Nilikuwa nawatetea sana singo mama lakini kwa hili la huyu mama limenikata maini kabisa

Nilikuwa nawatetea sana singo mama lakini kwa hili la huyu mama limenikata maini kabisa

HUyu mwanamke aliolewa akiwa na mtoto mwenye umri wa miezi 6 na jamaa mkatoriki

Mtoto kafariki akiwa mkubwa,huyo mwanamke anataka mtoto azikwe kwa imani ya kiislamu

Ebu fikiria nyumbani kwako kufanyike ibada ya imani tofauti na yako,wewe baba wa familia utajisikiaje

Jamaa kaamua kwenda polisi kuzuia maziko.

--

View attachment 2665378

Taharuki kubwa imeibuka huko Mkoani Mwanza baada ya mwili wa marehemu kufikishwa msikitini kuswaliwa kwa maziko lakini baba wa marehemu akazuia asizikwe.

Kwa mujibu wa maelezo ya mama wa marehemu huyo, kabla ya kuolewa mwanaume huyo alimkuta akiwa na mtoto wa miezi sita na kwamba mtoto huyo ana baba yake mwingine ambaye ni Mchaga na ni Muislamu.

Mara baada ya kufariki kwa mtoto huyo, mwanaume huyo ameibuka na kusema kwamba hataki mtoto huyo azikwe kiislamu huku mama wa mtoto akiweka wazi kwamba mtoto huyo siyo mkristo na hivyo anaomba mtoto wake azikwe kwa kufuata taratibu za dini yake ambayo ni dini ya kiislamu.

Aidha, kutokana na mvutano huo, Jeshi la Polisi limelazimika kuingilia kati na kuahirisha mazishi hayo mpaka pale mwanaume huyo aliyedai kwamba mtoto huyo asizikwe kiislamu ataporejea.
wewe unafikiri aliachika!!!??
 
Sijaona tatizo, huyojamaa anataka kuleta ulimbukeni.. kama hataki msiba uwepo nyumbani kwake aseme tu, sio kumzika mtu kwa imani isiyo yake.

Sijaona kosa la singo maza hapo.
 
Back
Top Bottom