Tatizo letu wanawake tukishajua una saliti hata ufanye nini huwezi kurudisha ile thamani ya mapenzi kama awali, kuna dharau fulani na roho ya kisasi inakuwa ndani kwetu, kichwani kwetu kuna kuwa na why?? Nyingine, unakuwa huaminiki tena. Kuna zile wanaita butterflies zinaondoka unakuwa kama hisia kinamna fulani kama zimekata.
Yan usitegemee yale mapenzi haswa yatakuwepo kilichobakia ni ku fake upendo maisha yasonge. Msichojua wanaume ndio hicho yan tukishagundua kuna usaliti mapenzi yetu kwenu hayawezi kuwa kama awali never yan kama ni penzi linakuwa limeshakufa kinachobakia ni mazoea tu.
Kabla hujafanya usaliti fikiria hizi consequences maana Moyo wa mwanamke ukishaumia unaweza kuamua lolote lile na huwezi kamweeee kurudisha upendo kama awali. Mwisho wa siku unaharibu nyumba yako kwa mikono yako na tamaa za michepuko ambayo wala haina thamani nawe isipokuwa inatizama pochi yako, unakosa mapenzi ya dhati kwa mwanamke wako sababu anakuona mshenzi tu. Mwisho wa siku una kosa mapenzi kwa michepuko (Pochi) na kwa mkeo (Usaliti). Ndoa nyingi za kiafrika zimebakia katika hali ya mazoea tu.