Nilikopa milioni 10, siku naona salary slip yanipasa kulipa 24m jicho la upande wa kushoto lilijifunga kama dakika 40 hivi. Nilijua limeparalyse!

Siyo asilimia 100 tu.Ni asilimia 140!Na hapo bado haujakutana na akina Faimbweka, Bayofpigs, Platedamnit nk. Huko mikopo ukisha kopa huwa haiishi. Watakukata maisha yako yoooteeee. Damnit!😂😂😂😂
Acha kabisa
 
Wala siyo kweli. Ina maana hukujaza Mkataba mpaka usubirie slip? Maana mkataba huainisha kiasi chote unachopaswa kulipa.

Na hakuna benki Tanzania inayotoza riba ya zaidi ya asilimia 100. Hakuna.

Hii ni Chai.
Naweza kukutumia mchakato wote dm; fedha iliyoingia na salary slip. Hakuna chai hapo, sina hata sukari ya kuungia
 
Acha kabisa mkuu. Inachekesha lakini imenitokea na nilikwama kwelikweli🤣🤣🤣
Miaka 5 au 7 au 10 ...sasa kuzungusha vzr mbona mtaji tosha? Miaka 7 uko hela watu ni fair sana wewe umeshindwa kupata hata nusu yake saving
 
Ukihitaji mkopo uso na riba na unaweza kulipika vizuri kakopeni bank ya amanawapo vizuri katika mikopo [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Taasisi za kifedha zote zinatumia njia mbili kukokotoa riba ya mkopo yaani Reducing balance au Flat rate. Hivyo ni bora umuulize afisa mikopo kuwa wewe mkopo wako unarudisha kwa njia ipi kati ya hizo?

Mfano wangu nitatumia kiwango hicho hicho cha Tshs. 6,100,000 ulichokopa wewe kutofautisha hizo njia mbili za riba ya mikopo kimahesabu kwa muda huo huo mmoja wa kurejesha pesa ndani ya miaka 3.

Flat rate,
Rejesho la mwezi = (Kiasi + (Kiasi * riba% * muda))/(muda * 12)
=(6100000 + (6100000 * 0.17 * 3))/(3 * 12)
=255,861.11
Hapa utaona flat rate rejesho kwa mwezi ni Tshs. 255,861.11 (kwa miaka 3 ni sawa na Tshs. 9,210,999.96)

Reducing rate,
Rejesho la mwezi = [kiasi * riba * (1+ riba)^muda]/[((1+ riba)^muda)-1)]
Angalizo; Riba hapa huwa inapungua kwa kugawanywa kwa 12 yaani ((17%/12) pia muda huzidishwa kwa 12 yaani (3 * 12)
=[6100000 * 0.01417 * (1 +0.01417)^36]/[((1 + 0.01417)^36)-1)]
=217,493.78
Reducing rate rejesho kwa mwezi ni Tshs. 217,493.78 ((kwa miaka 3 ni sawa na Tshs. 7,829,776.08)

Hitimisho, utaona hapo juu kuna utofauti mkubwa japokuwa wote mmekopa kiwango kinachofanana na muda wa marejesho ni ule ule ila njia iliyotumika kukokotoa riba ndiyo imewatenganisha. Muhimu sana kufahamu njia ya riba utayotumia ktk marejesho yako.
 
Bank gani hiyo dhalimu tujulishe nasi tukae mbali nayo?
 
Muda wa mkopo ndio jehanamu yenyewe. Muda wa mkopo ukiwa mdogo maumivu nayo yanakuwa madogo.
More years more pain
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…