Hii stori sijawahi kumuhadithia mtu yoyote. Ilikua mwaka 2017 nilikua naishi geto peke yangu.
Miaka ya nyuma nilikua siamini kama mtu anaweza kulala na njaa siku mbili asife. Lakini toka mwaka 2017 rasmi nilianza kuamini mtu anaweza kukaa na njaa wiki nzima na asife.
Nilipata changamoto kubwa ya kimaisha mwaka 2017, mwenye nyumba alikua ananidai kodi ya nyumba nilikua sijamlipa miezi kadhaa. Anaweza akaja asubuhi akagonga sana mlango nisimfungulie akihisi sipo kumbe nipo ndani nime lock na ufunguo. Au mara nyingine naweza amka hata asubuhi sana saa kumi asinikute. Kurudi pia nilikua narudi usiku hata saa saba usiku ili asije nidai hela kwa sababu sina,. Ingawa Arusha kuna vibaka usiku lakini niliamua hawa vibaka nitalala nao mbele maana sina namna nyingine.
Kulala siku tano bila kula ilikua kawaida, hiyo kushindwa kutema mate nime experience sana. Nilikopa sana maduka ambayo nilozoeleka mpaka yakaisha nikawa sina pa kukopa pengine. Kuna mama mmoja tulikua tunasali wote alikua anauza samaki wa kukaangwa,mihogo,ndizi etc muda wa usiku. Siku nikitingwa na njaa nilikua naenda kujipigisha story kwa yule maza mpaka namkopa.
Siku moja nilipigwa na njaa Kali sijala siku kadhaa nimelala nashindwa hata kuamka sina hata nguvu. Nikaona sasa leo officially kabisa naenda kufa. Nikajikongoja niende nje dukani kama naweza kopa. Hiyo ni mida ya saa sita usiku maduka yote ninayokopa yamefungwa limebaki moja tu ambalo muuzaji sikopagi kwake sina mazoea kabisa, hata yule mama muuza samaki amefunga muda sana kwa hiyo sina jinsi. Nikaamua kujikongoja kwenda home nikafie huko. Hapo tumbo linakata balaa. Kwa ambao hamjawahi kukaa na njaa kwa muda mrefu fahamu kuwa, tumbo linakua kama linavuta kwa ndani.
Nikiwa njiani narudi nyumbani nikakutana na dogo mmoja, huyu dogo miaka ya nyuma alikua anaishi na mama ake ni single mother. Enzi hizo dogo anasoma tulikua tunaishi mtaa mmoja, dogo alikua anamsumbua sana mama ake na alikua hataki kwenda shule enzi hizo anasoma so mimi ndo nilikua namchapa na kumpeleka shule.......... Sasa nilipokutana nae nikamwabia "alafu we msengE ulinisumbuaga sana wakat unasoma kila siku nafanya kazi ya kukupeleka shule, lete elfu tano chap nikanywe bia"...... Aisee kweli mungu yupo, dg alinipa elfu tano nikaenda nunua mazaga pale dukan nikaenda home gonga msosi wa maana. Aisee nikikumbuka ile siku uhai ungenitoka.