Nilijinunulia Pete, Nikagharamia harusi mwenyewe, Ndoa ikafa baada ya miezi minne

Nilijinunulia Pete, Nikagharamia harusi mwenyewe, Ndoa ikafa baada ya miezi minne

Kuna tatizo mahali,

Mwanzo mwisho wa Hii stori mwanamke anaongelea kugharamia matumizi yote panapohitajika pesa.

Mwishoni kabisa Anashauri wanawake waolewe na wanaume wachapakazi.

Ukirejea mwanzoni, anatumbia mwanaume wake aliachishwa kazi (he was jobless).

Ila kuna mahali kasema yeye alikua na kazi ilokua inampa kipato cha kutosha mpk Cha kugharamia nyumbani, Pete, HARUSI na ndoa n.k

Ila sijaona kokote alikoonyesha juhudi za kumkwamua mwanaume wake kiuchumi ili wasonge wote mbele.

angalau kusema kamtaftia mtaji afungue genge, au kumuunganisha na kazi fulani jamaa akagoma kwenda kuifanya.

Mtoa mada Ni Aina ya wanawake wanaotaka mwanaume FINISHED PRODUCT.

Ni mwepesi Sana wa kulaumu mwenzie kutokua na kazi au kujishughulisha.
Wakati hajampa nyenzo wala Njia yoyote ya atokee wapi.

Mtoa mada
Ni sawa na kina ndugai wanaposema vijana wajiajili, serikalini hamna ajira. Wakati hawajawatengenezea nyenzo yoyote wahitimu Hawa kujiajili.
Mmh
 
Hahah!ila hata mwamba kakazaa sanaa...we shangaa mwanamke ni mtu wa kuficha sanaa tabia zake ila hapa kajitanabahisha kuwa mtaani alikuwa kapewa jina la mdomo pistol....imagn mwamba alikuwa anaishije na hicho kiumbe?
Mwamba kakomaa kweli yani! Mie Dem mropokaji hatuvuki hata kigamboni😂
 
  • Kicheko
Reactions: BRB
Hii kwa wanaume wenzangu tutafute pesa..... leo dada kashidwana na mwenzie kamwaga mchele huku jf hadi na picha!!! Hii ni aibu kubwa sana kw sisi wanaume na pia kabla hamjaingia kwenye ndoa chunguza sana familia unayotaka kuoa na mwanamke unaetaka kumuoa’!! Usioe tu kwasababu ananipenda hapana chunguza mambo ya msingi,!! Mambo ambayo mkifanyiana Kwa upendo wenu wenyewe mwisho wa siku yanaweza kukuumiza na ukajifanya vibaya! Narudi kwa dada apo kwanza pole kwa changamoto, lakini nashidwa kutoa ushauri kwasababu kesi hatujasikiliza na upande wa pili unaseamaje.... pili umekosea kwann unaweka picha za mwenzio humu ivi ndo mlivyo kubaliana? Niliwai kusema ndoa Sio mahusiano kuishi maisha ya ndoa kuna hitaji mapenzi ya kweli na mapenzi ya kweli no regret..... sijui nilifanya ivi na vile ulifanya Kwa upendo basi ilo libaki na kuheshimiwa ivyo!!!! Kwenu kina dada wote sisi wanaume mki tucheat ukweli kabisa ili tendo hatuwezi kusamehe tegemea vurugu uko ndani kwako, mkiona mmefika hatua yakucheat make sure mwenzi wako asijue akijua ilo gubu lake sio la kawaida na litawacost!!!! Uyu jamaa kimemuuma wewe kucheat ndo sababu kila wakati anakukumbusha tafsiri yake kashidwa kusamehe ilo!!!!! Polee Sana rafiki lakn jikaze yatapita na maisha lazima yaendelee
 
Inaonekana jamaa hana hela tu lkn vingine yuko vizr hadi ugharamie vyote ivyo kwake tu ,pia akubali kurudi kwako tena n anakupenda sana kaa fikria upya , alaf wanaume huwa hatupigi wanawake tusiowapenda ,ni kama tu ku'kukumbusha mm cio dada ako ,unajisahau kuwa na hela hakufanyi mwanaume ,
 
Kilichomshinda mwanaume mwenzio ,ww nae mwanaume tu hawa ma' single mothers wengi wao n lazima wawe na usugu fulani,
 
Ninachoamini mimi, mwanamke mtulivu ni dawa ya mambo yote. Mie mwanaume hutulia hata kama niko vipi! Mwanamke hata ukijinunulia pete, mpe hela mwanaume, jitolee mahali, aisee ni kazi bure kama huna utulivu!

Mwanamke Limbukeni na Asiye mtulivu kiukweli mimi kwangu hao ni maadui!
 
Nimesoma yote ila tatizo una mdomo pistol hakuna mwanaume anataka kuishi na mwanamke mdomo pistol kama wako,kutokana na Domo lako nahisi ukawa una msimanga jamaa kisa hana kazi kipigo ndo kilikua size yako na hilo Domo lako pistol
 
Mume wangu tulikutana chuo, mimi nikiwa na miaka 20, yeye 21. Tukaanza kuishi pamoja kama mke na mume.

Tulikuwa tukiandika majarida mitandaoni ndo tunapata pesa ya kujitunza wenyewe, na ndo pesa nilimsomeshea mdogo wangu kwani mama alikuwa mgonjwa na tuliishi maisha duni sana. Mimi na mume wangu tulilelewa na mama pekee.

Ikatokea kozi aliyokuwa anasoma mwenzangu kuwa na shida, wote waliokuwa wanaisoma wakasimamishwa masomo kwa muda, na kulikuwa na kesi mahakamani. Lakini baadae ilirudishwa na wenzake walirudi shule lakini yeye hakurudi, kwahiyo hakumaliza chuo. Nafikiri pia pesa aliyokuwa akipata wakati huo ilimfanya asirudi chuo.

Me nilisoma nikamaliza. Sikukaa muda mrefu nikapata kazi. Huku mwenzangu kazi ya uandishi ilianza kusuasua, mara asiandike, kwahiyo me nikawa ndo nalipia matumizi yote nyumbani.

Nikasema itakuwa wakati muafaka kuzaa, labda tukipata mtoto atapata moyo wa kutafuta kwa bidii. Tukapata mtoto, lakini mambo yalikuwa yaleyale. Mimi huku nako niliendelea kuchakarika, kuanzisha biashara n.k.

Nilichogundua, mwanaume akiwa hana kitu chake/pesa yake anakuwa hajiamini kabisa.

Basi hapo akaanza ku cheat. Me mwenyewe kusema ukweli nili cheat pia, maana unaenda kazini unakutana na wanaume wachapakazi unarudi nyumbani unamuona mwenzako kakaa tu unawaza huyu vipi! Tukaenda hivyo baadae baada ya kugunduana tukakaa kuongea, tukasameheana tukakubaliana tuanze upya.

Lakini mambo yalikuja kuwa mabaya zaidi, alininyanyasa kihisia na mwishowe alikuwa akinipiga.

Tukaamua tuachane, hiyo ni baada ya miaka tisa ya kuwa pamoja. Akaondoka nyumbani. Kwakweli nilivurugwa sana. Nilihisi amenipotezea muda mwingi, kanikuchua Nina miaka 20 kaniacha nina 29.

Nikawa mtu wa pombe. Narudi nyumbani saa nane usiku na asubuhi naenda kazini yani sijui niliwezaje kufanya kazi. Nikawa na mahusiano kadhaa, mmoja hadi aliniingiza kwenye utumiaji wa madawa.

Baada ya miaka miwili ya hayo maisha nikasema huku nje sio! Bora kurudi kwa shetani ninayemjua. Na hilo lilikuwa kosa kubwa sana nililofanya. Basi tukarudiana na huyo mume wangu, ambaye bado alikuwa Hana kazi.

Hapo mimi nikawa nimeokoka. Nikasema haya mahusiano tusirudishe yalivyokuwa, tuanze upya kama Mungu anavyotaka. Basi tukajiunga kwenye darasa la wanaotarajia kuingia ndoani.

Tukapanga siku ya harusi. Nikawa nampa pesa alipie vitu hadi mahari, maana huwa tunaambiwa kumfichia mwanaume aibu unampa yeye hela ndo atoe.

Nilijinunulia Pete nikampa, siku mmoja tulienda mgahawani akanivalisha. Kwahiyo mitandaoni mtu anaona tu nimevalishwa Pete hajui story.

Nilikuwa very desperate kwakweli, na nilifanya hivyo kwasababu kwanza niliona maisha huko nje sio, na pili nilitaka mwanangu awe na familia iliyokamilika. Harusi ilinimalizia akiba yangu yote.

Basi tukafanya harusi, tukaanza kugombana huko huko honeymoon! Kurudi nyumbani tena manyanyaso yalizidi.

Nikiri kuwa wote na mume wangu tuna tatizo la hasira, tena me wananiitaga mdomo pistol maana maneno yanayonitoka nikikasirika ni kama pistol.

Alikuwa akininyanyasa kihisia kwa kunikumbusha makosa yangu ya zamani kila mara. Vipigo vilizidi hadi mama yangu ambaye alikuwa amekuja kuishi na sisi akasema hataki kuishi hapo arudishwe kwao.

Tulijaribu counseling, pastor wetu alijitahidi sana kusaidia ndoa yetu. Unakuta baada ya misa anatuita, ananiambia ukirudi nyumbani wewe fanya hivi na hivi lakini tukifika nyumbani unaibuka ugomvi, ananipiga hadi majirani wanaamka.

Mtoto naye niliitwa shuleni nikaambiwa anaongea sana kuhusu kupigana, kwamba anaogopa anataka kumlinda mama yake lakini hajui amlindeje. Wakamuanzishia therapy shule. Na kazini kwangu pia kuna huduma ya counseling nilimpeleka.

Alipata therapy kwa miezi kadhaa na alianza kupona maana aliacha kuuliza kama nitarudiana na baba na siku moja therapist wake alimwmbia achore picha ya familia yake, akajichora yeye na mimi tu.

Sasa hivi tunaweza kuangalia picha za baba yake tukamuongelea vizuri. Kabla ilikuwa akiona picha ya baba anaanza kulia. Inauma sana kuona mwanao anaumia, bora ingekuwa kaumia mwilini ungesema ngoja nimpake hiki, lakini kihisia hujui ufanye nini!

Baba yake niliachana naye baada ya kujua kuna mwanamke mwingine, ex wake.

Ndo nikasema haiwezekani juhudi zote nazofanya, nimejitahidi kubadilika, kuomba msaada kanisani, nikawa mtu wa sala asubuhi mchana jioni ni kuomba tu Mungu aiponye ndoa yangu, nalipia bills zote, yeye kutwa kunikumbushia makosa yangu ya nyuma, halafu kumbe ana mwanamke mwingine!!! Nisingejua kuhusu huyo mwanamke nafikiri bado ningekuwa naye. Nikamwambia aondoke. Hiyo ni miezi minne tu baada ya harusi.

Wakati tunafunga harusi binafsi nilikuwa na furaha. Lakini niliwahisha mambo, hatukukaa kufikuria kwanini mahusiano yalishindikana mara ya kwanza. Kwakweli kufanya harusi haiondoi matatizo kwenye ndoa au mahusiano yenu.

Niliumia sana kuachana naye, hasa baada ya kufanya harusi kubwa miezi minne tu iliyopita. Nilikuwa silali. Nilikuwa na mawazo ya kujiua. Nikaanza kupata anxiety attacks.

Nikaenda hospitali nikaanza kupewa dawa na kufanya therapy kwa miezi kadhaa. Mawazo ya kujiua yamepotea. Nimekubali kuwa nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuokoa ndoa yangu.

Nikajiunga na divorce classes, yanasaidia kukabiliana na hisia zinazokuja na talaka kama Uoga, hasira, Upweke. Ni ngumu kujifunga huko tena baada ya miezi minne tu ya ndoa, unawaza utaambiwa na watu Mungu hapendi talaka. Sawa hapendi talaka lakini anampenda yule mtaliki.

Najihisi nimekuwa mtu bora zaidi, Najua nilipokosea, Najua ninachotaka kwenye mahusiano.

Sisemi kwamba ikitokea shida udai talaka. Pigania ndoa yako. Ipiganie mpaka hata Mungu akishuka aseme kweli ulifanya hiki na hiki na hiki. Ukiona imefika mwisho, achana nayo. Talaka sio mwisho wa maisha.

Mimi naona mume mzuri ni mwanaume anayemjua na anayeongozwa na Mungu kwasababu huyo atajua jinsi ya ku behave. Awe mchapakazi na Anayechukulia maagano ya ndoa kwa uzito.

Nilikuwa nashangaa Tz nani ana muda wa ushauri nasaha Kwa matatizo ya mtu baki?
 
Da mdomo pistol mimi siwez kuvumilia kwa kweli nina hasira za karibu sana sipendi mwanamke talkative
Bullying sipendi tutauana bure
 
Ukizingatia jamaa ana stress za kuyumba kiuchumi

Nadani Tatizo kupigwa makofi kila Mara,
Nadhan chanzo Kiko hapa Hapa[emoji116]

"tena me wananiitaga mdomo pistol maana maneno yanayonitoka nikikasirika ni kama pistol....."
Na wanawake wengi shida inakuwaga hapo tu. Mwanamke mwenye tabia hizo namuogopa kama ukoma. Kama una tabia hizo za mdomo mdomo. Pamoja na yote uliyopitia sikuonei huruma. Ni size yako. Ndoa yako uliivunja kwa mikono yako
 
Wanawake uwa wanakosea mahusiano yao kwa ku-cheat tu,si rahis Mwanaume kuvumilia hilo suala.Ata akikusamehe,atabaki na kovu ambalo ukiligusa tu unalitonesha.
 
Tukasameheana

Sema Ukamsamehe.

Hayupo mwanaume timamu atakusamehe ukishamsaliti huyo sio mwanaume.

Wadada,mwanaume kamili hasamehi usaliti moja kwa moja.Akikusamehe usaliti ujue huna thamani km mwanzo,Ujue una mwanaume dhaifu sana,ujue atalipiza kwa namna nyingine.

Mwenye kusikia na asikie.Huo ndo udhaifu wa mwanaume.Tupo hivyo

Kama ambavyo mwanamke hawezi kutoa hela yake kwa mwanaume bila masimango.Wapo hivyo

Dada zangu ukisaliti ukastukiwa km upo kwenye mahusiano jua kbs ule upendo kwetu sisi haupo.Jua kbs 70% ya wanaume wanakuwa na chuki ambayo hata ukipata ajali kubwa au ukifa leo wanaweza sherekea kimoyomoyo.Huyo ndo mwanaume


Ila maendeleo yamekuja na wanaume dhaifu hili wadada litawasaidiA
Ndugu apa umemaliza asilimia 90.
 
Hongera umemove on. Mpk kuandika haya mean moyoni saizi unaamani ya kutosha. Bwana Yesu Asifiweeee. Sema Ameen!! Ubarikiwe
 
Unafaa sn kua mshaur sahii wa maswala ya ndoa.

Tukiongea wanaume tunaonekana tunawakandamiza na mfume dume,

Ila wanasahau kua nature Ndo imeselect iwe hivyo.
True Mimi mwenyewe ni mwanamke ila sipendi mambo ya ugomvi ugomvi na gubu, au kutukana kisa tumekoseana hyo huua kabisa mahusiano na kingine wanawake tu a midomo sana tukianza kuongea hatuna break na hapo ndio shida nyingine ilipo
 
Back
Top Bottom