Nilimtelekeza mke wangu, nimerudi nimekuta rafiki yangu kamuoa

Nilimtelekeza mke wangu, nimerudi nimekuta rafiki yangu kamuoa

mhhh una haki na mali yako tuu...

the rest ulikosea telekeza family bila taarifa. akikushitaki thru family law unamakosa.
kwa sheria ya land and mortgage utashinda nadhani.
 
mkuu Kaveli darasa uliotoa limeniingia vilivyo, asante
 
Last edited by a moderator:
mhhh una haki na mali yako tuu...

the rest ulikosea telekeza family bila taarifa. akikushitaki thru family law unamakosa.
kwa sheria ya land and mortgage utashinda nadhani.

Ni kweli, ila makosa yangu hayafuti ya kwake pia
 
bobby freetown

Kweli umekosea na lawama ni za kwako maana ulivyoondoka kimya kimya ulidhani yeye angeota upo angol?
 
Last edited by a moderator:
hujakoseam kabisa maamuzi magumu ndio yamerudisha mafanikio na njia nzuri...labda ulikosea kuchgua mke ambaye ukifulia anakulaumu hataki ukatafute af analalamika...huyo hafai kuendekezwa af kwa ujinga wake anabadili hati kumpa mwanaume umiliki....mjinga sana...kuchagu atuu ulibugi ila mengine big up komaa mali ni za watoto wako hapo
 
2006 - 2009 ulikua beach Nimekuelewa mnoo!!! Dah umenikumbusha maisha ya kibeach boy Ndani ya Capetown 2007 inataka moyo wa kishujaa...Awali ya yote pole sana tafuta wakili mzuri utashinda
 
Mh.Kaveli asante kwa darasa lako nina swali hapa kesi kama hiyo ya wanandoa kuoa au kuolewa bila ya kupeana talaka.Kwa mfano mume na mke wametengana kwa zaidi ya miaka mitano,mume akaamua kuoa bila ya mke kujua baada ya hiyo miaka mitano,sheria inasemaje hapo iwapo mke ataenda mahakamani kudai haki yake.
 
Chai bora tuinywe chai bora


Hahahahahaj

Kweli chai bora....katunyweshaje

Mnagunduaje kwamba ni chai? Nimerudia×2 nimeshindwa kuona mnachosema, mtusaidie mawazo

Pia nimeona umechangia mwanzo watu8 amekuja kusema chai umeungana nae so anakushikia akili (hypocrisy) anyway napenda kujua mnajuaje, otherwise kama ni assumption then mnamkosea heshima na haki yake mleta Uzi

Thanx
 
Salam zenu wanaume wenzangu,

Mwaka 2006 nilipata matatizo kazini, nikafukuzwa kazi tulishikwa red handed mim ina mwenzangu tukiuza mafuta ya kampuni, nilikua nafanya kazi kwenye kampuni ya mafuta Kurasini.

Kwa kweli nilikua na hela sana kutokana na kitengo nilichokuwepo, mabosi walinitumia mimi kuiba mafuta ya kampuni na mwisho tunagawana.Bahati mbaya mabosi waligombana mmoja akaamua kutuchoma, dili likabumbuluka na jumba bovu likaniangukia mimi ukawa ndio mwisho wangu hapo.

Siwezi kuwaficha wana Jf, nilikua nimeoa mwanamke mwenye matumizi makubwa sana, alipenda kula na kuishi vizuri na kuvaa kila fashion iliyoingia mjini alitaka awe nayo, na kwa kuwa ni mzuri ajabu nililazimika kutoa gharama na huduma hizo kwa kuwa hela nilikua nayo.

Sasa nilipofukuzwa kazi, alinibadilikia sana ndani, nyumba ikawa kaa la moto, niliambiwa maneno mabaya sana, hata hela ya kula ilianza kunisumbua, sikua nimesave wala kuweka mradi wowote wakati nina hela zaidi ya kujenga nyumba tuliyokua tunaishi,Marafiki wote tuliokua tukinywa bia pamoja walianza kunikimbia baada ya kuona nimekua mtu aa mizinga.

Nikapata wazo la kwenda Angola migodini, kuna mshikaji alinipa dili hilo, alikua huko siku nyingi, ila alisema ni kugumu sana, sikua na choice nikaamua kwenda, tulisafiri na basi kupitia Zambia.

Kwa kifupi nilimtoroka mke wangu na watoto wawili, nilijua wazi asingekubali mimi kwenda Angola, hata humu TZ alikua anakataa nisiende mikoani kutafuta, alikkua anadhani somehow muujiza utatokea hali ya pesa irudi tena bila fighting na hapo hapo akaendelea kunilaum sifanyi kitu kwamba nimekaa tu, hiyo ndo sababu niliamua kumtoroka na kwenda Angola kutafuta maisha.

Nimekaa Angola tangu 2009-2014 , tangu 2006 hadi 2009 nilikua bench tu.Nikiwa Angola nilisota kama miezi 8 hivi baadae nikawa napata ajira za muda katika makampuni yenye tenda kwenye migodi kama ya drilling na construction na kadhalika.

Sikutaka mawasiliano yoyote na nyumbani, si mama yangu, mke wala ndugu yoyote, walikua wamenizomea na kunicheka sana nilipokua juu ya mawe, hivyo niliamua kutafuta kimya kimya hadi nifanikiwe ndipo nirudi nyumbani.

2014 July, nikarudi Dar kwa Mara ya kwanza tangu 2009, sikurudi nikiwa tajiri, Bali nilirudi na msingi wa kuanza upya maisha, nilikusanya kiasi cha kutosha kuanza biashara na kujitegemea kiuchumi.

Surprisingly, nimekuta mke wangu ana ujauzito wa pili (ameshajifungua kwa sasa) tayari akiwa na mtoto mwingine mkubwa wa miaka 3, mbaya zaidi nikakuta rafiki yangu wa karibu anaishi na mke wangu kwangu kinyumba na ndie baba wa hiyo hiyo mimba na watoto wanadai wameshaoana kisheria kwa mkuu wa wilaya wakati hakuna talaka yoyote iliyotolewa na Mahakama yoyote ile hapa Tanzania kuvunja ndoa yetu ya awali.

Maana yeye ana claim hiyo ndio basis ya kuchukua hiyo nyumba yangu na kujimilikisha na sasa yanasomeka majina ya huyu rafiki yangu na yeye na sio majina ya watoto.

Sasa tuna kesi Mahakamani niliyoifungua mimi, nikiiomba Mahakama kubatilisha hiyo hati, iliyofanyiwa transfer kwa udanganyifu, pili mahakama itamke ndoa hiyo ni batili maana ndio iliyozaa udanganyifu wa hati.

Pia ndoa hiyo imefungwa huku kukiwa na ndoa nyingine halali ambayo wahusika waliidanganya ofisi ya mkuu wa Wilaya.
Mwisho nimeomba custody ya watoto wangu nikae nao mwenyewe maana anawakatalia pia

Wana Jf sio kwamba namuhitaji huyu mwanamke tena, bali nahitaji hiyo nyumba iwe ni mali ya watoto wangu kwa sasa imebinafsishwa na hawa wapenzi wawili.

Tangu nimerudi nimejenga nyumba yangu mivumoni tegeta ambapo nakaa, nafanya biashara zangu ni mfanyabiashara wa kipato cha kati, na napati kazi nyingi Angola ambapo huwa nakwenda Mara kwa Mara Kwa shughuli zangu, hivyo naendelea vizuri sana.

- Kuna pahala nilikosea katika haya yote?

- Naweza kubeba sehemu ya lawama kwa kitendo alichofanya huyu mama?

- Je, naweza kushinda hii kesi kwa mtazamo wenu?

Hakuna ulipokosea mkuu....Endelea kumtumaini Mungu aliyekuwezesha kupita katika jaribu hilo. Siku moja huyo mwanamke atakujia akiwa analia.
 
Hebu muache mwenzio alee watoto na ampendae....
 
Ndugu usidandie treni kwa mbele.....

Mimi nimemuelewa Watu8 alipoweka wimbo wa chai

Kama unahitaji kujua alimaanisha nini muulize

Mwisho nina maamuzi ya kukomenti chochote kwenye uzi au komenti yoyote


Mnagunduaje kwamba ni chai? Nimerudia×2 nimeshindwa kuona mnachosema, mtusaidie mawazo

Pia nimeona umechangia mwanzo watu8 amekuja kusema chai umeungana nae so anakushikia akili (hypocrisy) anyway napenda kujua mnajuaje, otherwise kama ni assumption then mnamkosea heshima na haki yake mleta Uzi

Thanx
 
Last edited by a moderator:
Wazo langu la kuitelekeza familia nimeliahirisha kutokana na. Uzi huu hadi hapo ntakapotangaza tena.Ijumaa Kareem

Ukiitelekeza nayo ITAKUTELEKEZA. si umeona jamaa hapa "wamemkata" na kwenye mahesabu kama mwaanafamilia wamemtoa. Angalia "USIKATWE".
aljumaa mubarak
 
Back
Top Bottom