Nilifumaniwa kwenye geto la demu enzi hizo lakini mzee wa nyumba ile akasema nisipigwe na vijana wanisindikize hadi kwetu.

Nilifumaniwa kwenye geto la demu enzi hizo lakini mzee wa nyumba ile akasema nisipigwe na vijana wanisindikize hadi kwetu.

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Hii huwa inajirudia rudia sana kichwani kwanini mzee yule aliwakataza vijana wake wasinipige na akateua wawili wale wakubwa wanipeleke na wa hakikishe nimefika salama salimini bila kupigwa?

Kipindi hicho genye ndo limeshika hatamu yaani huniambii kitu kuhusu mbususu mara kadhaa nilikuwa sili nyumbani ili niwahi kwa demu.

Kananuni ilikuwa ni moja ukiambiwa na demu kuwa nyumbani huwa tunalala saa4 hivyo itakupasa wewe ufike saa2:30 ili kusoma ramani na kujihakikishia wote wapo na wote wamelala kwenye mji huo. Ukienda muda huohuo tegemea kukamatwa maana unakuwa hujui nani yupo na nani hajarudi kutoka matembezini hivyo unaweza dakwa kirahisi mno.

Siku hiyo haikuwa nzuri kwangu mbu walikuwa wengi sana na sharti jingine mbu hutakiwi kuwapiga kofi maana mbwa au watu watasikia hivyo mbu unakuwa unawandoa kama rafiki zako yaani kama unapaka mafuta vile.

Hiyo siku niliona liwalo na liwe saa3 tu nikazama ndani wakiwa bado jikoni na wanaume wakiwa bado kwenye ule moto wa kisukuma tuinaita shikome.

Nikiwa mle kaliagizwa ka binti kaijie kitu fulani hata sikujua kwa vile kalikuja na tochi zile za kutengeneza maarufu umeme na demu alikuwa analala chini hakuwa na kitanda hivyo sikuwa na option yoyote ile ya kujificha.

Basi baada ya kuniona kale kabinti kalipiga kelele jambo lililo washitua watu wote nakuja mbio mle na mimi kukutwa sina namna kabisa hata usemi sina nasubiria hukumu tu.

Basi vijana waliowahi nakumbuka ni mmoja tu alinizaba makofi mfululizo kama ma4 hivi then baba mji akawaambia waniache mara moja.

Hapo nilijua sasa napigwa fimbo hadi basi ajabu aliitwa yule binti akaulizwa unamjua huyu akakili ndio namjua kisha akaambiwa nenda jikoni na vijana wawili wakubwa wakaambiwa mpelekeni na msimpige hadi afikishe kwao salama.

Aisee wale jamaa walitukana njia nzima lakini hakuna hata mmoja aliye nipiga na ikumbukwe mzee yule pale kijijni alikuwa anaogopeka vibaya mno huku akihusishwa na wizi (jambazi) lakini mimi mbele ya mbususu sikujari hata vijana wake pia walikuwa wababe wababe sana kiasi kwamba vijana wengi waliwaogopa sana mademu wa mji ule.

Kesho yake nilikaa kwa machale sana nikijua yule demu huenda ataletwa lakini haikuwa hivyo na kipindi kile hapakuwa na simu kwa sisi hata yeye hivyo nilimuwinda na kumuuliza akasema alipigwa bakora7 tu kesi ikaisha huku akinalaumu sana kuingia kabla ya muda nilio zoea nikamwambia mbu walikuwa wengi mno siku ile.
 
😂 ila enzi zile watu walikua wastaarabu sana.....nje ya mada ivi alieingiza sauti kwenye ile muvi ya Yesu ni nanii
 
Balaa sana.

Nakumbuka hata Mimi home simu Moja Giza limeingia nikazunguka Nyuma ya nyumba nikakuta njemba inanyemelea demu pale maskani. Nikaibana Hadi inanipa hela nikiacha ikaondoka.
 
Hahahahahahah hongera saana legend,

Msamaha sometimes huleta impact kubwa kuliko adhabu
Nikweli tangu siku hiyo sikuwahi kwenda tena kwenye mji ule hata nikimuona yule mzee nakata kona kali sana
Ila kama wangenipiga lazima ningeendelea
 
Balaa sana.

Nakumbuka hata Mimi home simu Moja Giza limeingia nikazunguka Nyuma ya nyumba nikakuta njemba inanyemelea demu pale maskani. Nikaibana Hadi inanipa hela nikiacha ikaondoka.
Mkuu ukiwa na dada hapo home kugongewa ni lazima uwe mpole au mkali hayo ni yako ila muhimu utagongewa tu
 
Back
Top Bottom