Nilikopa milioni 10, siku naona salary slip yanipasa kulipa 24m jicho la upande wa kushoto lilijifunga kama dakika 40 hivi. Nilijua limeparalyse!

Nilikopa milioni 10, siku naona salary slip yanipasa kulipa 24m jicho la upande wa kushoto lilijifunga kama dakika 40 hivi. Nilijua limeparalyse!

Acha kabisa aisee!

Nikiwa nimepagawa na changamoto iliyokuwa inanikabili bila kujua la kufanya, nikakimbilia benki moja kuomba mkopo. Kufika pale nikamuambia afisa mikopo kuwa nahitaji m15, akaniambia m10 ni utapata lakini si hizo ulizotaka. Nikaona kheri tu itaokoa kitu tena kwa kiasi kikubwa sana tu.

Wakati huo, simu inapigwa kila baada ya sekunde 20 kutoka huko kwenye changamoto iliyonifanya niende kukopa, nilipagawa sana. Wakati afisa mikopo ananieleza habari za makato n.k mimi hata sikuwa nasikia chochote.

Akili ilikuwa kwenye kupata pesa tu nikamalize tatizo. Siku kadhaa mbele nikafanikiwa na tatizo likaisha na akili ikarudi katika utulivu wa kawaida.

Siku zinavyoenda haraka, mwisho wa mwezi ukafika bwana! Aisee, ile naiangalia salary slip sikuamini nilichokiona. Milioni 24 nahitajika kulipa. 24M!!

Kwanza nilihisi baridi, halafu ganzi; baadae nikahisi uono wangu kama hauko sawa. Nikajiuliza imekuaje mbona sioni vizuri? Kwakuwa nilikuwa chumbani, nikasogea kwenye kioo kujiangalia. Dah, si ndo nakuta jicho moja la upande wa kushoto limejifunga, kope haitaki kupanda juu ('kukupila' watu wa pwani ya kusini wanasema).

Nikajaribu kulifunua kwa mkono, wapi! Nikiliacha linajifunga tena. Hali iliendelea hivyo kama dakika 40 au saa moja hivi. Baadae sana ndo likarejea katika hali ya kawaida. Nilishapagawa, nilijua limeparalyse!

Mikopo!!!! Ukiweza kuachana nayo iache ndg'angu!
Duh...mkopo sio aisee
 
bora yako wewe unahis kuchanganyikiwa,mm hapa nishavurugwaa kitambo kutoka kuchezea vicent mpk sas account zero,madeni yasikie tu kwa mwenzako ukiwa na maden ht usingiz haukubambi vzr yan pesa inatutesa san kwakwel hapa nadaiwa mpk na mama mkwe[emoji23][emoji23]
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Acha kabisa aisee!

Nikiwa nimepagawa na changamoto iliyokuwa inanikabili bila kujua la kufanya, nikakimbilia benki moja kuomba mkopo. Kufika pale nikamuambia afisa mikopo kuwa nahitaji m15, akaniambia m10 ni utapata lakini si hizo ulizotaka. Nikaona kheri tu itaokoa kitu tena kwa kiasi kikubwa sana tu.

Wakati huo, simu inapigwa kila baada ya sekunde 20 kutoka huko kwenye changamoto iliyonifanya niende kukopa, nilipagawa sana. Wakati afisa mikopo ananieleza habari za makato n.k mimi hata sikuwa nasikia chochote.

Akili ilikuwa kwenye kupata pesa tu nikamalize tatizo. Siku kadhaa mbele nikafanikiwa na tatizo likaisha na akili ikarudi katika utulivu wa kawaida.

Siku zinavyoenda haraka, mwisho wa mwezi ukafika bwana! Aisee, ile naiangalia salary slip sikuamini nilichokiona. Milioni 24 nahitajika kulipa. 24M!!

Kwanza nilihisi baridi, halafu ganzi; baadae nikahisi uono wangu kama hauko sawa. Nikajiuliza imekuaje mbona sioni vizuri? Kwakuwa nilikuwa chumbani, nikasogea kwenye kioo kujiangalia. Dah, si ndo nakuta jicho moja la upande wa kushoto limejifunga, kope haitaki kupanda juu ('kukupila' watu wa pwani ya kusini wanasema).

Nikajaribu kulifunua kwa mkono, wapi! Nikiliacha linajifunga tena. Hali iliendelea hivyo kama dakika 40 au saa moja hivi. Baadae sana ndo likarejea katika hali ya kawaida. Nilishapagawa, nilijua limeparalyse!

Mikopo!!!! Ukiweza kuachana nayo iache ndg'angu!
Pesa nyingine hukumkopea afisa mikopo kweli?!! Maana Tz kila mahali ni wizi tu.
 
Mkuu acha tu, wakopaji tunapitia hali ngumu hapa nilipo nahisi muda si mref ntachanganyikiwa.
Mungu atusaidie, mi nimelipokea kisaikolojia na sasa naweza hata kuliongelea kikawaida kama hivi. Mwanzoni hali yako ilikuwa ngumu sana.....nilikuwa naongea tu peke yangu
 
Issu ni time ya mkopo, km ulichagua makato madogo per month automaticaly miaka itakua mingi na ribq itakua kubwa sana
 
Sio wizi ila sisi sio waelewa wa masuala ya mikopo. Mfano wanakuambia riba ni 14 % Kwa mwaka, maana yake ni kwamba kama mkopo utakuwa wa miaka nane riba itakuwa 14% zidisha Kwa miaka 8 = 112%
Kama umechukua mkopo wa million 10 utarudisha zaidi ya million 22 Kwa hiyo miaka nane.
Ushauri wangu ni vyema tukope mikopo ya muda mfupi, napendekeza isizidi miaka 3.

Mfano wa pili kama angechukua hiyo hiyo million 10 Kwa miaka mitatu ingekuwa hivi;
14% zidisha Kwa miaka 3= 42%
Hapa angerudisha million 14 na laki kadhaa.
42÷100x1000000= 4,200,000/= hii ndio riba ukijumlisha na ile million 10 ndio unapata 14,200,000/=
Mtumishi wa Bwana. Hawa jamaa wa mikopo utumia hesabu za future value of money. Yaani kama unataka mkopo wa 20m, itatafutwa thamani ya hiyo 20m kwa muda wa mwisho wa mkopo. Kwa hesabu ni rahisi ni mf mkopo 20m(1+riba)" hicho kialama" ni muda wa mkopo.
 
Ndio maana mwenyezi Mungu akaharamisha riba.. Yaani anayetoa riba na anayepokea riba wote wametangaza vita na Allah tabaraka.. Riba ni mbaya sana kama Mungu mwenyewe ameliona ilo sisi ni nani mpaka tuone faida ya riba..
Mungu hajawahi kataza riba na hata alipoongelea wale waliopewa talanta, mmoja akaifukia alisema angepeleka kwa watoza riba naye angepata zaidi.
 
Kuna baadha ya hizi micro finance mfano Finca wanatoa mikopo kwa riba ya mwezi 5% kwa mwaka inakuwa 60%. Sasa unakuta mleta mada kachukua mkopo huko kwa muda wa miaka miwili tu riba inakuwa 120% bado hawajakata bima na Administration fee lazima uchanganyikiwe tu.!
Sheria imewabana kwa 42% p.a ambayo ni 3.5% p.mo
 
Back
Top Bottom