Nilimsomesha binti akaishia kuwa mcheza show

Nilimsomesha binti akaishia kuwa mcheza show

never na wala sijawahi kufikiri, mambo haya sitofanya kwenye maisha yangu yote 1.sitonunua malaya kwa pesa (namini ni chukizo) 2. sotomlala mwanamke bila ridhaa yake 3. sijawahi kuwaka tama kwa mabinti niliokaribu nao
Never say never,,
 
Naandika hili hapa kwa moyo mkujufu, sina kinyongo na wala sijutii ila namhurumia sana.

Mwaka 2015 ilikuwa ni first appoitment yangu as mwalimu, nilimkuta huyu binti akiwa kidato cha tatu, baada ya miezi mitatu niligundua ni mtoto mwenye uwezo wa juu darasani.

Baadae nikaja kufahamu kama ni mtoto wa mazingira magumu, baba yake alifariki na mama yake yupo anaishi mazingira magumu sana na yupo Tabora kwao. So kwa kuzingatia uwezo wake na kukutana na bibi yake niliamua kumsaidia suala la shule as mdogo wangu na itabaki kuwa hivyo milele, i rate her as my young sister.

Mungu si Athuman form four alifaulu vizuri, nilifanya mchakato wa kumfanya achuguliwe shule za jirani na combination iwe PCB, nashukuru alichaguliwa shule na comb. hiyo, so nikawa namhudumia kama mdogo wangu na nilimshukuru Mungu kuwa umenipatia mtu ambaye ananipa experience ya kusomesha.

Na hata form six alifaulu bahati mbaya hakuchagulia course za afya, so ilibidi nikae nae tutafte course ambayo itampa ajira na akikosa ajira iwe rahisi kujishikiza, na ikawa hivyo.

Alichaguliwa chuo na akapata course ambayo tulitarget, alipokuwa chuo niliendelea kutake care asilimia zinaboki za bodi ya mikopo na kumpatia fedha za matumizi kama mtoto wa kike tena mwanachuo (nilifanya hivyo kwa moyo mkujufu as namsaidia mdogo wangu).

Alipokuwa chuo mwaka wa mwisho kabla ya semister ya pili alikuja rafiki yangu na kuniambia amekutana na mdogo wangu huyo na binti mmoja msagaji, tena kamuliza yule msagaji na msagaji kakili kuwa yule binti ni msagaji na ukizingatia ni tom boy ilinichanganya sana.

Sikuona shida nilimpigia kumuliza hilo na kweli kuwa hayupo chuo yupo mtaani, akajibu kuwa ni kweli yupo mtaani kuna likizo fupi na yeye sio msagaji wanamsema vibaya kwa sababu ya muenekano wake wa u Tom boy (nakumbuka hiyo simu ilikuwa ya mwisho kuonanana naye wala kuwasiliana, kila nikipiga simu hapokei na akipokea haongei.

Kinachoniuma ni pale nilipopiga hesabu kuwa amemaliza chuo na sasa yupo mtaani (hata kunijulisha nimemaliza chuo hakufanya hivyo, I said ni utoto unamsumbua), badaye niliamua kumtaftia kazi baada ya kumpigia na kuona hapokei niliamua kutuma sms hakujibu, na kila nikimuona yupo mtandaoni na anarusha video zake akicheza music.

Namhurumia kwa sababu sioni future kwa anachokifanya ila ndio hivyo sina njisi ya kukaa naye, najiwazia sasa kama ningesomesha mwanamke kwa hoja ya mapenzi ingekuwaje, si ningepanic mimi? All in all nashukuru Mungu atakachonipa kama kinaweza kugawanywa na kuwafikia wengine i will do it, sijakata tamaa.
Waingereza wana msemo "No good deed goes unpunished".

Waswahili wanasema "Tenda wema nenda zako, usingoje shukurani".

Huyo mtu hana obligation yoyote ya kupokea simu yako.

Shika hamsini zako.
 
Aisee Mzee Raza mtu unaweza usiwe na lengo baya ila mtoto wa kike akifika form five anabadilika na kuwa dada mkubwa na utamu kuanza kuonekana.. hadi afike chuo tayari tunda linakuwa limeiva kabisa. Kwa wakati huo shetani anakuwa anakushawishi kula tu umegharamia sana.. na ukicheki toto kweli limekaa mkao. Kama hauna msimamo lazima uteleze. Bila kupepesa macho ndo anachopitia huyu TICHA.. Tumwombee mwalimh wetu asiingie dhambini.
Cc mpwayungu village
Hatari sana ndugu, haya mambo ni magumu mno kwa kweli.
 
Hongera kwa kuwa na moyo mzuri wa kujitoa. Ki ukweli katika maisha wanasema ukifanyiwa wema hata kama usipomlipa mtu basi kumbuka hata kutoa shukrani. Naamin hata maandiko ya biblia yanasema hivyo. Na siku zote inaleta moyo pale unapomsaidia mtu msaada ule uzae matunda hata kama asipokusaidia basi abadilishe hali ya nyumbani kwa kuwa msaada mzuri kwa ndugu na jamaa zake. Sema ndo hivyo binadamu huwa tunasahau maisha ni nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa tumekisamehe kwa kukosa aya kwenye uandishi, tumekusamehe kwa kuumia moyo lakini ticha, ndo usitupe hata username yake tuone mauno?
 
Hivi uwongo unawasaidia nini, nani anawalipa? Peleka haya mauwongo yako kwenye majukwaa ya kipuuzi. Mara nilifanya mchakato wa kumfanya achaguliwe shule za jirani.

Hapo yu ni uwongo, we ulikuwepo wakati wizara inawapngia shule za kwenda A level? Yote umeandika hayana mantiki, upoyoyo tu.
Jf kuna watu
 
Back
Top Bottom