Zamani nikiishi kwa baba angu mdogo, alkua dreva pale Ofisi ya rais-magogoni.
Alkua na MKE wake akifanya kazi pale bandar.
Jpm alipoingia Ikulu,
Jamaa akawa demoted hadi Kua dreva Tamisemi.
Aisee alipitia kipind kigumu Sana KIUCHUMI, ukzingatia alkua mtu wa Bata Sana.
Alkua na kitambi, kilikata chote.
Baadae (2018) akaja rudishwa nafas yake kule kule Ikulu, aisee mambo yalirudu Kama mwanzo.
Ila alichofanya ndani ya wiki TU ya kuanza kazi,
Mzee alimuachisha kazi MKE wake pale bandar, Tena kwa ukali na akampiga adi boss wake mkwara Kama akiendelea na kazi watafikishana pabaya.
Nilimuona Kama mzee muonevu Sana.
Ila nilivokua mkubwa,
Nilikuja gundua aisee huenda mzee alikua sahii japokua hajawai nambia sababu hasa za kumuachisha ile kazi.