Nilimpenda sana mpenzi wangu ila kanisaliti

Nilimpenda sana mpenzi wangu ila kanisaliti

Joined
Jun 20, 2016
Posts
97
Reaction score
106
Kwema wakuu Niko kwenye kipindi kigumu Sana ni hv nilikuwa na uhusiano na dada mmoja wa kichaga yeye wakati huo anaishi na dada yake wakati mahusiano yako hot Mara nyingi alikuwa ananambia anelaenda kusali kwa mwamposa.

Sasa Kuna siku Niko kazini nikapigiwa simu na jamaa ananiuliza unamfahamu x nikasema ndio akasema ni nani kwako nikamwambia ni mtu wangu jamaa akahamaki Sana akauliza kama nilishawahi kutumia Kinga nikamwambia no kufupisha story kumbe alikuwa na mahusino na jamaa at the same time Yuko na mwamba nilipombana akasema alikuwa nae kabla yangu so akatoa maamuzi kuwa yeye anataka aendelee na Mimi baadae ya hapo ikaonekana ana mimba

Sasa ikawa mtihani kwangu kwa maana tumeshare penzi na jamaa nikamtunza kibishi hivyo hivyo kiukweli kipindi hicho sikuwa na pesa so akawa anasema namnyanyasa nk Kuna siku akanambia anaona damu inamtoka so hajui tatizo ni nn nikamwambia jarbu kuulizia kwa wanawake wenzio wakupe uzoefu yeye wakati huo Yuko Moshi kwa wazaz wake Sasa siku moja nikawa namwambia nakutumia hela uende hosp wakati huo nachrt na dada kwa wakati mmoja Sasa dadaake akakosea sms badala atume kwa mdgo wake akatuma kwangu anasema nenda kacheki hospital ukiona uko fresh usimwambie ili ule pesa yake

Sasa baadae ya SMS ile nilitokea kuwachukia Sana yeye na dada yake alienda hospital akacheki ikaonekana mimba Iko nnje ya kizazi wakatoa baadae ya kuitoa dogo akawa na jeur kwangu na zarau tukigombana tukaachana kiukweli japo tuliachana bila mawasiliano kwa mwaka mzm lkn bdo nilikuwa nampenda nakumkumbuka Sasa juzi nikampigia akapokea tumeongea Sana akadai Hana hela Hana kazi nimsaidie kutafta kazi Nika mwambia sawa Ila nikamwambia nataka niombe ruhusa nije Moshi nikuone akasema utakaa siku ngapi nikamwambiila siku tatu akaniambia sawa lkn si unaniona tu unaendelea na ratba zako pale pale nikaishiwa nguvu kiukweli

Nampenda kupitiliza lkn ananipa drama nyingi ikifika usiku simu haipokelewi Ila asbh fasta atakwambia nilipitiwa na usingizi imagine saa tatu Sasa najikuta Sina Raha yaani nimekuwa mtumwa wake sijui ndio limbwata nampenda mnoo najitahidi kuwa mwema ili anielewe wapi

Kuna mda akili inaniambia tafuta pesa siku aje akuheshimu nakomaa na hiyo philosophy lkn najikuta Tena nampigia simu n

Naomba waliowahi kukutana na Mambo haya wanipe tips walifanyaje kuachana nao mnisamehe kwa mwandiko wangu kiukweli Niko down Sana nahitaji msaada.
 
Story yako kidogo ilingane na yangu, ni mchaga hivyo hivyo na alikuwa na bwana mwingine na akapata mimba,Nilipogundua kuwa alichepuka siku za hatari nikamtimua kwao Moshi mpaka mtoto azaliwe tupime DNA.

Hata mimi nikiri roho inaniuma sana hasa ukizingatia nilimpenda sana lakini haina jinsi,siwezi kuishi na mwanamke msaliti,Hata mtoto kama atazaliwa wa kwangu atabaki kuwa mama mtoto tu,lakini si mke.INAUMA sana! Lakini hakuna jinsi,Jikaze mkuu,Maisha lazima yaendelee.
 
Kwa kusoma tu haraka, nimejiwa na mambo yafuatayo...

1. Unaonekana una umri mdogo sana, yaani huna sana uzoefu wa maisha...

2. Kuna uwezekano pia huyo mwanamke ni mpenzi wako wa kwanza, hivyo moyo wako hauna uzoefu bado na namna ya kudeal na aina tofauti za wanawake...

3. Inaonesha pia huna kazi inayokuweka busy...

Mwisho, achana naye na tendea kazi hiyo 1-3 kama vipo sahihi.

Mahali fulani, wakati usioujua kuna mwanamke kwa ajili yako anakungoja, ni suala la muda tu
 
Kwa kusoma tu haraka, nimejiwa na mambo yafuatayo...

1. Unaonekana una umri mdogo sana, yaani huna sana uzoefu wa maisha...

2. Kuna uwezekano pia huyo mwanamke ni mpenzi wako wa kwanza, hivyo moyo wako hauna uzoefu bado na namna ya kudeal na aina tofauti za wanawake...

3. Inaonesha pia huna kazi inayokuweka busy...

Mwisho, achana naye na tendea kazi hiyo 1-3 kama vipo sahihi.

Mahali fulani, wakati usioujua kuna mwanamke kwa ajili yako anakungoja, ni suala la muda tu
Asante mkuu age 33yrs nakuwa busy sana bt nadhani nahitajj kujitafakari upya thnks for ya comments

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Story yako kidogo ilingane na yangu,Ni mchaga hivyo hivyo na alikuwa na bwana mwingine na akapata mimba,Nilipogundua kuwa alichepuka siku za hatari nikamtimua kwao Moshi mpaka mtoto azaliwe tupime DNA.Hata mimi nikiri roho inaniuma sana hasa ukizingatia nilimpenda sana lakini haina jinsi,Siwezi kuishi na mwanamke msaliti,Hata mtoto kama atazaliwa wa kwangu atabaki kuwa mama mtoto tu,lakini si mke.INAUMA sana! Lakini hakuna jinsi,Jikaze mkuu,Maisha lazima yaendelee.
Inaumaa Sana bro

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Mkuu tambua hilo jambo lipo tu kumpenda mtu sio dhambi means kuna ishu zinatokea ziko nje ya uwezo wako yeye anaweza kudhania kama humpendi in reality you efforts has limited to accomodate her mfano kuna sehemu ulishindwa kumpa pesa ni tatizo nje ya uwezo wako ila anatafsiri kwamba umembania kama ipo ipo.

Mi 2019 nilishindwa ivyo ivyo kwa demu tulipendana sana nikamwacha aende kwa jamaa aliye na uwezo sio dhambi maana hata mwelekeo wa maisha nilikuwa sina kiroho safi kawekwa mimba jamaa anapanda kumuoa sijajua wanaendeaje ila nilishindwa kama elfu 70 akasema bora tuachane nikasema okey to let her go.

We usiwaze kama ipo ipo
 
Naona unasubilia Meli AirPort!! Hivi wanaume au wavulana wengine hua Kweli mnauelewa kichwani! Hadi ukute mtu yupo kwenye sita kwa sita Ndio utaamini huyo ana mtu!? Wewe uliotoa hii post jipige kifua uambie moyo wako UACHE UFALA!
 
Nilichogundua;
Huyo mdada ndie mwanamke wa kwanza kutembea/kushiriki nae kimapenzi. Mkuu tafuta sehemu tulivu, tafuta rafiki yako wa kiume/kike mwaminifu kaa nae ili mjadiliene kuhusu hatima yako.

Toka na maamuzi magumu, na yachukuwe kiume ili maisha yaende, bila kufanya hivyo utapigwa sana ndugu yangu.

Mimi niliwahi kuambiwa nina mimba yako, nikatumiwa na vipimo lakini nilipogundua kuwa yote yale ni maigizo nilipiga chini haraka, nikabidilisha line ya voda, nikahama kabisa mazingira aliyokuwepo ili kujinusuru na hiyo shida.

Ogopa sana watu wanafuatilia movie za akina Sepetu, muda wote hata ukitaka vipimo watakutumia maana wanatumia hela yako kutengeneza majibu FAKE.

Nakuomba uachane na huyo sister haraka ili kunusuru hali yako kiuchumi, hata ikitokea umemuoa ndugu zako na wazazi wako watapata shida sana maana hatajali yeyote na atakuwa kwako kwa ajili ya kutafuta hela kupitia mgongo wake na siyo kukusaidia kimaisha.

Shutuka ndugu yangu, elewa dunia ya sasa tunahitaji watu tunaofanana na kuongea lugha moja ili kutatua shida zetu, na siyo kutengeneza matatizo FAKE ili upate hela ya kuendesha maisha. Wanawake ni wengi sana mkuu, tafuta mdada anaejitambua na kuelewa dini, mwenye lengo na akili ya kutambua umuhimu wa mchumba/Mme ni nini.

Kila lakheri kwenye majukumu, na Mungu akusimamie uvuke salama. Hii dunia ina watu wa kila aina, jifunze life intelligence na namna ya kusoma mtu kwenye maandiko (sms) na maongezi ukiwa unaongea nae.

Muongo hana kumbukumbu, siku moja unamrudisha nyuma kama vile umesahau ili usikie maelezo yake yatafanana.
 
Back
Top Bottom