Kuna tatizo mahali,
Mwanzo mwisho wa Hii stori mwanamke anaongelea kugharamia matumizi yote panapohitajika pesa.
Mwishoni kabisa Anashauri wanawake waolewe na wanaume wachapakazi.
Ukirejea mwanzoni, anatumbia mwanaume wake aliachishwa kazi (he was jobless).
Ila kuna mahali kasema yeye alikua na kazi ilokua inampa kipato cha kutosha mpk Cha kugharamia nyumbani, Pete, HARUSI na ndoa n.k
Ila sijaona kokote alikoonyesha juhudi za kumkwamua mwanaume wake kiuchumi ili wasonge wote mbele.
angalau kusema kamtaftia mtaji afungue genge, au kumuunganisha na kazi fulani jamaa akagoma kwenda kuifanya.
Mtoa mada Ni Aina ya wanawake wanaotaka mwanaume FINISHED PRODUCT.
Ni mwepesi Sana wa kulaumu mwenzie kutokua na kazi au kujishughulisha.
Wakati hajampa nyenzo wala Njia yoyote ya atokee wapi.
Mtoa mada
Ni sawa na kina ndugai wanaposema vijana wajiajili, serikalini hamna ajira. Wakati hawajawatengenezea nyenzo yoyote wahitimu Hawa kujiajili.