dah kumbe ni hivi
kuna dada mmoja yeye mumewe alijenga nyumba ila hati ya hiyo nyumba ipo WAZO aliweka JINA LA KAMPUNI yake
makusudi mazima sasa alimfumania mkewe na mwanaume mwingine alichofanya kaenda mahakamani kudai talaka kesi
ilisikilizwa mwanaume alimwachia mkewe samani zote za ndani kwakuwa walipanga apartment mikocheni, rent
ilivyoisha mwanaume akachukua nguo zake tu na kusepa akamwacha mkewe na watoto 2 , kwa kuwa rent iliisha mkewe
alimtaarifu kuhusu rent mumewe akamjibu mii nataka talaka siwezi kuishi na wewe na hao watoto chukua na vitu vyote
chukua , sasa dada amechanganyikiwa watoto walizoea kusoma Genesis yeye hana fedha ya kuwasomesha huko kifupi
ameshapewa talaka sasa where is justice in such a circumstance if you won't mind nimeona umejibu murua na subsection nini dah
Basically, TALAKA ikishakuwa granted by court, hufuatia IMPACT kuu 3:
(a) Kugawana mali za ndoa (distribution of matrimonial properties). Hapa mali zinazohusika ni zile tu zilizopatikana/zilizochumwa wakati wa uhai wa ndoa (jointly acquired during the marriage). Na hapa ndipo huibuka swali la je "yupi anapata kiasi gani?" (katika huo mgawanyo wa mali), hili tuliache kwanza.
(b) Custody of the Children. Uangalizi na malezi ya watoto. Generally, Sheria ya Ndoa inataka mtoto aged under 7 years, aishi kwa mama. Notably however, katika ku-grant custody ya mtoto, mahakama huzingatia sana maslahi bora ya mtoto (the best interest of the child). Kwamba ni upande upi mtoto akiishi ataenjoy na kupata haki zake zote za msingi including malezi bora, elimu, n.k. Hili limekuwa sensitively reflected kwenye Sheria ya Mtoto ya 2009.
(c) Maintenance of the children. Matunzo ya mtoto. Sheria ya ndoa inaeleza clearly kabsa kwamba jukumu la matunzo ya mtoto/watoto ni la baba (biological father. Matunzo hayo ni including basic needs kama chakula, mavazi, pia elimu, afya, n.k. Note: suala la matunzo ya mtoto liko pale pale hata kama hamkufunga ndoa, hata kama umemzalisha tu. Nadhani unakumbuka mahakama ilivyoamua ile kesi ya HOUSE GIRL Vs IGP MAHITA, juu ya matunzo ya mtoto, mpaka vipimo vya DNA vilitumika na Mahita akawa bound!! However, mama anaweza saidia matunzo ya mtoto endapo baba hajiwezi kabsa kiuchumi.
Kwaiyo, kama kuna mtoto/watoto na mali za ndoa, mahakama inatakiwa i-compromise izo inshu 3 hapo juu (a to c) in alongside with issuance of TALAKA.
So kuhusu case ya huyo mdada, kuna possible legal channels mbili: (1) Umesema walikuwa wanaishi nyumba ya kupanga, ila kuna nyumba ilijengwa na ikawa registered with Hati Miliki ya kampuni ya mwanaume. Japo hujaeleza kama nyumba hiyo ilijengwa wakati wa ndoa ama kabla ya ndoa. Now, kama ilijengwa wakati wa ndoa, possibly anaweza akapata haki yake ktk hilo, kwa ku-determine mchango wake wa hali au fedha au huduma kwa mume. Arudi mahakamani ku-establish hiyo issue ya nyumba in terms of mgawanyo wa mali za ndoa, note: kama tu ilijengwa wakati wa ndoa!
(2) Aende mahakamani kufungua kesi ya "matunzo ya watoto" dhidi ya baba wa watoto.
WITH EMPHASIS: ni jukumu la baba kuprovide full matunzo kwa watoto wake, huwezi kulikwepa hili kwa mlango wa sheria. Ila kibongo-bongo, akina mama wengi wanaachiwa watoto na kuhangaika nao pekeyao. This is due to the fact that watanzania wengi bado hatupo courageous (not aggressive) kudai haki zetu throuh legal settings zilizopo. Pia our systems for dispensation of justice bado zipo ineffective and very corrupt! So ili kuepuka legal complications plus kupoteza muda na pesa kufuatilia kesi, akina mama wengi huamua kupotezea tu na kukomaa kulea/kutunza watoto pekeyao.
Mkuu, I hope maelezo yangu yamekidhi hoja yako kwa kiasi fulani, japo mwanga wa kuanzia. Naamini wataalamu zaidi wa sheria watatoa michango yao pia. Also, my sincere apologies if my writing irritates, maana nimeandika kwa simu!
-Kaveli-