifadhaika sana kupata watoto wa kike tu

Kweli kwa jinsi alivyohangaika atamfanya "mungu" wake hapo ndo balaa linapoanzia.

“Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya miungu wa uongo, au kinyago cha chochote kilicho mbinguni, katika nchi au majini chini ya dunia. Usiisujudie wala kuitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha hao wanichukiao. Lakini nawafadhili maelfu ya wale wanipendao na kuzishika amri zangu(Kutoka 20:3-17).

 
Ukisoma hii thread utasema kuzaa mtoto wa kiume ni dhambi na laana.
Mungu naomba rehema na neema zako ziwe juu ya watoto wangu watatu wa kiume na wanne ninayetarajia kumpata pamoja na wa mleta mada Amen.
 
Kuna Mtu yupo Amejaamiiana mara moja kwa Kificho na mimba ikaja na ni mtoto wa kiume; Kukuelewa kwamba uliomba Mungu akakupa inakuwa ngumu sana. All in all Hongera sana.
Mtoto huyo anafanana na mimi sana. Unaweza kumficha mwanadamu lakini huwezi kumficha Mungu. Na mtu akiwa na uhusiano wa karibu na Mungu, Mungu anamfunulia mambo yaliyofichika. Kama huwa unasoma Biblia kumbuka Petro alivyofunuliwa jambo walilokuwa wameficha Anania na mkewe Safira.
 
Ukisoma hii thread utasema kuzaa mtoto wa kiume ni dhambi na laana.
Ukisoma hii thread kwa macho manne, utagundua kuwa kuzaa watoto wa kike au kiume tu sio dhambi wala sio laana. Ila furaha ya wanandoa wengi huwa timilifu wanapopata watoto wa kiume na wa kike.
 
Basi iwekwe option ya watu ku-dislike ili ujumbe uende kwa wahusika,haileti maana naandika ujinga halafu nipewe likes kwa hivi nitazidi kuonyesha ujinga wangu maana najua wapo wanaokubaliana na mimi.

Mods tunaomba hiki kitu,DISLIKE BUTTON iwepo.

Cc:invisible
Sioni sababu ya Dislike button. Thread title kama naona haina mashiko, sina haja ya kusoma content. Mtu akiamua kusoma content ni wazi title imemvutia. Hivyo wanaogonga likes wako sahihi kabisa.
 
Kwanini ufadhaike kwa kuwa na watoto wa kike? Kumbuka bila mama yako labda usingekuwepo duniani na bila mkeo usingeitwa Baba. Tuache tabia ya kudharau watoto wa kike nao wana mchango wao mkubwa na wa maana sana katika jamii zetu.
Kufadhaika sio kudharau. Au TUKI inasemaje?
 
Ukisoma hii thread kwa macho manne, utagundua kuwa kuzaa watoto wa kike au kiume tu sio dhambi wala sio laana. Ila furaha ya wanandoa wengi huwa timilifu wanapopata watoto wa kiume na wa kike.
Moyo wa mtu ni kichaka na umejawa na mambo mengi. Pengine huyo anayesema watoto wote ni sawa hana mtoto hata mmoja au pengine ndo anaye mmoja so hajajua ya mbeleni.Watoto wote ni wazuri na ni baraka kuwa nao na mtu huona furaha zaid akichanganya jinsia hata kama wakiwa ratio ya wanne kwa mmja ilimradi amechanganya jinsia.Na Mungu huwa anajibu kwa kukupa unachomuomba kama umemuomba kwa imani na kama mnaishi kwa kumlingana Mungu.haina haja ya kuongea sana....time will tell
 
Kabla hujaoa, ulitamani sana upate mke, ukapata, ukafurahi. Baada ya muda ukatamani upate mtoto, ukapata wa kwanza wa kike, ukafurahi, ukapata tena wa pili na wa tatu, wote wa kike, ukafurahi. Baadaye ukatamani upate mtoto wa kiume, ukapata, furaha ikaongezeka. Ndivyo maisha yalivyo. Ukipata furaha ya aina moja unatamani upate aina nyingine ya furaha. Watoto hao wakikua utatamani wapate kazi nzuri wajitegemee. Ikitokea hivyo utafurahi zaidi. Wakioa na kuolewa na kukuletea wajukuu, utafurahi zaidi kuanza kuitwa"babu."
Mlolongo huo wa furaha mara nyingi haupatikani kirahisi. Kuna vikwazo. Mungu anajua mambo mengine hatuwezi kuyapata kwa akili au juhudi zetu wenyewe ndio sababu anatuambia tuombe lolote tutapewa ili furaha zetu ziwe timilifu.

Yn 16:24​

Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu
 
Moyo wa mtu ni kichaka na umejawa na mambo mengi. Pengine huyo anayesema watoto wote ni sawa hana mtoto hata mmoja au pengine ndo anaye mmoja so hajajua ya mbeleni.Watoto wote ni wazuri na ni baraka kuwa nao na mtu huona furaha zaid akichanganya jinsia hata kama wakiwa ratio ya wanne kwa mmja ilimradi amechanganya jinsia.Na Mungu huwa anajibu kwa kukupa unachomuomba kama umemuomba kwa imani na kama mnaishi kwa kumlingana Mungu.haina haja ya kuongea sana....time will tell
Naam, umenena vema
 
Kupata watoto jinsia moja hupelekea ndoa kuwa na idadi kubwa ya watoto. Mfano hapa ninapoishi familia moja ilifikisha watoto kumi na moja wa kiume tu. Katika kutafuta Mtoto wa kike yule mama alibeba mimba mara ya 12, alipojifungua alipata mapacha wawili, wote wa kike.
Bora kuchanganya jinsia zote. Maana kama ni wakike wote wakikuwa na kuolewa basi kwako kunakuwa hakuna wakurithi. Na wakiwa wakiume kwa mfano Mama umekuwa Mzee/ ukaumwa Mtoto wa kiume hawezi kumtunza Mama kama anavyotunzwa na Mtoto wa kike.(pia kinyume chake kwa Baba).

Wale wanaosema watoto ni watoto hawajawahi ona jinsi mwisho wa uzee unavyokuwa mbaya hasa ukiwa na watoto wa jinsia moja tu.
Dah, umeona mbali, mkuu
 
Ndugu zangu, Mungu hana upendeleo, alisikia maombi yangu na kutupatia mtoto wa kiume. Kinachotakiwa tu ni kuhakikisha mahusiano yetu na Mungu ni mazuri na kuomba kwa imani, pasipo shaka.
  1. Ibrahim alikosa kabisaaaa!!! Wakati wa Bwana ulipofika hayawihayawi yakawa.
  2. Sara hakuwa mchoyo, alimshauri Ibrahimu, mumewe mpendwa, atazametazame huko na kule huenda angepata, Ikawa
  3. Mshauri mkeo hali inapokuwa siyo asikubane kivileeeeeeeeeee! Anaweza kuwa Sara kwa muda haidhuru
 
shauri mkeo hali inapokuwa siyo asikubane kivileeeeeeeeeee! Anaweza kuwa Sara kwa muda haidhuru
Kwetu sisi tunaomwamini Yesu, tunajua huu ni wakati wa Agano Jipya. Hivyo ndoa inapaswa kuwa ya mme mmoja na mke mmoja tu hadi kifo kiwatenganishe.
 
Dunia ina mambo! Wakati ww unafadhaika kupata mtoto wakike wengine wanatamani waone mimba inafananaje
You are right bro, if not sister! Duniani kuna mifadhaiko mingi. Kuna batu wanafadhaika kula wali na nyama kila siku wakati wengine wanatamani wapate uji wa chunvi.

Yesu alijua katika dunia hii kuna ufadhaikaji mwinngi. Tazama anavyotutia moyo ktika kitabu cha Yohana 14:1-3 "Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo."
Thank you Lord Jesus for this great hope.
 
Back
Top Bottom