Nililogwa ili nife kwa kisukari na pressure

Nililogwa ili nife kwa kisukari na pressure

Hivi hamuwezi kuziandika na kuziweka kwenye uzi mmoja vitu vyote bila kuchosha watu na miendelezo yenu ya robo boro!?? 9
 
Yule kijana alipokwambia kuhusu uganga ukamjibu wewe ni mkristo unalindwa na Yesu huna hata chale mwilini mwako hii ilikuwa ni katika sehem ya pili au ya tatu,hii sehem ya mwisho unasema hukuwa unaamini uwepo wa Mungu[emoji23]
 
Hivi hamuwezi kuziandika na kuziweka kwenye uzi mmoja vitu vyote bila kuchosha watu na miendelezo yenu ya robo boro!?? 9
Hahaaaaaaa, kweli JF kina watu wana stress zao. Vipi bro, leo sister wako hajakupa chakula kilichobaki cha uncle zako?
 
ni kweli ukiwaomba ushahid wa uchawi hawana.
Uchawi unavumishwa na wavivu kufikili mi niliendaga kwa babu yangu huko bariadi ndani ndani ambapo babu yangu anasifika kwa uganga na ukifika kuna nyomi yaani hadi majambazi yanakuja kuchenjia eti dawa ya kukinga risasi yaani nikawaza polisi wangeweka ma informas kwa waganga maarufu wangeokota waarifu wengi mno.
Kiufupi pale nakula supu za kuku na mbuzi daily ila nilichojifunza babu ni wale wazee wajanja wajanja wana akili kubwa sema hawajapata nafasi ya kusoma.
NITAENDELEA
 
😂😂
 
SEHEMU YA TANO:

Wakati maumivu na mateso yanaendelea na hata nilipokuwa naenda Hospitali pamoja na wao kunipa Dawa kwa ajili ya Ugonjwa wa sukari na pressure, sikuwahi kuzitumia hizo dawa kwani nafsi yangu ilikuwa inaniambia huo sio ugonjwa wa kibinadamu. Mama yangu alinieleza kuwa mwanangu huo sio ugonjwa wa kawaida ni Mapepo hayo. Muangalie Mungu.

Kipindi chote hiko na maumivu yote, kukataliwa na kusemwa vibaya, kukonda n.k hakuna Dr aliyenithibitishia kuwa nina either pressure au sukari. Nikaamua maamuzi ya kumtafuta Mungu.

Kulikuwa na kanisa moja la kilokole lililokuwa limejengwa kwa miti na juu limeezekwa kwa nyasi jirani na hapo kwangu. Huyo Mchungaji alikuwa ni yeye na mkewe na watoto tu na kimsingi nilikuwa namdharau na pamoja nilikulia kwenye familia ya wazee wa Kanisa ila nilikuwa napinga uwepo wa Mungu. Nikaona kwanini niteseke wakati nimekulia kwa Baba na Mama ambao ni wazee wa Kanisa. Nimekulia na kulelewa katika maadili ya Kikristo na nakumbuka Mwaka 1998 Bwana aliniambia na nilimuona waziwazi katika Maono ya usiku kuwa nitamtumikia. Nikasema, sifi nitaishi ili nitangaze matendo makuu ya Bwana. Nikachukua hatua na kwenda Kanisani kwa yule Mchungaji.

Hapo ndipo maisha yangu yalibadilika, nikaokoka na kumkabidhi Yesu Maisha yangu na tola mwezi huo wa kumi 201.... imebaki kuwa historia. Vile vifaa nikavitoa msaada hospitali moja huku nilipo sasa japo changamoto hiyo ilinifanya nikimbie kutoka kule na pia nilipoteza nyumba yangu ambayo nilikuja uiza kwa hasara, mashamba ekari 50 ambazo wasukuma waliofukuzwa kwenye maeneo ya hifadhi wakati wa Operation tokomeza ujangili walizivamia na viwanja 6 (sita) nilivyokuwa nimenunua niliviacha na kukimbia japo navyo nilikuja kuuza kwa hasara.

Sasa nina amani na kumtukuza Mungu japo nilipoteza vingi vya kimwili ila ninauzima na nimepata vingi vya Kiroho ikiwemo kumjua Mungu wa kweli yaani Yesu Kristo.

Asanteni wote na tumefikia MwishoView attachment 2633258
Yesu ni mwemasana umefanya maamuzi sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom