Mimi ni mtumishi, nilikopa kwenye Kampuni ya Bayport kiasi cha Shilingi Milioni 5 tangu Machi 2026. Nilikopa kwa muda wa miaka kumi. Nimetumikia deni langu kwa kipindi cha miezi 6. Nimeomba balance ili nilipe deni langu lote liishe, nimetumiwa barua natakiwa nilipe Shilingi milioni 9.
Nashindwa kuelewa imepandaje mpaka kufika Sh Milioni 9 kwa kipindi cha miezi sita, na huku walikuwa wananikata kwenye mshahara! Nisaidie nipate kujua kwa wana-forum, maana hata nimewapigia siwaelewi sababu wananikatia simu.
Imekaaje ndani ya miezi sita milioni tano riba yake iwe milioni nne, na huku hiyo miezi sita wameshanikata?