Nilijikuta naishi maisha ambayo sikuyategemea ila sina jinsi

Mwanamke bado ana maumivu makali sana, ex husband alitakiwa atumie ndugu watu wazima sana wa karibu wa mwanamke ili wamtafute ndugu yao waongee nae taratibu kwanza kwa upole na kumtangulizia ombi la msamaha...mwanamke yupo sawa 100% kawa wazi kuonyesha chuki na hasira yake kwa baba watoto wake kwa aliyomtendea...kinachomtesa mwanaume kwasasa ni kuona kuwa mama watoto wake mbona hamtafuti kulia shida,nani anampa kiburi, mbona anaishi,mbona aombi ombi kwa ndugu na jamaa au yule mtoto anayehisi sio wake mbona hajasikia kachukuliwa na baba yake?
Ndoa zina mambo mengi yaliyojificha.
 
Hivi ulimalizia mkuu?

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Niliachana na aliyekuwa mume wangu miaka 5 imepita, kuachana kwetu kulikuwa kubaya sana kwa mambo mabaya yaliyopita katikati yetu. Sipendi kuyaeleza maana ni mabaya ila nilishayasahau na kuyaacha yapite.
Usiniambie baada ya haya unataka kurudi kwa mumeo aisee songa mbele kama hakujua thamani yako Jana Leo ataijuaje zaidi atakurudisha kwenye maumivu Yale yale usijaribu piga moyo konde tafuta vibarua vingne zaidi
 
Bila mwanaume kuleta mrejesho hapa wewe ndio utabaki kuwa tatizo la kuachana na mwanaume wako kwenye jamii na ukoo mzima baada ya kipato cha mwanaume kilipo pungua..

Tutakuamini endapo upande wapili utakua live hapa na sio vinginevyo
 
Pole sana dada..
Tuombe MwenyeziMungu atajalia kheri watoto watakuwa pamoja na mitihani unayopitia.
kuna watu humu wameshakariri wanawake huwa ndo chanzo cha matatizo katika ndoa .kiasi kwamba hata ujieleze vp bado utaonekana we ndo mwenye makosa .
wanasahau kuwa kuna wanaume wengine pia wanaweza kuwa chanzo cha kuharibika ndoa .
Mf. kuna dada namjua kaolewa tu amemaliza form six..Mwanaume alimkataza asifanye shughuli yoyote na kamzalisha watoto watatu fast fast.
mwanaume akapata pesa zaid Kaenda kuoa.
Mdada wa watu maskini kaumia sana..matumizi yakapungua mpaka basi..na hapo kumbuka bado hataki afanye kazi au biashara .
dada watu anavumilia haya kaenda kuongeza mke wa tatu ..ndo ikawa balaa .
mwanamke mpaka analia machozi..kiukweli kuna wanaume wana roho mbaya sana. humtunzi mtu vizuri halafu hutaki ajitafutie kipato cha ziada.
Sasa kwa mfano huo utasema mwanamke ndo mbaya au tamaa na roho mbaya tu.
Ila fimbo aliyoipata ..kasimamishwa kazi na madeal yote yameisha ..mke mdogo kashaondoka ..wa pili nae yuko mbioni.
Sa hivi linabaki linamwambia mkewe ..we ndo unapenda kwa dhati . eti afungue moyo ridhiki zirudi.
Yaan unampa salute mwanamke mwenzangu si kwa kuvumilia kule.
Mwisho kwenye mahusiano mwanamke au mwanaume anaweza kuwa chanzo cha kuharibu. na haswa anapoingia mtu wa tatu ..michepuko.
 
Ni ujinga sana kukosoa kile mtu amekisema ata kama alikosea mmewe siyo kuacha watoto kuna wanaume wajinga sana kuisi kumbwagia mwanamke watoto ndyo kumkomesha
Ushafikiria unapambana na familia kuitunza afu mtu mmegombana anakuambia wewe mwanaume gani kwanza watoto sio wako na maneno kibao mimi naungana na wote wanaosema mwanamke atoe sababu
 
People should vent😔
The struggle is real.

M/Mungu akawe dira yako kila unaposafiri kifikra, Inshallah 🙏
 
Chai
 
Nimejaribu kuvaa viatu vyako nimeshindwa kabisa. Naishia hapa kwa leo
 
PAMOJA NA YOTE USILUDI KWA HUYU BABA KAMWE,
MUNGU HATOKUACHA
 
Vipi kuhusu story ya shetani, imekaajee maana apa Ni story ya upande wa mungu tu.
 
Hili jina lako mbona namjua Mtu anaitwa hivyohivyo yaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…