Nilijenga kwenye kiwanja cha familia ya mke wangu sasa bahati mbaya mke wangu huyo amefariki

A
Hahahaaa yaani unajenga kwenye kiwanja cha zawadi kutoka ukweni? Kwani vikao vyenu vile huwa hauhudhurii?
Wala amna tatizo kabsa ukisha tamka kwamba umetoa zawadi iyo ni imeisha.. anacho takiwa kufanya uyu bwana kama kitanuka ni aweze kuthibitisha tu kwamba icho kiwanja baba mkwe alitoa kama zawadi ivyo inabaki kua subject to wanandoa na sio baba mkwe

Sijaelezea sana kwa sababu ndo kwanza ana waza na akija nuka, siku nyingine mkipewa zawadi hakikisheni mna iweke kwa maandishi iwe Deed of Gift
 
Wakuu ndiyo ipo hivyo

Baba yangu mkwe alibahatika kuwa na uwanja mkubwa sana hivyo aliamua kuufanya uwanja huo kuwa ni uwanja wa familia yake hivyo aliamua kuwagawia kiwanja hicho watoto wake wote kila mtoto wake na kipande chake.

Watoto wake wenyewe wapo sita hivyo kila mmoja akamkatia kiwanja chake na kilichobakia anakaa yeye mwenyewe baba mke na mke wake na ndugu wengine.

Sasa mimi na mke wangu tukaona haina haja ya kununua uwanja mwingine ni bora tu nijenge kwenye uwanja huo huo ili kuokoa gharama ya kununua uwanja mwingine.

Sasa kwa bahati mbaya mke wangu amefariki. Najiuliza maswali mengi sana.
Hatma yangu ni ipi baada ya mke wangu kufariki?

Naweza kuoa mke mwingine na kuishi naye hapa kwenye hii nyumba niliyojenga kwenya kiwanja cha familia alichopewa marehemu mke wangu na baba yake na ndugu wa mke wangu aliyefariki wakaniacha salama kweli?

Je, naweza kuuza nyumba hii niliyojenga kwenye huu uwanja wa familia kweli na ndugu wa mke wangu alifariki wakanielewa?

Naweza kuishi hapa kwa amani kweli?

Mmmmmh! Nimekumbwa na balaa zito sana wakuu.
Ungetafuta ushauri kabla ya kujenga . Hapo jomba maji yashamwagika hesabu maumivu
 
Kama wewe ni muislamu omba wakupe/wakuozeshe dadamtu au mdogomtu au hata binamu ya mkeo uendeleze ukoo maana hakuna ujanja hapo unless uwe na makaratasi ya makabidhiano kisheria
 
Aah pole sana mkuu fanya maamuzi ya kiume
👉Mosi muelwane muuze mugawane
👉Pili, iache tu watoto wataish hapo baadae
"👉Fanya sadaka, mali huja, mali hupotea, jichange tena ujenge sehemu N. B HAKIKISHA kiwanja hakina ukakasi wowote. Jifunze kutokana na makosa

👉Mwisho, ushauri wa kijinga ibomoe mkwose wote🤣
 
Si una watoto?
itakuwa ni nyumba yao.
Wewe jipange kivingine, huwezi kuoa hapo wala kuuza hiyo nyumba wala kuibomoa.

Hama huo mji!
Kwanza una moyo!
Uliwezaje kuishi eneo kuna Mkuu wa kaya na wewe ukajiona bado ni Baba mwenye mnhumba? , hata kukaza uliwezaje kiukweli?
 
Wakuu ndiyo ipo hivyo

Baba yangu mkwe alibahatika kuwa na uwanja mkubwa sana hivyo aliamua kuufanya uwanja huo kuwa ni uwanja wa familia yake hivyo aliamua kuwagawia kiwanja hicho watoto wake wote kila mtoto wake na kipande chake.

Watoto wake wenyewe wapo sita hivyo kila mmoja akamkatia kiwanja chake na kilichobakia anakaa yeye mwenyewe baba mke na mke wake na ndugu wengine.

Sasa mimi na mke wangu tukaona haina haja ya kununua uwanja mwingine ni bora tu nijenge kwenye uwanja huo huo ili kuokoa gharama ya kununua uwanja mwingine.

Sasa kwa bahati mbaya mke wangu amefariki. Najiuliza maswali mengi sana.
Hatma yangu ni ipi baada ya mke wangu kufariki?

Naweza kuoa mke mwingine na kuishi naye hapa kwenye hii nyumba niliyojenga kwenya kiwanja cha familia alichopewa marehemu mke wangu na baba yake na ndugu wa mke wangu aliyefariki wakaniacha salama kweli?

Je, naweza kuuza nyumba hii niliyojenga kwenye huu uwanja wa familia kweli na ndugu wa mke wangu alifariki wakanielewa?

Naweza kuishi hapa kwa amani kweli?

Mmmmmh! Nimekumbwa na balaa zito sana wakuu.
Yakutunga kuwaumiza watu akili.....tumestukaa
 
Kwa vile maji yamemwagika na vikao huudhurii nakupa mbinu ya mwisho mtafute baba mkwe ongea nae kiutu uzima awe kama anakuuzia kiwanja kilicho chini ya hyo nyumba ukishampa hela akakupa na document amua kuuza sasa hiyo nyumba ukatafute eneo lingine

Kama hilo ni gumu na una watoto na huyo mkeo basi achana napo wanao wataishi hapo japo itafika mda baba mkwe akifariki ndugu pia wanaweza kuipora hyo mali kama wana roho mbaya na hutaweza kufanya chochote

La mwisho ukiona hakuna kinachowezekana bomoa nyumba yako waachie uwanja wao

Mwisho kabsa kama unaweza kuanza upya mahali pengine achana na hiyo nyumba kajipqnge upya na uoe kama ukitaka
 
Back
Top Bottom