Nilimtelekeza mke wangu, nimerudi nimekuta rafiki yangu kamuoa

Nilimtelekeza mke wangu, nimerudi nimekuta rafiki yangu kamuoa

Yaani kuna baadhi ya binadamu akili zao sijui ziko miguuni wanazitembelea tu.......

Hivi unammilikishaje mwanaume mwingine nyumba????

Naona wife mahaba nichanganye ya shemeji yake yamemvuruga.....sasa tulia aone huyo shemeji mume atakamvyomgeuka...hahahaha wanawake wengine viazi kweli
 
Mwanamke akibadilisha uelekeo ni ngumu sana kumuweka Sawa, ila usikate tamaa.!
 
Mkuu, kwa uelewa wangu mdogo: Among others, sababu zifuatazo (as per Sheria ya Ndoa ya 1971, Revised 2002) zinaweza kuishawishi mahakama kuamini kuwa NDOA husika hairekebishiki tena (the marriage has broken down beyond repair) na kisha kuivunja na kutoa TALAKA kwa muombaji-talaka (the petitioner):

(a) Kutelekeza mke (desertion) kwa zaidi ya miaka mitatu;
(b) Kutengana (separation) kwa zaidi ya miaka mitatu;
(c) Under 'presumption of death' (Dhana ya kifo), kwamba mtu akipotea kabisa without knowing his whereabouts for 7 years, then anadhaniwa kuwa ameshakufa.

Now, considering the circumstances za issue yenyewe, mleta uzi alimtelekeza mke wake tangu 2009 mpaka 2014. So kuhusu kuibatilisha hiyo talaka ni ngumu. Ila kuhusu nyumba pamoja na mali walizochuma pamoja wakati wa ndoa yao, still there are avenues possibly for him to secure back the assets. Apambane!

-Kaveli-

Well and fine....apiganie nyumba hata kama kwa kugawana.
 
Du kaka wewe ni source ya matatizo yote hayo miaka yote hiyo ulitegemea mkeo aishije na watoto, hata kama angeuza nyumba yako angeshaimaliza hela hiyo. Hivyo muombe msamaha na nyumba mwachie na kikubwa watoto wapo mshukuru Mungu.
 
Pole sana ndugu, hayo yote ni mitiani ya dunia chamsingi piga miyo konde huna haja ya kumshtaki uyo bibie,

mwachie MUNGU wewe tafuta kukaa na watoto wako, mwachie hiyo nyumba,

tengeneza maisha yako na watoto wako, maana sidhani kama utarudia makosa ya nyuma ndugu yangu,

maani usijilaum pindi unapokosea bali jifunzi na utafakari ni wapi ulipo anguka ili usianguke tena,

mwisho
rudi kwa MUNGU maana dunia na vyote ni ubatili yeye atakuongoza katika njia iliyo nyooka,

na utaishi maisha ya furaha na Amani, yenye baraka tele, maana kwake hakuna majuto,
 
Ndo maana huwa siwahitaji marafiki kwenye mahusiano yangu kabisa.
Ubadilishe jina la hati ya nyumba unajitafutia kifo
 
Hivi kwa hali ya kawaida mimi nikijiangalia nikikimbia familia yangu na endapo mke wangu hafanyi kazi miezi mitatu tu hali itakuwa tete???? think about it? Then mtu anakuja kujilalamisha hapa eti mke ana kosa that is stupid !! Hebu kwa mfano nyumba yako hiyo ingekuwa mil. 50, matumizi ya watoto wadogo wawili na mama yao ya miaka uliyotoka si zaidi ya hiyo hela??? maana life style yako wewe mwenyewe umetuambia, hukuwa unaishi maisha yako, life ilikuwa juu. Ningekuwa hakimu ningekuweka ndani kwa kumsumbua huyo mdada ili wanaume wengine waone uchungu wa kukimbia familia.
 
Mkuu ww ndo umesababisha hayo yote,kama kipindi ulikuwepo unasema pesa ya kula ilikuwa inataka kukupiga chenga na ulikuwa huna mradi wowote vp kwa wife wako yeye angefanyaje? Kwanza mshukuru huyo rafiki yako kwa kulelea wanao cha msingi PIGANIA KUBADILISHA HATI YA NYUMBA TU MENGINE ACHANA NAYO .
 
Hukutakiwa kukaa muda wote bila mawasiliano yaani ulitaka mwanamke akae miaka 5 bila kupiga ororo wakati huo huo huna mawasiliano nae.
 
HONGERA KWA KUPIGANIA MAISHA
Ulipokosea Ni Kuondoka Bila Kutoa Taarifa Hata Kwa Ndugu Yako Mmoja Ambae Japo Angekuwa Anaenda Kusalimia Familia Yako.
Japo Wengi Tunamlaumu Mke Wake Hivi Ungekuwa Wewe Miaka Mitano (mtoto Miaka3) no taarifa yoyote ungesubiri?
Tena anaakiri kiasi maana mwingine angeiuza kabisa, na bila shaka na mwenyewe uliyatarajia ndo maana hujamuanzishia bifu rafiki yako.
Hyo ilikuwa plan B ya mkeo ili aishi na watoto ila alikosea kuweka jina la jamaa
 
Pole sana mwenye makosa yote ni wewe mwenyewe huwezi muacha mkeo kipindi chote hicho bila taarifa yoyote,kikubwa pigania hiyo nyumba tu,hatuwezi jua ilikuwaje mpaka jina likabadilishwa labda mkeo aliuza jamaa akainunua na akaamua kuoa kabisa.
 
Namfahamu mama mmoja aliyefiwa na mme wake akapata mwanaume wa kuishi naye
yule mwanaume akawa anamtaka amwonyeshe hati za nyumba,yule mama alimgomea
akasema hizo nyumba ni mali ya watoto wenye baba yao aliyewatafutia.Akamshauri
watafute fedha wajenge za kwao,yule mwanaume hakuwa tayari
ila alianza vitimbwi vya uchawi na yule mama akambwaga huyo mwanaume asiyejitambua.
ilikuwa bahati yake kwamba alimshtukia mapema.

Nawashauri wadada kama imekutokea ukalazimika kuolewa tena ,usifanye kosa
la kubinafsisha mali uliyotafuta na baba watoto wako utakuja kujuta.
Huenda huyo mdada aliyekufanyia hayo,yupo humu jf
namshauri atubu,na hata akitubu ni vyema akabatilishe hizo hati bandia
maana muda si mrefu yatamtokea puani,asisahau urembo ni maua tu
makunyanzi ya usoni yakijitokeza lijamaa litatafuta bibie mwingine
na nyumba limeishamilikishwa atalia kilio cha mbwa wakati hakuna wa
kumuhurumia.Bro chukua watoto wako usijaribu kumrudia huyo mmama
anaweza kukuua,pambana upate haki yako na watoto.Ila kama ulikosea ukasajili
kiwanja kwa jina la huyo mdada itakughalimu japokuwa kama una lisiti ulizokuwa unanunulia
vifaa vya ujenzi zinaweza kukupa haki yako.kama na lisiti zote zimeandikwa majina yake
basi hapo usipoteze fedha kuendesha kesi maana hutashinda,itaonekana alikuoa kisha ukaondoka
kama ulivyokuja.
 
Pole sana ndugu,inawezekana huyo jamaa alikuwa anakuchapia mkeo hata kabla haujamkimbia,mm nadhani muachie tu hiyo nyumba mkeo cha msingi mshauli hiyo hati iwe kwa jina lake au la watoto na nikwa faida yake na ya watoto pia,muache aendelee na maisha yake ila mkubaliane tu vizuri namna ya kuwalea watoto.
 
Kaka ulikosea kujisahau kazini na hizo hela ulizokuwa unapata.
Ungeweka miradi ya kutosha mapema.
Ila umeshajifunza.
Kila la kheri ktk kufuatilia haki zako.
 
Imeniuma sana hivi huyo rafiki yako ana kazi gani haswa mpaka akampata mkeo?
au Mkeo alikuwa ni kigeugeu na akakutingisha
pigana Mwanawane rudisha nyumba yako na watimue kabisa
ikiwezekana iuze ukaendeleze huko Mvumoni
 
Pole sana. Mungu huwa haangalii makosa yetu yy huwa anasamehe siku zote. Hata kama ulikosea ww ni binadamu hujakamilika. Mungu atakupigania upate unachostahil kupata . Amen
 
Umekosea mahali pamoja kwa kuhoji hiyo ndoa mahakamani,achana naye huyo mwanamke,pigana upate nyumba yako kwanza. Atakuwa amewadhibiti watoto wakuchukie kwa kujifanya anawapenda sana,pigania nyumba kisha watoto baadaye maana hamna njia ya kubadilisha watoto kwenye ubin wako.. Hizi story ni kawaida siku hizi wanawake ni wa kuchunga sana. Kuna rafiki yangu mmoja mkewe akimkazania sana awaandikie nyumba yeye na watoto,yule rafiki yangu akaniomba ushauri,mimi nilimwambia asifanye hivyo,hakunisikia,akaniambia nimsindikize kujua taratibu za kubadilisha jina,kule tukamkuta mtu wa busara sana naye akamshauri kama mimi na hatari iliyoko mbele yake kuwa akishawaandikie inakuwa si ya kwake tena wanaweza kumtimua wakati wowote,hakusikia. Ilifika wakati bwana yule akawa hana kazi starehe za pombe na outing tena hakuna,mke akaanza kumfanyia visa,anaenda kulewa anarudi nyumbani muda anaotaka. Bwana akachoka na visa siku moja akamkung'uta vizuri,mtoto wa kiume akaingilia kati na kupambana na baba yake na mwisho jamaa akatimuliwa kwenye nyumba,saa hizi anapanga vichochoroni. Hawa jamaa wa kuchunga sana
 
Kosa lako ni kukimbia mke. Mshukuru jamaa yako kakusaidia kulea watoto. Ila kamla mkeo peku peku hadi kampa mimba ila kukimbia mke ndio kosa lako.
Cha munimu usiumie moyo. Yote ni maisha
 
Back
Top Bottom