Nilikamatwa na Polisi na kufichwa Kituo kilichopo Dar kwa siku tatu bila kula nikipewa vitisho

Awamu iliyopita vitu hivyo vilikuwa normal sana .
 
Milioni 20 kwenye gari limepaki Polisi?
 
Ila Kuna watu wanajua kutesa wenzao duniani hapa sababu ya pesa jamani daah!! Pole mkuu..

Watu wenye pesa hasa za ulimwengu wa roho wanatesa sana. Ni pesa inaongea, umesikia " Mimi Sina sheria Nina pesa "
Huniwezi kipesa, kiuchawi wala kiserikali, nipe mkono.😁😁
 
Pole sana kama ni kweli, kwa niliyoyaona Dakawa inaweza kua kweli!

Haki ipo kwa mwenye pesa.
Mkuu Dakawa uliona nini? Nappafahamu pale kabla ya kuwa na kituo, nasikia kwa sasa kuna kituo cha Polisi kule ndani ndani, niliwahi kuishi kijiji kile na nilisoma pale darasa la kwanza mpaka la nne miaka ya 90 huko, kitambo sijafika.
 
Jamani ni 2022 funguka kila kitu weka majina na vituo vyao vya kazi unadhan ukificha ficha ndio inasaidia
Naomba kuuliza hivi vituo vya police hawawezi kuviweka kwa hali ya usafi na kutengeneza mazingira mazuri kiafya juzi kuna rafki aliwekwa aliniambia pachafu sana ,miaka kwenda uchafu ushapitwa na wakati kwanin pasiwe pasafi tu
Halaf police wanapenda rushwa mdhamana mpaka pesa ndio anatoa waweke camera
Siwapendi police
 
Kisa cha kuombwa ni nini? Kwamba rushwa ni lazima? Aisee Dunia tambala bovu..

Nini kilifuata baada ya hapo?
 
Dah,yani we jamaa sijui unaongea vitu gani.
 
Hivi nyie polisi huwa hamsimuliani yanayowakuta? Sio kila mtu ni wa kuonewa.

Kuna kisa cha polisi kukamata gari la samaki wa mtu mmoja wa kanda ya ziwa hadi wakaoza....waliokamata nao walianza kuumuka wakiwa hai.

Tenda wema na tafuta mali kwa haki sio dhuluma. Hata usipofanyiwa kisasi, karma ipo na inatenda.
 
Wewe acha hizo hii nchi haifuati sheria hata kidogo..kwani ni mara ngapi watu wamekamatwa na usalama wa taifa na kuteswa vibaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…