Nilijiapiza mjini nitarudi kutembea tu, lakini hapa nimelalia maboksi baada ya kuungua na maisha ya kijijini

Nilijiapiza mjini nitarudi kutembea tu, lakini hapa nimelalia maboksi baada ya kuungua na maisha ya kijijini

Ilikuwa ni mwezi wa saba sikumbuki tarehe ndo niliaga JF na kuelekea kijijini nikitokea Dar, baada ya kumaliza mafunzo ya ufundi, na nikijiapiza mjini ntarudi kutembea tu. Lakini hapa ninapoandika huu ujumbe nipo nimelalia maboksi kwenye geto la kupanga baada ya kuungua na maisha ya kijijini huku nikiwa na ujuzi wangu vizuri tu. Kwanza kabisa mimi ni fundi - simu, radio, umeme wa majumbani. Natengeneza video mbali mbali na vitu vingi vingi tu vinavyotumia umeme.

Changamoto za kijijini:
  • Upatikanaji haraka wa diode au spea za maredio tv nk.
  • Umbali wa kuvifikia nauli 12000 kwenda na kurudi.
  • Intaneti, unapokuwa unahitaji msaada wa kiufundi kupitia google
  • Kazi za msimu
  • Wateja wengi ni malialia n.k
Ndo vimenifanya leo hii nimelala kwenye mabox na vifaa vyangu vya kazi hapa Arussha mjini leo hii

Asanteni nawasilisha
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji23] dah mkuuu umefikia viji vya wapi uko arusha mnk
 
Nashukuru sanaaa broo kwani kijiji kizima fundi mwenye vifaa na utaalamu ilikuwa ni mm pekee lakini ndo hivo maslahi yamenifanya niondoke
Naomba nimlete kijana angu umfundishe kaz hzo za ufundi mmkuu naomba sana kjn yuko atusha pale pale
 
Lazima ucheke! Maana wewe uko kwenye kundi la wale watu wanaokula, bila ya kutoka jasho!

Nadhani umenielewa vizuri. Hivyo sina sababu ya kuingia ndani zaidi.
Sidhani kama ni kweli hilo huku hatujuani muache bint wa watu achekee mkuu
 
Natafuta vijana 5 manunda kweli,kazi yetu itakuwa ni kuvamia popote penye pesa,hakuna kucheka na mtu niza kichwa tu
Wew kijana wa arusha ndio unaongea ujinga gani wew s ulisema kwemu maisha ni bora na baba ako alikuwa tajiri huku dsm. Kumbe wee ni kibaka
 
Ungeweka kijiwe kwenye kasenta hapo kijijini, ungekuwa unakula hela zao; ila changamoto ya bush, mzunguko wa fedha ni mdogo.
 
sasa mkuu kama ulikuwa na ujuzi wa ufundi kwa nini uliondoka mjini??
 
Arusha ni kijijini?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Maana yake nimeondoka kijijiniShida broo kijiji chetu sh
kuna kaujinga fulani unako nilivo kusoma.
kijijini kutengeneza jina mpaka kufanikiwa kunachukua mda na mda ukifika basi kila mtu hata kupa kazi wewe na si mwingine.
kijijini unaweza kuanza na ziro na ukafikia kuwa hero.sababu mtaji utakuwa haraka mda unavozidi kwenda na utakuwa na ushindani mdogo.
kijijini unaweza kuwa wewe ndio muhasisi hapo nenda vijiji vingi utakuta walioanzisha kitu ndio matajiri wa hapo vijijini.
ida kubwa ni mtandao wa.interneti maana ujuzi wa siku hizi unategemea saana mtandao pia
 
Maisha yapo kichwani mwako. Fursa moja ikigoma jaribu zingine. Popote penye watu pesa ipo ni wewe tu kuangalia jinsi ya kuivuta kwako usave Ili uwekeze.
 
kuna kaujinga fulani unako nilivo kusoma.
kijijini kutengeneza jina mpaka kufanikiwa kunachukua mda na mda ukifika basi kila mtu hata kupa kazi wewe na si mwingine.
kijijini unaweza kuanza na ziro na ukafikia kuwa hero.sababu mtaji utakuwa haraka mda unavozidi kwenda na utakuwa na ushindani mdogo.
kijijini unaweza kuwa wewe ndio muhasisi hapo nenda vijiji vingi utakuta walioanzisha kitu ndio matajiri wa hapo vijijini.
Na wengi wao huwa ni wageni sababu huja na mawazo mapya kupitia fursa wanazoziona.
 
Na wengi wao huwa ni wageni sababu huja na mawazo mapya kupitia fursa wanazoziona.
Shida babu ni internet na usafiri wa gari moja kwa siku kwenda mjini
 
Back
Top Bottom