Nilimtelekeza mke wangu, nimerudi nimekuta rafiki yangu kamuoa

Wakuu nawashukuru kwa ushauri na mawazo yenu, nimefarijika sana

Lengo langu sio kumrudia ex wife wangu, mtu mwenye watoto wawili Wa mwanaume mwingine nitake kumrudia? Nitakua kichaa

Nachotaka ni nyumba yangu isiende kwa mwanaume mwingine wakati watoto wapo pale, kama ningekuta majina kwenye hati yapo ya kwangu vile vile, ningekaa kimya kabisa hata pamoja na huyo jamaa kuishi hapo kwangu

Sababu za Ku challenge ndoa yao ni kwa kuwa ndoa hiyo ndio chanzo cha nyumba kubadilishwa hati,
Waliitumia ndoa hiyo kama kigezo

Hata hivyo nina makazi mazuri sasa, hivyo nachopigania ni haki ya watoto na si mm

Mkuu nimekuelewa vizuri sana. Nakushauri tafuta mwanasheria akusimamie kwenye hili. Wewe komaa na nyumba yako tu, full stop. Halafu jifunze kutokana na makosa, BINAADAMU YEYOTE si mtu wa kumwamini 100% hata kama ni mkeo/mumeo/mwanao. Ungehakikisha kabla hujaondoka umebeba document zako zote na kuziweka mahala salama. Shukuru kwamba nyumba ipo, what if ungekuta alishaipiga bei na hela amekula na hana senti tano?
 
si uachane na vyote uanze moja..huo mda utakaopoteza kwenye kesi na gharama utakuja kujutia one day...samehe nyumba..watoto watakutafuta wakikua...life z uaz
 
Jamaa amemsitiri mkeo uliemtelekeza na watoto.

Ulitaka wawe machokoraa?
Karucee, uko right sana, hivi miaka yote hiyo hakuwahi kufikiri huyo mkewe na watoto wanakula nini? ANGALAU ASHUKURU ANA RAFIKI MZURI AMEKUBALI KUPOKEA MATATIZO YA MKEWE NA AMESAIDI KULEA WATOTO SALAMA, NA AMEWAKUTA SALAMA.

Aisee pole kiongozi...Ila wanaume jina wapo wengi sana tu miaka hii.
 
Nashukuru mkuu kwa mawazo yako mazuri

Katika kesi hii ex wife hakuomba talaka mahakamani kabla ya kuolewa upya, aliolewa tu, sheria inasemaje kuhusu hili? Hapaswi kupata talaka kabla ya kuolewa upya?

Je kama mtu amepotea na Kuwa prounanced dead au presumed dead, je ex wife wangu hakupaswa kufuata taratibu za kisheria ili mamlaka husika zini presume mm dead? Au yy mwenyewe kisheria ana mamlaka hayo?

Let say alikwenda polisi akaripoti, ikapita miaka 3 hakuna taarifa Mpya kutoka polisi wala kwa ndugu, je anaweza kuamka tu kesho na kwenda kufunga ndoa nyingine?

Maana Haya niliyoorodhesha hapo juu hayakufuatwa

Na pia lengo langu sio kumrudia mke awe Wa kwangu, na challenge hiyo ndoa kwa kuwa ndio chanzo cha hati kumilikishwa Mme Mpya

Na pia unapompeleka mtu mahakamani na mashtaka mengi inakaa vizuri zaidi kuliko kumpeleka na shtaka moja tu la hati ya nyumba

Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa, nchini Tanzania tuna aina (types) mbili za ndoa:
(a) Ndoa ya mke mmoja (Monogamous marriage)
(b) Ndoa ya wake wengi (Polygamous).

Hivyo, ni hiari ya partners kuamua na kukubaliana wao wenyewe waishi kwenye ndoa ya aina gani kati ya hizo hapo juu. So mnapofunga ndoa, mnapewa Cheti cha Ndoa. Cheti hicho, among other particulars, huonesha ni aina gani ya ndoa iliyofungwa na wahusika/wanandoa.

Kisha, kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa, kuna taratibu/namna 3 za kufungisha ndoa. Yaani taratibu au namna ya kuzifungisha hizo ndoa hapo juu (a) or (b). Taratibu hizo ni:

(i) Kidini. Utaratibu huu unawahusu wakristo, waislam, na wenye imani zingine za kidini.

(ii) Kiserikali. Utaratibu huu unatumiwa na mtu yeyote yule bila kujali imani za kidini, mfano wanandoa wana imani tofauti za kidini labda huyu ni muislam na mwenzake ni mkristo. Watu wengi wanaovamia waume/wake za watu hukimbilia kwenye utaratibu huu coz ni utaratibu ambao ni wa fasta na hauhitaji mashahidi wengi wala masharti mengi kama ilivyo kwenye utaratibu wa Kidini. Ndoa zinazofungwa kwa utaratibu huu wa kiserikali hufanyika katika offisi za Wilaya, na husimamiwa/huendeshwa na msajiri (Registrar) wa Wilaya. Katika utaratibu huu ni rahisi sana mtu kudanganya kuwa hajaoa/hajaolewa, maana ni watu wachache tu wa karibu na marafiki ndo wanahudhuria kama mashahidi, kwenye chumba/office, Registrar anakuja pale, mnaapishwa viapo, anawafungisha ndoa, watu wanapiga vigelegele, kisha mnaondoka zenu. Simply like that!!!!

(iii) Kimila. Utaratibu huu mara nyingi hufanyika kule vijijini. It varies from tribe/customs to tribe/customs. Hawaendi kanisani wala serikalini, bali ndoa inafungwa kwa mujibu wa misingi ya mila husika za wanandoa. Mfano kuna baadhi ya makabila, wazee wenye hakima/busara upande wa muoaji wanaenda nyumbani kwa mwanamke ili kujadili mahari, kisha inapangwa siku ya kuja kuchukua mahari (mara nyingi huwa ni mifugo kama ng'ombe, mbuzi, n.k). Then inapangwa siku wazazi wa pande zote mbili wanakutana kwenye ka-ceremony ka kunywa pombe na kufurahi pamoja. Hapo tayari NDOA inakuwa ishafungwa hivyo. Kuna baadhi ya makabila, inabidi kwanza umtoroshe mwanamke aje kwako/kwenu, wataanza kumtafuta na kumkuta kwako/kwenu, wanamchukua. Kisha muoaji ataenda kumgomboa kwa kulipa fine na mahari. Hapo NDOA inakuwa ishafungwa hivyo.

Now back to your scenario.
Basically, TALAKA ndo benchmark kuwa NDOA husika sasa imevunjwa rasmi kisheria. Chombo pekee kinachoweza kuvunja ndoa ni MAHAKAMA. Na kabla ya kufungua shauri la talaka mahakamani, ni LAZIMA kwanza wanandoa hao wapitie kwenye Marriage Reconciliation Boards ambazo ni including Baraza la Serikali ya Mtaa, Baraza la Kanisa, na BAKWATA (kwa waislamu). Sheria ya Ndoa inaeleza kuwa wanandoa sharti wapitie kwanza kwenye mabaraza hayo kwa ajili ya ushuluhishi, ikishindikana kuwapatisha hapo ndo wanakuwa referred to Court for further legal procedures to disolve the Marriage. Na kama nilivyoeleza kwenye post iliyopita, NDOA ikishavunjwa rasmi na Mahama by issuing the divorce, IMPACT 3 hufuatia: KUGAWANA MALI ZA NDOA (mali mlizochuma pamoja wakati wa ndoa yenu); UANGALIZI WA WATOTO / CUSTODY OF CHILDREN (thus watoto wataishi kwa nani kati yenu); na MATUNZO YA WATOTO / MAINTENANCE OF CHILDREN (matunzo ya watoto). Under any factor (including kutelekeza, kutengana/separation, dhana ya kifo, n.k) to disolve the Marriage, ni lazima TALAKA itolewe ndipo NDOA husika inakuwa imevunjwa rasmi !

Kwa utaratibu wa Kidini, UKRISTO unatambua ndoa ya mke mmoja tu. As such, NDOA yoyote inayofungwa kabla ya kuivunja ile ndoa ya awali, ni BATILI (invalid). Isipokuwa kwa utaratibu wa dini ya kiislamu ambao unatambua ndoa ya mke zaidi ya mmoja.

Kwa ndoa ya mke mmoja under utaratibu wa kidini wa kikiristo, Sheria ya Ndoa imeeleza clearly kabisa kwamba a MAN or WOMAN who is married, shall not cotract another marriage while the former marriage still legally subsists. Kwa utaratibu wa kidini wa kiislamu, Sheria Ndoa ina-imply kwamba a WOMAN who is married, shall not cotract another marriage while the former marriage still legally subsists.

Kaka mleta uzi, kwahiyo kama hao watu walioana Serikalini bila kuivunja kwanza ile NDOA ya awali (former marriage), walikurupuka na hawakuwa smart. Hiyo ndoa yao (subsequent marriage) ya serikalini ni BATILI completely as we speak right now. Na kama ndoa ni BATILI, then all undertakings thereto are illegal ! They are not in valid marriage, rather they are committing adultery!!

Kama kweli hawakuwahi kuivunja ndoa ya awali mahakamani, hereunder are possible legal channels for you to go for:

(1) Wafungulie kesi ya ugoni (adultery). Hii huwa ni kesi ya madai (civil case) udai fidia. Na major evidence ya ugoni huu, ni
hao watoto waliozaa.
(2) Wafungulie kesi ya JINAI kuhusu hiyo illegal 'transfer of ownership' ya Hati ya Nyumba. Kwa vile the marriage is invalid, then there are some elements of criminality kwenye hiyo TRANSFER OF OWNERSHIP ya nyumba.

Wish you the best of luck in that regard. Pambana mkuu upate haki yako unayostahili, kuna jasho lako katika hiyo nyumba.
Ila pia waweza kusamehe na kuanza upya, kwa kuzingatia kwamba ULIIKIMBIA familia yako for 5 years !!!! LIFE must go On.

-Kaveli-
 
Duuh! Pole sana Mkuu! Nakutakia mafanikio katika kupigania haki ya wanao!
 
Duh kwahiyo rafiki yako anapumzika kwa mkeo kweli dunia uwanja wa fujo.
 
Hakuna aliemzuia madam, arudishe tu nyumba ya watoto then akaishi kwa mmewe, ampendae si anapaswa kuwa na makazi!! Anaendaje kukaa kwa mwanaume mwenzie

Jamani si naishi na watoto hapo nyumbani sasa ukisema arudishe nyumba ya watoto mi nakuwa sikupati kabisa...
 
Kosa lako kubwa lilikuwa katika kuchagua mke. Si kila mwenye jinsi ya kike anafaa kuwa mke Na mama. Hujachelewa pigania haki ya wanao tu.
 
Jamaa amemsitiri mkeo uliemtelekeza na watoto.

Ulitaka wawe machokoraa?

Tunamshukuru kwa kumsetiri mke wa rafiki yake ila angekuwa mstaarabu basi akamsetiri kwenye pango jingine sio hapo alipojenga mwanaume mwenzie!! Halafu huo ni wizi Wa mchana kabisa!!
 
Kosa lako kubwa ni pale ulipoamua kutoroka na kukata mawasiliano si wa mama yako, ndugu zako na hata na mkeo. Sasa ulitegemea mkeo afanye nini ili aweze kuishi yeye na na wanao. Ila kesi ya kudai nyumba yako unaweza kushinda na nakutakia kila la heri
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa, nchini Tanzania tuna aina (types) mbili za ndoa:
(a) Ndoa ya mke mmoja (Monogamous marriage)
(b) Ndoa ya wake wengi (Polygamous).

Hivyo, ni hiari ya partners kuamua na kukubaliana wao wenyewe waishi kwenye ndoa ya aina gani kati ya hizo hapo juu. So mnapofunga ndoa, mnapewa Cheti cha Ndoa. Cheti hicho, among other particulars, huonesha ni aina gani ya ndoa iliyofungwa na wahusika/wanandoa.

Kisha, kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa, kuna taratibu/namna 3 za kufungisha ndoa. Yaani taratibu au namna ya kuzifungisha hizo ndoa hapo juu (a) or (b). Taratibu hizo ni:

(i) Kidini. Utaratibu huu unawahusu wakristo, waislam, na wenye imani zingine za kidini.

(ii) Kiserikali. Utaratibu huu unatumiwa na mtu yeyote yule bila kujali imani za kidini, mfano wanandoa wana imani tofauti za kidini labda huyu ni muislam na mwenzake ni mkristo. Watu wengi wanaovamia waume/wake za watu hukimbilia kwenye utaratibu huu coz ni utaratibu ambao ni wa fasta na hauhitaji mashahidi wengi wala masharti mengi kama ilivyo kwenye utaratibu wa Kidini. Ndoa zinazofungwa kwa utaratibu huu wa kiserikali hufanyika katika offisi za Wilaya, na husimamiwa/huendeshwa na msajiri (Registrar) wa Wilaya. Katika utaratibu huu ni rahisi sana mtu kudanganya kuwa hajaoa/hajaolewa, maana ni watu wachache tu wa karibu na marafiki ndo wanahudhuria kama mashahidi, kwenye chumba/office, Registrar anakuja pale, mnaapishwa viapo, anawafungisha ndoa, watu wanapiga vigelegele, kisha mnaondoka zenu. Simply like that!!!!

(iii) Kimila. Utaratibu huu mara nyingi hufanyika kule vijijini. It varies from tribe/customs to tribe/customs. Hawaendi kanisani wala serikalini, bali ndoa inafungwa kwa mujibu wa misingi ya mila husika za wanandoa. Mfano kuna baadhi ya makabila, wazee wenye hakima/busara upande wa muoaji wanaenda nyumbani kwa mwanamke ili kujadili mahari, kisha inapangwa siku ya kuja kuchukua mahari (mara nyingi huwa ni mifugo kama ng'ombe, mbuzi, n.k). Then inapangwa siku wazazi wa pande zote mbili wanakutana kwenye ka-ceremony ka kunywa pombe na kufurahi pamoja. Hapo tayari NDOA inakuwa ishafungwa hivyo. Kuna baadhi ya makabila, inabidi kwanza umtoroshe mwanamke aje kwako/kwenu, wataanza kumtafuta na kumkuta kwako/kwenu, wanamchukua. Kisha muoaji ataenda kumgomboa kwa kulipa fine na mahari. Hapo NDOA inakuwa ishafungwa hivyo.

Now back to your scenario.
Basically, TALAKA ndo benchmark kuwa NDOA husika sasa imevunjwa rasmi kisheria. Chombo pekee kinachoweza kuvunja ndoa ni MAHAKAMA. Na kabla ya kufungua shauri la talaka mahakamani, ni LAZIMA kwanza wanandoa hao wapitie kwenye Marriage Reconciliation Boards ambazo ni including Baraza la Serikali ya Mtaa, Baraza la Kanisa, na BAKWATA (kwa waislamu). Sheria ya Ndoa inaeleza kuwa wanandoa sharti wapitie kwanza kwenye mabaraza hayo kwa ajili ya ushuluhishi, ikishindikana kuwapatisha hapo ndo wanakuwa referred to Court for further legal procedures to disolve the Marriage. Na kama nilivyoeleza kwenye post iliyopita, NDOA ikishavunjwa rasmi na Mahama by issuing the divorce, IMPACT 3 hufuatia: KUGAWANA MALI ZA NDOA (mali mlizochuma pamoja wakati wa ndoa yenu); UANGALIZI WA WATOTO / CUSTODY OF CHILDREN (thus watoto wataishi kwa nani kati yenu); na MATUNZO YA WATOTO / MAINTENANCE OF CHILDREN (matunzo ya watoto). Under any factor (including kutelekeza, kutengana/separation, dhana ya kifo, n.k) to disolve the Marriage, ni lazima TALAKA itolewe ndipo NDOA husika inakuwa imevunjwa rasmi !

Kwa utaratibu wa Kidini, UKRISTO unatambua ndoa ya mke mmoja tu. As such, NDOA yoyote inayofungwa kabla ya kuivunja ile ndoa ya awali, ni BATILI (invalid). Isipokuwa kwa utaratibu wa dini ya kiislamu ambao unatambua ndoa ya mke zaidi ya mmoja.

Kwa ndoa ya mke mmoja under utaratibu wa kidini wa kikiristo, Sheria ya Ndoa imeeleza clearly kabisa kwamba a MAN or WOMAN who is married, shall not cotract another marriage while the former marriage still legally subsists. Kwa utaratibu wa kidini wa kiislamu, Sheria Ndoa ina-imply kwamba a WOMAN who is married, shall not cotract another marriage while the former marriage still legally subsists.

Kaka mleta uzi, kwahiyo kama hao watu walioana Serikalini bila kuivunja kwanza ile NDOA ya awali (former marriage), walikurupuka na hawakuwa smart. Hiyo ndoa yao (subsequent marriage) ya serikalini ni BATILI completely as we speak right now. Na kama ndoa ni BATILI, then all undertakings thereto are illegal ! They are not in valid marriage, rather they are committing adultery!!

Kama kweli hawakuwahi kuivunja ndoa ya awali mahakamani, hereunder are possible legal channels for you to go for:

(1) Wafungulie kesi ya ugoni (adultery). Hii huwa ni kesi ya madai (civil case) udai fidia. Na major evidence ya ugoni huu, ni
hao watoto waliozaa.
(2) Wafungulie kesi ya JINAI kuhusu hiyo illegal 'transfer of ownership' ya Hati ya Nyumba. Kwa vile the marriage is invalid, then there are some elements of criminality kwenye hiyo TRANSFER OF OWNERSHIP ya nyumba.

Wish you the best of luck in that regard. Pambana mkuu upate haki yako unayostahili, kuna jasho lako katika hiyo nyumba.
Ila pia waweza kusamehe na kuanza upya, kwa kuzingatia kwamba ULIIKIMBIA familia yako for 5 years !!!! LIFE must go On.

-Kaveli-

Asante ndugu kaveli kwa maelezo ya kina

Hizo point za mwisho ulizojadili ndizo zimepelekea mm kufungua kesi, hiyo ni baada ya kufanya upelelezi Wa kina na kubaini hayo

Naendelea na hiyo kesi, naamini hoja nilizoieleza court zina mashiko na zitasikilizwa

Thanx
 
Back
Top Bottom