Nilikopa Sh 5M kutoka Bayport, nimekatwa kwa miezi 6, nimeomba balansi wanasema imebaki Sh 9M, kivipi?

bapi

Member
Joined
Dec 11, 2023
Posts
6
Reaction score
25
Mimi ni mtumishi, nilikopa kwenye Kampuni ya Bayport kiasi cha Shilingi Milioni 5 tangu Machi 2026. Nilikopa kwa muda wa miaka kumi. Nimetumikia deni langu kwa kipindi cha miezi 6. Nimeomba balance ili nilipe deni langu lote liishe, nimetumiwa barua natakiwa nilipe Shilingi milioni 9.

Nashindwa kuelewa imepandaje mpaka kufika Sh Milioni 9 kwa kipindi cha miezi sita, na huku walikuwa wananikata kwenye mshahara! Nisaidie nipate kujua kwa wana-forum, maana hata nimewapigia siwaelewi sababu wananikatia simu.

Imekaaje ndani ya miezi sita milioni tano riba yake iwe milioni nne, na huku hiyo miezi sita wameshanikata?
 
Wewe ushindwe kukusanya za kwako taratibu taratibu usubiri kwenda kuchukua za wenzako ukidhani ni Rahisi Tu?

Pes sio nyepesi kiasi Hicho, punguzeni tamaa fanyeni mnayoweza kwa mshahara yenu
 
Mikopo haiendi kwa formula ya riba nyepesi kama mnavyodanganywa eti ni asilimia 10 au 15%.

Kitu ambacho watoa mikopo wote wanaficha ni Compound Interest hii hat mabenki hawakwambii.

Ndio Maana wakopaji wengi hohehahe wenye vipato vidogo huwa wanashindwa kulipa madeni
 
Umempa ushauri au unamsimanga, kukopa sio dhambi, kama kuna namna u anajua mambo ya mikopo unamsaidia. What you've written is utter rubbish.
 
Fika ofisini upate mchanganuo wa deni.....
Yawezekana kuna mambo mengi mfano:-
1) adhabu ya kulipa deni kabla ya kuiva (early repayment penalty)
2) adhabu ya kuchelewesha marejesho (ikiwa ulichelewesha marejesho ya kila mwezi) n.k

Pia ukumbuke kwamba kwa kuwa mkopo wako ni wa muda mrefu, miaka 10, marejesho uliyofanya kwa miezi yote 5 ya mwanzo yalikuwa, kwa kiasi kikubwa, ni riba na sio principal.......
 
Sasa mkuu milioni 5 ulipe kwa muda wa miaka 10 unategemea nini.. riba lazima ipande, piga mahesabu milioni 5 ya 2016 vitu ilivyokuwa inavinunua 2016 ndio sawa na leo? Haya yeye kakukopesha milioni 5, kumbuka ni biashara yeye atafaidika na nini?
 
Umekopa 5M ili uilipe kwa miaka 10.

Wao washaproject profit ya zaidi ya 11M halafu leo baada ya miezi 6 uwape hii stori wakuelewe?

Mzee hapo mtatoana damu.

Calculation yao hii hawawezi kukuelewa.
IMG_20261006_100337_947.png
 
Mikopo haiendi kwa formula ya riba nyepesi kama mnavyodanganywa eti ni asilimia 10 au 15%.

Kitu ambacho watoa mikopo wote wanaficha ni Compound Interest hii hat mabenki hawakwambii.

Ndio Maana wakopaji wengi hohehahe wenye vipato vidogo huwa wanashindwa kulipa madeni
Sio maskini tu, hata matajiri wanashindwa kulipa madeni.
 
Yaani milioni tano unalipa kwa miaka kumi? Acha upigwe.
Tatizo mnapokuwa na shida ya pesa huwa hamtafuti taarifa sahihi, mnakuja kuzitafuta baada ya kukwama.

Angalia nakala yako ya mkataba au nenda ofisini kwao watakupa maelezo ila huko sio kwa kukopa.
 
Back
Top Bottom