Inawezekana. Nakumbuka wakati wa Nyerere, nchi kama USA, UK, Sweden nk walikuwa wakiteua mabalozi wa kuja Tanzania ambao ni makini sana, kwa sababu wakiwa yeboyebo Nyerere alikuwa anawaaibisha mno wanapokuwa na mazungumzo nae na hawaelewi mambo. Mwinyi alipoingia madarakani ndio tulianza kuletewa mabalozi ambao walikuwa wapowapo tu, kwa sababu hizo nchi ziliona ku-deal na president kama Mwinyi was a walk in the park.
Kwa hiyo Samia akijua mtu kama Mwabukusi ndio raisi wa TLS, atataka awe na mtu makini sana kama AG, la sivyo serikali itaaibika kila siku.
Kwa hiyo mtoa mada ana point, sio kwamba ewepo wa Mwabukusi TLS umemfanya Samia afanye haya mabadiliko, akijua Feleshi sio size ya Mwabukusi atafanya serikali iumbuke