Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😂😂🔥Mchawi sio mpaka aruke na ungo?
Uzi huu nimeweka jukwaa la biashara nategemea michango yenye tija. Tujue kutofautisha biashara na vituo vya kutoa misaada bure, msikiti, kanisa, n.k,
Kuna kaduka nilifungua, kwakuwa utumishi umenibana niliweka msaidizi anisaidie.
Biashara imeshuka lakini kibishi naendelea nayo
nikitoa gharama za frame nayolipia laki 5 kila mwezi (AISEE !!), mshahara, allowance, umeme, usafi, Tra, leseni, n.k. naingiza faida ya laki 3 hadi 4, Kabla biashara haijashuka ilikuwa ni Laki 8+
msaidizii aliwahi kuniomba aanze kuweka bdhaa zake, Nilichukulia poa kwasababu niliona bidhaa anazouza ni ndogo na ni nje ya biashara nayofanya, Nikamruhusu.
Mshahara naomlipa ni 150,000 kwa mwezi, allowance ya matumizi yake elf 70, jumla 220,000
Leo nilifika dukani hayupo kafunga, nina ufunguo wangu nikaingia, kuna kidaftari nilikiona kwenye draw.
Kapangiliaia vizuri sana hesabu zake, kila siku anafunga hesabu kwa faida ya elf 6 hadi 7, sometmes elf 8
Nilipiga picha fasta, nimefika home nimepiga hesabu, mwezi uliopita kaingiza faida 183,500
Kuna maamuzi kadhaa nataka nichukue
- Nimwambie awe anachukua faida asilimia kadhaa kwa biashara yoyote atayoifanya dukani kwangu
- Nisimlipe mshahara wake niwe nampa aloowance pekee, ajilipe mshahara kwenye faida
- Nimpe miezi kadhaa auze, baada ya hapo iwe biashara yangu
Ni jambo liliilonfanya nitafakari sana, nichukue maamuz yapi.
Kwa wale ambao mnaingiza mambo ya huruma, mle mlale
Unapopiga goti kumuomba Mungu usisahau kumuomba moyo wenye huruma na unyenyekevuUzi huu nimeweka jukwaa la biashara nategemea michango yenye tija. Tujue kutofautisha biashara na vituo vya kutoa misaada bure, msikiti, kanisa, n.k,
Kuna kaduka nilifungua, kwakuwa utumishi umenibana niliweka msaidizi anisaidie.
Biashara imeshuka lakini kibishi naendelea nayo
nikitoa gharama za frame nayolipia laki 5 kila mwezi (AISEE !!), mshahara, allowance, umeme, usafi, Tra, leseni, n.k. naingiza faida ya laki 3 hadi 4, Kabla biashara haijashuka ilikuwa ni Laki 8+
msaidizii aliwahi kuniomba aanze kuweka bdhaa zake, Nilichukulia poa kwasababu niliona bidhaa anazouza ni ndogo na ni nje ya biashara nayofanya, Nikamruhusu.
Mshahara naomlipa ni 150,000 kwa mwezi, allowance ya matumizi yake elf 70, jumla 220,000
Leo nilifika dukani hayupo kafunga, nina ufunguo wangu nikaingia, kuna kidaftari nilikiona kwenye draw.
Kapangiliaia vizuri sana hesabu zake, kila siku anafunga hesabu kwa faida ya elf 6 hadi 7, sometmes elf 8
Nilipiga picha fasta, nimefika home nimepiga hesabu, mwezi uliopita kaingiza faida 183,500
Kuna maamuzi kadhaa nataka nichukue
- Nimwambie awe anachukua faida asilimia kadhaa kwa biashara yoyote atayoifanya dukani kwangu
- Nisimlipe mshahara wake niwe nampa aloowance pekee, ajilipe mshahara kwenye faida
- Nimpe miezi kadhaa auze, baada ya hapo iwe biashara yangu
Ni jambo liliilonfanya nitafakari sana, nichukue maamuz yapi.
Kwa wale ambao mnaingiza mambo ya huruma, mle mlale
Hii imekaa poa kabisa jamaa aache kuendekeza tamaa atakuja kujuta mbeleniMuite muweke chini, umueleze kikubwa biashara yako kaiona imedrop, gharama za frem, mshahara na vitu vingine biashara haiendi, yeye anaonaje.. Msikilize kwanza.
Muulize kwake biashara ikoje, kama inalipa vizuri, umuongezee posho, mshahara muuvunje mpaka pale biashara itakapokaa sawa.
Kama kweli anapata faida atakubali.
Lakini mkuu faida ya 180k ndio ya kukutoa roho?
Ilitakiwa amshauri Boss wake aongeze hizo biashara ndogo ndogo Ili mapato ya Boss yaongezeke. Hili nitatizo la wabongo wakipewa ajira wanaangalia namna ya kujinufaisha wao badala yakuongeza mapato katika biashara walizo ajiriwa.Hii roho yako mleta mada ndio wabongo wengi wapo hivyo,
Huruma inakuwa mwanzoni ili mtu ajihisi yupo huru kufanya chochote ili tu awe comfortable.
Najua huko kumwambia ajiongeze kwa vitu vidogo vidogo dukani kwako ilikuwa ni kumfanya awe huru na asijutue kufanya kazi kwako.
Lakini matokeo ya uhuru huo ndio wabongo wengi hawapendi na roho mbaya na chuki juu ya mtu ndio inapo anzia.
Hapo cha kufanya ni umuache aendelee na kazi yake na usimuingilie kwa chochote as long as anakufanyia kazi na anakuingizia pesa kama inavyotakiwa.
Akikuza msingi wake na akiamua kuondoka kufungua biashara yake pia unatakiwa umuache aende .
Wabongo wengi hatuwezi kuajiriwa Wala kujiajiri. Mtu umepewa nafasi ya ajira, badala utumie nafasi hio kukuza biashara ya boss wako, sisi hutumia nafasi hio kuangalia namna ya kujinufaisha. Ni mpumbavu pekee anaeweza ruhusu kitu hicho. Vinginevyo awe ni mtu tajirii ambae kashajipata, ambae anataka kutoka kwenye uuzaji wa rejareja kwenda jumla.Kuna wadau wanasema una roho mbaya lakini siyo roho mbaya umakini unahitajika kwenye biashara,ni kosa kuanzisha biashara ndani ya biashara ya mtu mwingine haina uaminifu,fremu unalipa wewe,mshahara na posho unamlipa,ajiongeze na hela za malipo yake mwisho wa siku aache ajira yako afungue biashara zake.
Hiyo kitu ilinifelisha kwenye biashara kuja kugundua ananirudisha nyuma,aliomba aanzishe biashara yake ndani ya kwangu mwisho wa siku anajikopesha bidhaa zangu atumie kuendesha biashara yake humo humo,mwisho wa siku hata katon ya maji ataleta ataacha yako yake itoke kwanza ndo auze yake we unashangaa mbona bidhaa hazitoki kumbe ana zake humo anazitoa kwanza. Nikajiuliza mi nikikaa kwenye biashara siku sina kazi naingiza hela kubwa kuliko siku yeye akiwa mwenyewe.
Hakuna tamaa hapo, yupo sawa nikosa kuanzisha biashara ndani ya biashara ya mtu mwingine. Ilitakiwa aangalie namna yakuongeza faida ya Boss wake, kwa kumshauri waongeze bidhaa hizo ndogo ndogo. Automatically na boss angefikiria kumuongeza bonas au mshahara kwa kuona kijana aliemuweka ni mbunifu. Kwa hali hii wa Tz tutaishia kuwa machinga tu.Hii imekaa poa kabisa jamaa aache kuendekeza tamaa atakuja kujuta mbeleni
Nilitaka nimuambie kitu Kama hili.Tena huyo kukuibia hawezi maana anajipambania mwenyewe pia
Huo mshahara ni mdogo sana.Hakuna tamaa hapo, yupo sawa nikosa kuanzisha biashara ndani ya biashara ya mtu mwingine. Ilitakiwa aangalie namna yakuongeza faida ya Boss wake, kwa kumshauri waongeze bidhaa hizo ndogo ndogo. Automatically na boss angefikiria kumuongeza bonas au mshahara kwa kuona kijana aliemuweka na mbunifu na muaminifu.
Mindset za biashara nikua ukisharuhusu hicho kitu, basi kijana ataangalia biashara nyingine ambayo haipo dukani kwa boss wake ataongeza, mwisho wasiku atampoteza huyo kijana.Huo mshahara ni mdogo sana.
Mwingine angewza kumuibia bosi au kuacha kazi.
Angalau huyo kaomba hiyo nafasi ili abakie muaminifu kazini.
Hapo inatakiwa asifanye biashara ambayo inafanana bidhaa na mwenye duka.
Ikiwezekana kila anapoleta bidhaa zake mpya amjulishe mmiliki wa duka thamani na idadi yake.
Amuwekee kikomo Cha ceiling ya mtaji au ukubwa wa biashara yake huyo kijana. Ikifikia hapo wajadili partnership au aondoe au akubali iishiie kiwango hicho tu.
Amuwekee malengo ya kufikia biashara ya bosi wake. Mfano atakiwe kubuni bidhaa mpya za kufikia hayo malengo n.k.
Watanzania weusi wenzetu wengi wagumu kufanya hiki kitu.Mimi mahala napofanyakazi kama tukifanikiwa kuingiza faida nzuri kwa boss wetu, pindi unapo renew mkataba boss wetu anatupa bonas kulingana na performance ya mwaka huo. Kwahio Kila mtu hulazimika kufanya kazi Ili impact yake ionekane.