Nilikamatwa na Polisi na kufichwa Kituo kilichopo Dar kwa siku tatu bila kula nikipewa vitisho

Nilikamatwa na Polisi na kufichwa Kituo kilichopo Dar kwa siku tatu bila kula nikipewa vitisho

Mwanaume unaanzaje kusema ulitaka kubakwa kituo cha Polisi?

Hadithi yake ina gapes kibao, kwanza Usalama wa Taifa hawajishughulishi na mambo ya arrest.

Na ikitokea Afisa usalama wa Taifa yuko joint venture na Polisi basi ujuwe hicho ni kikosi kazi kwa kazi maalum na hapo hakuna mizaha kama hii anayohadithia huyu jamaa.
Awamu iliyopita vitu hivyo vilikuwa normal sana .
 
Sitaandika yote kuficha kujulikana Kwasababu za usalama wangu na sitataja Kituo (mojawapo ya vituo vya police DSM) Kwasababu walio nifanyia hayo mateso, wapo na wanaendelea na utumishi wao kuumiza wa Tanzania.

Sitosahau mwaka 2021 mwezi March nilipokea simu ya mtu aliyejitambulisha kuwa ni mpemba ana kazi ya Ujenzi wa ghorofa nane anahitaji kuonana
Milioni 20 kwenye gari limepaki Polisi?
 
Ila Kuna watu wanajua kutesa wenzao duniani hapa sababu ya pesa jamani daah!! Pole mkuu..

Watu wenye pesa hasa za ulimwengu wa roho wanatesa sana. Ni pesa inaongea, umesikia " Mimi Sina sheria Nina pesa "
Huniwezi kipesa, kiuchawi wala kiserikali, nipe mkono.😁😁
 
Pole sana kama ni kweli, kwa niliyoyaona Dakawa inaweza kua kweli!

Haki ipo kwa mwenye pesa.
Mkuu Dakawa uliona nini? Nappafahamu pale kabla ya kuwa na kituo, nasikia kwa sasa kuna kituo cha Polisi kule ndani ndani, niliwahi kuishi kijiji kile na nilisoma pale darasa la kwanza mpaka la nne miaka ya 90 huko, kitambo sijafika.
 
Jamani ni 2022 funguka kila kitu weka majina na vituo vyao vya kazi unadhan ukificha ficha ndio inasaidia
Naomba kuuliza hivi vituo vya police hawawezi kuviweka kwa hali ya usafi na kutengeneza mazingira mazuri kiafya juzi kuna rafki aliwekwa aliniambia pachafu sana ,miaka kwenda uchafu ushapitwa na wakati kwanin pasiwe pasafi tu
Halaf police wanapenda rushwa mdhamana mpaka pesa ndio anatoa waweke camera
Siwapendi police
 
Sitaandika yote kuficha kujulikana Kwasababu za usalama wangu na sitataja Kituo (mojawapo ya vituo vya police DSM) Kwasababu walio nifanyia hayo mateso, wapo na wanaendelea na utumishi wao kuumiza wa Tanzania.

Sitosahau mwaka 2021 mwezi March nilipokea simu ya mtu aliyejitambulisha kuwa ni mpemba ana kazi ya Ujenzi wa ghorofa nane anahitaji kuonana na mimi ili kunipa Sub-contract Kwasababu main contract wanatumia kampuni ya nje, tuliahidiana kukutana kesho yake DSM.

Siku ya pili saa 3:15 nilifika sehemu tuliyoahidiana, kukutana.
Nilikutana na watu wawili walijitambulisha kwangu kuwa mmoja ni Askari Polisi kutoka DODOMA amepata maelekezo kwa mkuu wa police Dodoma kuja kunikamata na mwingine (Bonge la mtu) alijitambulisha kuwa ni Afisa wa Mkubwa wa Usalama wa Taifa KUTOKA MAKAO MAKUU DODOMA kwa hiyo nipo chini ya ulinzi nisifurukute chochote la sivyo watanifumua ubongo na risasi.

Niliuliza kosa langu sikuambiwa ilikuwa ni vitisho tu niliomba vitambulisho wakanitisha wao ni maalumu hawana vitambulisho.

Walinipeleka mojawapo ya kituo cha Polisi kilicho karibu ambacho wengi wanaoshikiliwa katika hicho kituo wengi ni vibaka.

Nilikabidhiwa kwa mpelelezi akaniandika jina na kunisweka lockup bila hata kupokelewa mapokezi na nikaambiwa kuna mtu atanifuata ndiye ataniambia kosa langu.

Nilikaa lockup na vibaka hao (niliponea chupu kubakwa na nikawaahidi kuwapa hela ndio wakaniacha kidogo wanishughulikie, Polisi wao hawana muda)

Nilishinda njaa, mchana ulikwisha kiza kilianza na nilianza kuhisi, njaa Kali kila nilipoomba Askari vijana wanaoleta chakula cha wafungwa kuwa naomba kuongea nao walinitisha kunivunja vunja na kuniambia niangalie vibaka wenzangu walivyo vunjwa vunjwa. Nilijitahidi kuwaambia kuwa sijui kosa langu niliambua matusi na vitisho.

Usiku mwingi (sijui saa ngapi) kukadiria Kama saa 7. Niliitwa Mara moja sogea huku cha kunishangaza alikuwa ni polisi akiambatana na mtu ambaye ni (Achtect) MFANYAKAZI WA TARURA ambaye tumewahi kuwa na UGOMVI kwa kutompa RUSHWA aliyoniomba tangu 2019.

Nilimuuliza hivi Sheikh wewe ndiye umefanya mchongo wote huu kunitesa hivi akacheka kwa dharau na kuniambia hiyo hela (RUSHWA) umeshindwa kulipa, milioni Saba sasa utalipa milioni 20 la sivyo hao vibaka watakubaka humo.

Aliniuliza una milioni 20 kwenye gari nikuachie au niruhusu ushughulikiwe na hao vibaka, niliumia sana nilitamani geti lifunguliwe nimrukie nimtafune hata meno na aliniambia hivyo mbele ya Polisi.

Alinitisha atanisafirisha katika buti na kunipeleka Kigoma kituo chake cha kazi kama sina hela atanitupa ziwa Tanganyika au atatoa ruhusa nifungwe jela miaka 10.

Nilimuuliza wewe ni nani mpaka unitishe hivi?

Alijibu: hapo upo wapi? Mimi nina hela sina Sheria.

Ningependa niendelee ila Sina muda Kama nitapata mda nitamalizia kwa siku nyingine.

Jeshi la Polisi lijitafakari je ni kweli wanalinda Raia na Mali zao au ni watesi wa Raia na Mali zao.
Kisa cha kuombwa ni nini? Kwamba rushwa ni lazima? Aisee Dunia tambala bovu..

Nini kilifuata baada ya hapo?
 
Mwanaume unaanzaje kusema ulitaka kubakwa kituo cha Polisi?

Hadithi yake ina gapes kibao, kwanza Usalama wa Taifa hawajishughulishi na mambo ya arrest.

Na ikitokea Afisa usalama wa Taifa yuko joint venture na Polisi basi ujuwe hicho ni kikosi kazi kwa kazi maalum na hapo hakuna mizaha kama hii anayohadithia huyu jamaa.
Dah,yani we jamaa sijui unaongea vitu gani.
 
Hivi nyie polisi huwa hamsimuliani yanayowakuta? Sio kila mtu ni wa kuonewa.

Kuna kisa cha polisi kukamata gari la samaki wa mtu mmoja wa kanda ya ziwa hadi wakaoza....waliokamata nao walianza kuumuka wakiwa hai.

Tenda wema na tafuta mali kwa haki sio dhuluma. Hata usipofanyiwa kisasi, karma ipo na inatenda.
 
Mwanaume unaanzaje kusema ulitaka kubakwa kituo cha Polisi?

Hadithi yake ina gapes kibao, kwanza Usalama wa Taifa hawajishughulishi na mambo ya arrest.

Na ikitokea Afisa usalama wa Taifa yuko joint venture na Polisi basi ujuwe hicho ni kikosi kazi kwa kazi maalum na hapo hakuna mizaha kama hii anayohadithia huyu jamaa.
Wewe acha hizo hii nchi haifuati sheria hata kidogo..kwani ni mara ngapi watu wamekamatwa na usalama wa taifa na kuteswa vibaya?
 
Back
Top Bottom