Zee la madawa
JF-Expert Member
- Nov 28, 2022
- 1,895
- 4,478
Week hii miongoni mwa story kubwa mitandaoni ni kuchumbiwa kwa mtoto wa Rais Samuel Ruto na ndugu yetu wa kitanzania Isaya Yunge.
Kupitia story hiyo nikakumbuka kisa changu cha sekunde kadhaa na binti huyo.
Mwaka 2023 October nilikwenda Mombasa kushiriki mkutano mkubwa wa program ya kimataifa inayoitwa Global Opportunity Youth Network (GOYN) katika mkutano huo wa siku 4 au 5 siku moja tulikwenda kutembelea watu waliowezeshwa na program hiyo (success stories) basi washiriki wote wa mkutano tulipanda mabasi madogo kuelekea huko.
Mimi nilikaa seat moja na mama mmoja wa kizungu ambae tulikuwa na mazungumzo mazuri sana na ilipofika wakati wa kurudi yule mama wa kizungu alichelewa kuingia kwenye gari, mara akatokea binti mmoja akanisalimia na kuniuliza kama angeweza kukaa na mimi. Kwakweli sikumdharau lakini nilitamani sana yule mama wa kizungu arudi tukae wote na tuendelee na maongezi yetu, hivyo jawabu langu kwa yule binti wa lilikuwa ni moja tu kuwa "kuna mtu anakuja kukaa"
Nae alienda kukaa kwenye siti nyingine na mtu mwingine, ajabu ya binti huyo hakutaka kukaa peke yake ...maana siti zilizo wazi zilikuwa nyingi. Baadae mzungu wangu akaja moyo wangu ukafurahi safari ikaendelea... 😃
Wakati tunashuka kwenye gari kuna kijana wa kikenya akanifuata ambaye tayari tulishafanya mazoea akaniuliza "unamjua ni nani yule alikuomba kukaa na wewe ukamkatalia?" Bila kumjibu kama namjua au simjui nikakanusha kuwa sikumkatalia bali kulikuwa na mtu angekuja kukaa.. akacheka kisha akaniambia "yule ni Charlene Ruto" .."mtoto wa Rais Ruto...?" nilipigwa na butwaa... pale pale nilijilaumu sana kwanini nilikosa hiyo nafasi ya kukaa na mtoto wa Rais tukapiga story, na nikavuta kumbukumbu jinsi alivyokuwa akiongea na mtu mwingine waliokaa seat moja ambae alikuwa ni msichana, nikasema ile ilikuwa nafasi yangu😃
Lakini pia nilishangaa kumuona akitembea bila ya ulinzi..
Niliendelea kumshangaa na kuuliza watu mbona huyu mtoto wa Rais hana ulinzi? Kila mtu aliniambia watu wote wamemzoea hivyo na hata hawamshangai tena, wanasema "she is so social "
Katika picha inayoambatana na story hii utaniona mimi juu kushoto kabisa na charlene chini nimemzungushia blue kichwani.
Hadithi hii simaanishi ningemuoa mimi😃
Nawaza tu labda angekuwa rafiki yangu kama ningepata nafasi ya kukaa nae😃