Nilimezwa na chatu mwaka 2008

Nilimezwa na chatu mwaka 2008

Sitaisahau elnino ya mwaka tajwa hapo juu, mvua zilikuwa kubwa sana kule maeneo ya Mbeya bila kujua nikaingia kwenye mtego wa chatu, alinidondosha.

Pona yangu sikuamka, na ukilala chali chatu hakuwezi alinitambaa sana mwilini ili anivingirishe ila nilijikaza na ile ngozi yake laini ilivyokuwa inanitambaa mwilini.

Nilijikaza lakini alibahatisha kunimeza mguu wote; alishindwa kunimalizia kwasababu nilikuwa nimetanua mguu wa kulia hivyo sikupita mdomoni mwake. Niliokolewa baada ya masaa matatu ila mguu uliungua sana.

Huwezi amini tulikuwa tunaangaliana jicho kwa jicho huku nimelala, ujasiri huu niliupata baada ya kulewa sana pombe ya Kiroba ilikuwa maarufu sana kule Mbeya inaitwa Double Punch.

Chatu msikie tu. Yupo kama jini au shetani, yale macho yake mkitazamana kwa karibu.
Tatizo ana macho ya binadamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simu za camera tangu miaka ya 2005,faza wangu mdogo alikuwa anaenda Kampala kurangua simu zile za kufunua zilikuwa na kamera hapa bongo alikuwa anauza simu moja laki tano, enzi hizo tena anauza mkononi Ila zilikuwa mpya,2008 zilikuwepo simu zenye kupiga picha sema zilikuwa chache.
Ahsante atakua mtoto uyu
Bora ma legendary mmemkumbusha
 
Tuma picha ya mguu ulioungua, ndipo tutakuamini..

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulikatika mkuu....baada ya hilo tukio alijaribu kuvuka MTO wenye mamba baada ya KUANGALIA ile muvi ya The hardway.....mamba wakapita na mguu ulioungua,na walishukuru sana maana ulikuwa umeshapikwa na chatu...sasa hivi anatumia mguu wa tatu kutembelea!!!!
 
Back
Top Bottom