Nilijua hajui ila nimefanikiwa kupindua meza

Nilijua hajui ila nimefanikiwa kupindua meza

Sheffer95

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2020
Posts
211
Reaction score
515
Habarini za muda huu wanajamii forum pole na majukumu mazito ya ujenzi wa taifa.

Iko hivi hizi siku za hv karibuni nimeona mabadiliko makubwa kwa mwandani wangu wa muda mrefu, moja amekuwa mkimya sana na kukosa ile nuru na uchangamfu ambao alikuwa nao sikuzote, pili pindi niwapo mbali amekuwa na taboa ya kutokujibu sms na muda mwingie hata simu nikimpigia kujua Hali ya hapo nyumbani ikoje. Sasa niliporudi ikabidi nimuweke chini nimueleze juu ya tabia hizi na kwamba Nina mpango nimrudishe kwao akapumzike na kujitafakari upya, ndipo alipo niambia

Anhaaa hongera naona unataka kunirudisha nyumbani ili uvinjali na mchepuko wako ..xxxx... aisee mwanaume nikashtuka na kijasho Chembamba kikaanza kunitoka kwamba amemjuaje huyo mtu na mbona mm nipo makini sana?

Akaanza kuniambia huyo mtu sehemu anapoishi, duka lake lilipo ambalo anahisi nimemfungulia, na mambo mengine mengi kumhusu mtu huyo mpaka nikashangaa na akaniambia ni kama miezi 6 sasa toka ajue na kufuatilia. Aiseeee ikabd kwanza nimkazie na kumwambia kwann hqkuniuliza mida wote huo na kuendelea kunijudge wakati mtu huyo ni rafiki tu ambae huwa tunataniana na kwamba huyo ana mtu wake pia mm siwezi toka na mtu kama huyo nikajitetea pale nashukuru amenielewa na nimemuonya kuacha kuweka vitu moyoni badala yake aulize, hivyo nawashauri wanaume we zangu tuwe makini sana hatuwezi jua hawa viumbe emotions zikiwapanda watafanya nn.

Anyway kumridhisha zaidi leo weekend nilimtoa out na kuweka mambo Sawa na kuzungumza zaidi mipango yetu mikubwa na namnq tupambanie kufanikisha sio kusikiliza maneno ya uchonganishi na umbea huko nje
 
images(23).jpeg
 
Hamna wanawake wagumu kuliwa kama wacha Mungu wakweli.

Kua karibi na Mungu, kunamuondolea Roho ya kisasi +Ashiki anakua hana.


Tofauti nahawa wengine.
Na hamna wanawake wenye nyege za karibu sana kama Hawa watu.huko kwenye hofu ya mungu wanafanya vichaka tu

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo letu wanawake tukishajua una saliti hata ufanye nini huwezi kurudisha ile thamani ya mapenzi kama awali, kuna dharau fulani na roho ya kisasi inakuwa ndani kwetu, kichwani kwetu kuna kuwa na why?? Nyingine, unakuwa huaminiki tena. Kuna zile wanaita butterflies zinaondoka unakuwa kama hisia kinamna fulani kama zimekata.

Yan usitegemee yale mapenzi haswa yatakuwepo kilichobakia ni ku fake upendo maisha yasonge. Msichojua wanaume ndio hicho yan tukishagundua kuna usaliti mapenzi yetu kwenu hayawezi kuwa kama awali never yan kama ni penzi linakuwa limeshakufa kinachobakia ni mazoea tu.

Kabla hujafanya usaliti fikiria hizi consequences maana Moyo wa mwanamke ukishaumia unaweza kuamua lolote lile na huwezi kamweeee kurudisha upendo kama awali. Mwisho wa siku unaharibu nyumba yako kwa mikono yako na tamaa za michepuko ambayo wala haina thamani nawe isipokuwa inatizama pochi yako, unakosa mapenzi ya dhati kwa mwanamke wako sababu anakuona mshenzi tu. Mwisho wa siku una kosa mapenzi kwa michepuko (Pochi) na kwa mkeo (Usaliti). Ndoa nyingi za kiafrika zimebakia katika hali ya mazoea tu.
 
Maana yangu ukiwa na hofu na Mungu, utachukia uovu wa aina yoyote, Utakua karibu na Mungu kimawasiliano.

Na kwa muktadha huo. Mungu anakua ndani yako, na ndan ya nyumba yako.
Mimi nachukia uovu, lakini sina hofu na mungu na wala siko karibu na mungu wala sihitaji kuwa karibu yake ili nichukie uovu.
Hii inaonyesha mungu hana jipya amefulia.
 
Habarini za muda huu wanajamii forum pole na majukumu mazito ya ujenzi wa taifa
Iko hv hizi siku za hv karibuni nimeona mabadiliko makubwa kwa mwandani wangu wa muda mrefu, moja amekuwa mkimya sana na kukosa ile nuru na
Mwamba huyu mkeo lazima aliwe.

JIANDAE TU KISAIKOLOJIA.

"Nafsi iliyoumizwa hutafutakulipiza kisasi""

#YNWA
 
Back
Top Bottom