Nilikopa Sh 5M kutoka Bayport, nimekatwa kwa miezi 6, nimeomba balansi wanasema imebaki Sh 9M, kivipi?

Sasa mkuu milioni 5 ulipe kwa muda wa miaka 10 unategemea nini.. riba lazima ipande, piga mahesabu milioni 5 ya 2016 vitu ilivyokuwa inavinunua 2016 ndio sawa na leo? Haya yeye kakukopesha milioni 5, kumbuka ni biashara yeye atafaidika na nini?
mimi sijui kwanini naonaga kama ni sawa tu, hiyo million 5 mtu akiiweka sehemu sahii mtaji wa million 10 utafika ndani ya mwaka tu, kwa miaka mitatu atakuwa anapata faida tu kwenye hiyo miaka 10,
 
Mimi ni mtumishi, nilikopa kwenye Kampuni ya Bayport kiasi cha Shilingi Milioni 5 tangu Machi 2026. Nilikopa kwa muda wa miaka kumi. Nimetumikia deni langu kwa kipindi cha miezi 6. Nimeomba balance ili nilipe deni langu lote liishe, nimetumiwa barua natakiwa nilipe Shilingi milioni 9.

Nashindwa kuelewa imepandaje mpaka kufika Sh Milioni 9 kwa kipindi cha miezi sita, na huku walikuwa wananikata kwenye mshahara! Nisaidie nipate kujua kwa wana-forum, maana hata nimewapigia siwaelewi sababu wananikatia simu.

Imekaaje ndani ya miezi sita milioni tano riba yake iwe milioni nne, na huku hiyo miezi sita wameshanikata?
Hahahaaa hao wahuni walikimbizwa na magu wamerudi tena

Mbona ulipokopa ujatuambia uliogopa mzinga eeh
 
Mimi ni mtumishi, nilikopa kwenye Kampuni ya Bayport kiasi cha Shilingi Milioni 5 tangu Machi 2026. Nilikopa kwa muda wa miaka kumi. Nimetumikia deni langu kwa kipindi cha miezi 6. Nimeomba balance ili nilipe deni langu lote liishe, nimetumiwa barua natakiwa nilipe Shilingi milioni 9.

Nashindwa kuelewa imepandaje mpaka kufika Sh Milioni 9 kwa kipindi cha miezi sita, na huku walikuwa wananikata kwenye mshahara! Nisaidie nipate kujua kwa wana-forum, maana hata nimewapigia siwaelewi sababu wananikatia simu.

Imekaaje ndani ya miezi sita milioni tano riba yake iwe milioni nne, na huku hiyo miezi sita wameshanikata?
Wameweka na emergency ikitokea umekufa miaka 10.mingi mkuu

Hizo hati kama umeweka sahau kama hilo gari sahau la kwao
 
Unaenda kukopa Bayport, Letshego!
CRDB na NMB hamuwaoni?
Bila shaka wewe ni mwalimu, maana inaonekana benki kubwa zimewapita pembeni kabisa!
Na ukishamaliza mkopo wao hawakwambii bado wanaendelea kukukata na mpka waje kukutoa kwenye fyekeo lao ni kimbembe
 
Mimi ni mtumishi, nilikopa kwenye Kampuni ya Bayport kiasi cha Shilingi Milioni 5 tangu Machi 2026. Nilikopa kwa muda wa miaka kumi. Nimetumikia deni langu kwa kipindi cha miezi 6. Nimeomba balance ili nilipe deni langu lote liishe, nimetumiwa barua natakiwa nilipe Shilingi milioni 9.

Nashindwa kuelewa imepandaje mpaka kufika Sh Milioni 9 kwa kipindi cha miezi sita, na huku walikuwa wananikata kwenye mshahara! Nisaidie nipate kujua kwa wana-forum, maana hata nimewapigia siwaelewi sababu wananikatia simu.

Imekaaje ndani ya miezi sita milioni tano riba yake iwe milioni nne, na huku hiyo miezi sita wameshanikata?
Mikataba wako unasemaje kwani.

Riba ni asilimia ngapi?
Kuna ada ya kuvunja mkataba(kutaka kusettle mkopo wako kabla ya muda) unaweza kuta ni asilimia 3 au mbili ya Ile principal amount

Ukipata majibu ya maswali hapo juu utajua imefikaje m9 au unapigwa kumbuka pia hayo marejesho ya mwanzo mara nyingi hua yanaenda kulipia riba kwa asilimia Kama 90 au zaidi
 
Mkataba uliokuwa umeingia nawo hapo mwezi machi ulikuwa wa muda gani? Kama haikuwa huwo muda ambao wewe unataka kuumaliza basi hapo huna sababu ya kuhoji imefikaje M9.
Imefika milioni tisa kwa maana ya kipindi chote cha huwo mkataba ambao mlikubaliana.
 
Yaani milioni tano unalipa kwa miaka kumi? Acha upigwe.
Tatizo mnapokuwa na shida ya pesa huwa hamtafuti taarifa sahihi, mnakuja kuzitafuta baada ya kukwama.

Angalia nakala yako ya mkataba au nenda ofisini kwao watakupa maelezo ila huko sio kwa kukopa.
Hata mie nimeshangaa 5M ulipe kwa 10yrs, duuh, huyu hakufanya maamuzi sahihi.
 
Mimi ni mtumishi, nilikopa kwenye Kampuni ya Bayport kiasi cha Shilingi Milioni 5 tangu Machi 2026. Nilikopa kwa muda wa miaka kumi. Nimetumikia deni langu kwa kipindi cha miezi 6. Nimeomba balance ili nilipe deni langu lote liishe, nimetumiwa barua natakiwa nilipe Shilingi milioni 9.

Nashindwa kuelewa imepandaje mpaka kufika Sh Milioni 9 kwa kipindi cha miezi sita, na huku walikuwa wananikata kwenye mshahara! Nisaidie nipate kujua kwa wana-forum, maana hata nimewapigia siwaelewi sababu wananikatia simu.

Imekaaje ndani ya miezi sita milioni tano riba yake iwe milioni nne, na huku hiyo miezi sita wameshanikata?
Wewe jiandae kulipa deni lote la milioni 9 ndipo siku nyingine akili itakukaa sawa. Tumepiga sana kelele humu jukwaani kuwazuia kukopa kwenye hizo taasisi za fedha, hamsikii.

Bayport, Platinum credit, Fanikiwa, na takataka nyingine siyo taasisi za kukimbilia kukopa. Wana ruba kandamizi sana.
 
Back
Top Bottom