Nilijinunulia Pete, Nikagharamia harusi mwenyewe, Ndoa ikafa baada ya miezi minne

Nilijinunulia Pete, Nikagharamia harusi mwenyewe, Ndoa ikafa baada ya miezi minne

Ubarikiwe sana mkuu,
hizi ndo busara Sasa wanawake mnatakiwa kufundishana.

Ndoa za Mashindano always hazinaga mwisho mzuri.

Umeongea point[emoji106]
Ni better mtu ukiwa na hasira unywe maji au utoke nje ukatembee mbali kuanza kurushiana maneno huharibu kabisa mambo. Hasira zikipungua ndio muongee
 
Mwanamke akishakuwa mchepukaji tu ndoa haiwezi kudumu lazima mikosi ije mfululizo. Kosa la kwanza ilikuwa kuchepuka kwa lengo la kushindana na mwanaume. Pamoja na mapungufu ya mwanaume lakini haikuwa suluhu kuamua kuchepuka bali kuleta mikosi maradufu.
 
Ukizingatia jamaa ana stress za kuyumba kiuchumi

Nadani Tatizo kupigwa makofi kila Mara,
Nadhan chanzo Kiko hapa Hapa[emoji116]

"tena me wananiitaga mdomo pistol maana maneno yanayonitoka nikikasirika ni kama pistol....."
Tatizo lipo hapo na Mambo ya wawili ukisikiliza upande mmoja uwezi pata ukweli ingawa ukisoma ukweli wake unaona hata yeye ni chanzo Cha matatizo yake. Wakati mwingine kwa Africa mtoto wa kike akienda shule ni Kama umezika ndoto zake sio wote lakini. Mungu tusaidie
 
Mdomo pistol'uzinzi na jeuri...hakuna mwanaume anayaweza kuvumilia. Ni story ya upande mmoja.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Youtubers kwa kutafuta viewers wapo vizuri! Huwa wanpenda story za kutunga
 
Huyu kinachomponza ni uzungu mwingi wakati yuko Africa,kitu kidogo tu Therapy,huku kwa Magu watu wanadundana na Therapy hawaendi na ndoa zinaendelea,ushauri punguza uzungu uwe kama mama yako utakaa kwenye ndoa,na kingine punguza huo mdomo pisto,hakuna mwanaume anayependa mwanamke wa kumpigia kelele(Vuvuzela)
Actually ukimsikliza kwenye hiyo interview mama yake naye hakuwa na historia nzuri, akaishia kwenye pombe za kupitia kiasi, mwishowe akapata pressure then kapata stroke kapooza upande, haongei. Huyo dada akawa anasema wazazi wetu walikuwa wakivumilia mengi na hawakuwa open Kwa therapy, Bora yeye alikuwa mrahisi kutafuta msaada ambao umemsaidia sana, na anapendekeza therapy.
 
Wanawake wa hivi huwalisha Sana sumu watoto wao wawachukie baba yao bill sababu.

Unakuta mtoa mada kamfukuza mwenyewe baba mtoto wake.

Ila akikaa na mwanae atamlisha sumu kua baba ako hakukujali Wala kukulea, alkua anaendekeza starehe.

Mwisho wa siku mtoto anamuona baba Kama mtu mmoja mbaya sana.
Kama umesikiliza interview au kusoma nilichoandika, clearly huyo mama hamesemei baba mtoto vibaya. Stop generalizing and demonizing people.
 
Mume wangu tulikutana chuo, mimi nikiwa na miaka 20, yeye 21. Tukaanza kuishi pamoja kama mke na mume.

Tulikuwa tukiandika majarida mitandaoni ndo tunapata pesa ya kujitunza wenyewe, na ndo pesa nilimsomeshea mdogo wangu kwani mama alikuwa mgonjwa na tuliishi maisha duni sana. Mimi na mume wangu tulilelewa na mama pekee.

Ikatokea kozi aliyokuwa anasoma mwenzangu kuwa na shida, wote waliokuwa wanaisoma wakasimamishwa masomo kwa muda, na kulikuwa na kesi mahakamani. Lakini baadae ilirudishwa na wenzake walirudi shule lakini yeye hakurudi, kwahiyo hakumaliza chuo. Nafikiri pia pesa aliyokuwa akipata wakati huo ilimfanya asirudi chuo.

Me nilisoma nikamaliza. Sikukaa muda mrefu nikapata kazi. Huku mwenzangu kazi ya uandishi ilianza kusuasua, mara asiandike, kwahiyo me nikawa ndo nalipia matumizi yote nyumbani.

Nikasema itakuwa wakati muafaka kuzaa, labda tukipata mtoto atapata moyo wa kutafuta kwa bidii. Tukapata mtoto, lakini mambo yalikuwa yaleyale. Mimi huku nako niliendelea kuchakarika, kuanzisha biashara n.k.

Nilichogundua, mwanaume akiwa hana kitu chake/pesa yake anakuwa hajiamini kabisa.

Basi hapo akaanza ku cheat. Me mwenyewe kusema ukweli nili cheat pia, maana unaenda kazini unakutana na wanaume wachapakazi unarudi nyumbani unamuona mwenzako kakaa tu unawaza huyu vipi! Tukaenda hivyo baadae baada ya kugunduana tukakaa kuongea, tukasameheana tukakubaliana tuanze upya.

Lakini mambo yalikuja kuwa mabaya zaidi, alininyanyasa kihisia na mwishowe alikuwa akinipiga.

Tukaamua tuachane, hiyo ni baada ya miaka tisa ya kuwa pamoja. Akaondoka nyumbani. Kwakweli nilivurugwa sana. Nilihisi amenipotezea muda mwingi, kanikuchua Nina miaka 20 kaniacha nina 29.

Nikawa mtu wa pombe. Narudi nyumbani saa nane usiku na asubuhi naenda kazini yani sijui niliwezaje kufanya kazi. Nikawa na mahusiano kadhaa, mmoja hadi aliniingiza kwenye utumiaji wa madawa.

Baada ya miaka miwili ya hayo maisha nikasema huku nje sio! Bora kurudi kwa shetani ninayemjua. Na hilo lilikuwa kosa kubwa sana nililofanya. Basi tukarudiana na huyo mume wangu, ambaye bado alikuwa Hana kazi.

Hapo mimi nikawa nimeokoka. Nikasema haya mahusiano tusirudishe yalivyokuwa, tuanze upya kama Mungu anavyotaka. Basi tukajiunga kwenye darasa la wanaotarajia kuingia ndoani.

Tukapanga siku ya harusi. Nikawa nampa pesa alipie vitu hadi mahari, maana huwa tunaambiwa kumfichia mwanaume aibu unampa yeye hela ndo atoe.

Nilijinunulia Pete nikampa, siku mmoja tulienda mgahawani akanivalisha. Kwahiyo mitandaoni mtu anaona tu nimevalishwa Pete hajui story.

Nilikuwa very desperate kwakweli, na nilifanya hivyo kwasababu kwanza niliona maisha huko nje sio, na pili nilitaka mwanangu awe na familia iliyokamilika. Harusi ilinimalizia akiba yangu yote.

Basi tukafanya harusi, tukaanza kugombana huko huko honeymoon! Kurudi nyumbani tena manyanyaso yalizidi.

Nikiri kuwa wote na mume wangu tuna tatizo la hasira, tena me wananiitaga mdomo pistol maana maneno yanayonitoka nikikasirika ni kama pistol.

Alikuwa akininyanyasa kihisia kwa kunikumbusha makosa yangu ya zamani kila mara. Vipigo vilizidi hadi mama yangu ambaye alikuwa amekuja kuishi na sisi akasema hataki kuishi hapo arudishwe kwao.

Tulijaribu counseling, pastor wetu alijitahidi sana kusaidia ndoa yetu. Unakuta baada ya misa anatuita, ananiambia ukirudi nyumbani wewe fanya hivi na hivi lakini tukifika nyumbani unaibuka ugomvi, ananipiga hadi majirani wanaamka.

Mtoto naye niliitwa shuleni nikaambiwa anaongea sana kuhusu kupigana, kwamba anaogopa anataka kumlinda mama yake lakini hajui amlindeje. Wakamuanzishia therapy shule. Na kazini kwangu pia kuna huduma ya counseling nilimpeleka.

Alipata therapy kwa miezi kadhaa na alianza kupona maana aliacha kuuliza kama nitarudiana na baba na siku moja therapist wake alimwmbia achore picha ya familia yake, akajichora yeye na mimi tu.

Sasa hivi tunaweza kuangalia picha za baba yake tukamuongelea vizuri. Kabla ilikuwa akiona picha ya baba anaanza kulia. Inauma sana kuona mwanao anaumia, bora ingekuwa kaumia mwilini ungesema ngoja nimpake hiki, lakini kihisia hujui ufanye nini!

Baba yake niliachana naye baada ya kujua kuna mwanamke mwingine, ex wake.

Ndo nikasema haiwezekani juhudi zote nazofanya, nimejitahidi kubadilika, kuomba msaada kanisani, nikawa mtu wa sala asubuhi mchana jioni ni kuomba tu Mungu aiponye ndoa yangu, nalipia bills zote, yeye kutwa kunikumbushia makosa yangu ya nyuma, halafu kumbe ana mwanamke mwingine!!! Nisingejua kuhusu huyo mwanamke nafikiri bado ningekuwa naye. Nikamwambia aondoke. Hiyo ni miezi minne tu baada ya harusi.

Wakati tunafunga harusi binafsi nilikuwa na furaha. Lakini niliwahisha mambo, hatukukaa kufikuria kwanini mahusiano yalishindikana mara ya kwanza. Kwakweli kufanya harusi haiondoi matatizo kwenye ndoa au mahusiano yenu.

Niliumia sana kuachana naye, hasa baada ya kufanya harusi kubwa miezi minne tu iliyopita. Nilikuwa silali. Nilikuwa na mawazo ya kujiua. Nikaanza kupata anxiety attacks.

Nikaenda hospitali nikaanza kupewa dawa na kufanya therapy kwa miezi kadhaa. Mawazo ya kujiua yamepotea. Nimekubali kuwa nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kuokoa ndoa yangu.

Nikajiunga na divorce classes, yanasaidia kukabiliana na hisia zinazokuja na talaka kama Uoga, hasira, Upweke. Ni ngumu kujifunga huko tena baada ya miezi minne tu ya ndoa, unawaza utaambiwa na watu Mungu hapendi talaka. Sawa hapendi talaka lakini anampenda yule mtaliki.

Najihisi nimekuwa mtu bora zaidi, Najua nilipokosea, Najua ninachotaka kwenye mahusiano.

Sisemi kwamba ikitokea shida udai talaka. Pigania ndoa yako. Ipiganie mpaka hata Mungu akishuka aseme kweli ulifanya hiki na hiki na hiki. Ukiona imefika mwisho, achana nayo. Talaka sio mwisho wa maisha.

Mimi naona mume mzuri ni mwanaume anayemjua na anayeongozwa na Mungu kwasababu huyo atajua jinsi ya ku behave. Awe mchapakazi na Anayechukulia maagano ya ndoa kwa uzito.

Mtuleteage true story sio kutafsiri story za watu, ala!!!
 
Nadhani una msongo wa mawazo ni wapi nimeandika Mwanaume aki cheat nami ni cheat acha Ungese nitakutia pumbavu [emoji1610]
[emoji91][emoji16][emoji16][emoji16][emoji122][emoji122][emoji122][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji112]
 
Kama umesikiliza interview au kusoma nilichoandika, clearly huyo mama hamesemei baba mtoto vibaya. Stop generalizing and demonizing people.
Jamaa hakua tayr kuoa ndo maana hajagharamua chochote mpaka Ndoa inakamilika.
 
Na Kuna wengine wanavumilia na Mambo yanakuwa mazuri to yeye . Kuna jamaa yangu wa karibu alikuwa kicheche na mlevi balaa. Mke kavumilia karibia miaka 10 anasali anamwombea mme wake. Ghafla mme kabadilika, Kawa mtulivu mtu wa kujali familia kaachana na maovu Yale.
Kila mtu alishangaa tukabaki kuitukuza utukufu wa aliye juu. Hakika atakayevumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka.
Ha ha haa,sawasawa
 
Back
Top Bottom