Uzi huu nimeweka jukwaa la biashara nategemea michango yenye tija. Tujue kutofautisha biashara na vituo vya kutoa misaada bure, msikiti, kanisa, n.k, THIS IS BUSINESS
Kuna kaduka nilifungua, kwakuwa utumishi umenibana niliweka msaidizi anisaidie.
nikitoa gharama za frame, mshahara, allowance, umeme, usafi, Tra, leseni, n.k. Duka linaingiza faida ya laki 3 hadi 4
msaidizii aliwahi kuniomba aanze kuweka bdhaa zake, Nilichukulia poa kwasababu niliona bidhaa anazouza ni ndogo na ni nje ya biashara nayofanya, Nikamruhusu.
Mshahara naomlipa ni 150,000 kwa mwezi, allowance ya matumizi yake elf 70, jumla 220,000
Leo nilifika dukani hayupo kafunga, nina ufunguo wangu nikaingia, kuna kidaftari nilikiona kwenye draw.
Kapangiliaia vizuri sana hesabu zake, kila siku anafunga hesabu kwa faida ya elf 6 hadi 7, sometmes elf 8
Nilipiga picha fasta, nimefika home nimepiga hesabu, mwezi uliopita kaingiza faida 168,500, Mwezi huu hadi leo kaingiza 87,000 probably anaweza kuingiza 180k mwisho wa mwezi
Kuna maamuzi kadhaa nataka nichukue
- Nimwambie awe anachukua faida asilimia kadhaa kwa biashara yoyote atayoifanya dukani kwangu
- Nisimlipe mshahara wake niwe nampa aloowance pekee, ajilipe mshahara kwenye faida
- Nimpe miezi kadhaa auze, baada ya hapo iwe biashara yangu
Ni jambo liliilonfanya nitafakari sana, nichukue maamuz yapi.