Kuachia mashuzi au kwenda kujisaidia na kutoacha ustaarabu wa kimazingira ni aina ya uchafu kama uchafu mwingine.
Kujamba ukiwa na mwenzako halafu maharufu yakasambaa na mwenzako akayanusa ni ushamba kama mwingine tu na ni kukosa adabu.
Kwenda chooni kujisaidia na kisha kuruhusu mwenzako akapata ile harufu ya shughuli zako ni matokeo ya kutokuwa na nidhamu na kutojiheshimu.
Huyo mwanamke anajitambua na ana adabu sana na wewe. Miaka mitatu ameweza kukupa taswira kuwa yeye ni msafi muda wote hiyo itakufanya uwe very comfortable ukiwa nae. Ni rahisi sana kuwa na ustaarabu kwa mwenzako na asipate kero ya harufu za ajabu. Ni sehemu ya kuheshimiana na kuishi kwa adabu na kufanya uwe na mvuto kwa mwenzako zaidi.
Weka ratiba yako ya kukata gogo muda ambao mwenzako atakuwa aidha ametoka au yupo busy na kazi.
Jifunze kumpisha mwenzako chumbani bila kuongea chochote. Ukiona kaingia washroom wewe toka hata uende nje kujinyoosha ili umpe privacy ya kujilipua.
Hakikisha bafuni kuwe na maji ya kutosha, na marashi ya kuleta harufu nzuri hapo ndani. Kuwe na usafi wa muda wote.
Ukibanwa na ushuzi nenda nje tafuta kona nzuri achia shuzi lako then rudi ndani kwa mwenzako ukiwa hauna hewa chafu. Kumjambia mtu ni ishara kuwa hauna adabu kwake na hauna heshima nae. Hivi unaweza kumjambia baba yako au mama yako au mkweo au boss wako, au mchungaji wako au mufti wako? Why sasa umjambie mtu muhimu kama mwanaume/mwanamke wako?
Anyways, tuwaheshimu wapenzi wetu wanaotuheshimisha hapa duniani.