Nilimtelekeza mke wangu, nimerudi nimekuta rafiki yangu kamuoa

Haki yako hapo ni nyumba na hao watoto uliyozaa na huyo mkeo wa zamani.
 
Mke uliyekua umeoa hakua saizi yako, uzuri wa umbo lake tu ndo ulikuchanganya na kipato ulichokua nacho. Cha msingi wewe waache waendelee kula raha zao, wewe fight nyumba yako na mali zako zingine. Hangaikia watoto wako waende shule. Kiruka huyo huna haja ya kugombana naye.
 
Huyo Mke siyo kabisa,kashirikiana na hawara yake kishirikina wakupeperushe ili wafanye yao,DAWA zimeisha mume karudi,lianzishe uikomboe nyumba yako
 
Kama ulivyo pigana kupata pesa, pigana kupata mwana mwali mwingine kisha endelea na michakato yako, kama ni watoto waudumie wakiwa huko huko, na kama wanakupenda watakufata.

Haina haja ya wewe kupoteza muda mahakamani, mwisho wakuloge bure. Achana nao sahau yote komaa mbele kwa mbele, kwani mambo mazuri yapo mbele kwa mbele.
 
Hiyo avatar yako umetumwa na nani??

CC Kaizer ... shemeji anahujumu mwezi wa rozari
ahaahahahahahhahahhaha kwani mafungu ya rozari yanasema kuna kwadegesma?
hem acha mambo yako!
af nna libido ya kukuooooona,siku mingi sana chaaaa
 
Mkuu upo vizuri na shukrani coz nimejifunza mengi toka kwako. Nami na kaswali kidogo tu, je ikiwa ndoa imefungwa ukiwa na nyumba iliokamilika Kwa 80%, wanasemaga nyumba hua aiishagi na hiyo 20% ikakamilika mkiwa kwenye ndoa je incase of anything na kufanya mkataba wa ndoa kuvunjika hapo kwenye swala la nyumba mgawanyo unaendaje? Ahsante
 
Kwanza pole kwa yote uliyokutana nayo. Nilivyoona tu heading nikataka kukuweka kwenye kundi la watu ninaowaita wahuni na wapuuzi. Lakini baada ya kusoma mwanzo hadi mwisho nimebaini kuwa pamoja ns mambo hayo yote wewe huwezi kuongia kwenye kundi hilo la wahuni na wapuuzi.

Hata hivyo, kuhusu lawama nadhani unayo sehemu yako ya kuibeba. Kwanza kwa kutokuwa mwaminifu kazini na pili kwa kuendekeza matumizi yasiyo ya lazima na kushindwa kujiwekea akiba. Hiyo mke naye anasehemu yake ya lawama ambao anapaswa kuzibeba.
 
Mario katika ubora wake, unaishije kwenye nyumba ya mwanaume mwenzio!!!!!!!!!! pigania nyumba ya watoto wako na kesi utashinda, ila na wewe hukumuaga hata mama ako jamani miaka yote hiyo una roho ngumu baba
 
Mmhhhh ngumu kumesa atiiii....................anyway just forget and start afresh
 
Pigania nyumba yako urudishiwe ila.kama mlijenga kipindi mpo kwenye.ndoa ni.vizuri ikauzwa mkagawana na wewe ukatafuta.maisha engine.kama ulizaa naye chukua watoto wako ambao sio wako usichukue
 


Mkuu, kuhusu mgawanyo wa mali za ndoa baada ya Talaka (baada ya ndoa kuvunjwa kisheria), Sheria ya Ndoa (ya Tanzania) imeeleza pia kuhusu mali zilizopatikana kabla ya ndoa, lakini mali hizo zikaboreshwa wakati wa ndoa.

Hebu jisomee wewe mwenyewe kifungu cha 114 cha Sheria ya Ndoa, kuhusu mgawanyo wa mali za ndoa. Soma chote kifungu hiki :



Hapo mwisho kwenye kifungu kidogo cha (3), kimejibu swali lako vizuri kabisa.

MUHIMU:

Mali za ndoa ni sharti ziwe zimepatikana kwa 'juhudi za pamoja' (joint efforts). Kwa muktadha wa Sheria ya ndoa, JOINT EFFORTS ni nini?

Sheria ya Ndoa imekuwa ikifanyiwa marekebisho from time time ili kulinda haki za wanawake. "Joint efforts" kwenye mali za ndoa ina tafsiri kuu mbili:

1. Kuwa na direct contribution kwenye mali za ndoa. Yaani kuwa na mchango wa moja kwa moja. Mfano, kiwanja cha mwanamke afu mkashirikiana kujenga nyumba. Mfano, mke kaajiriwa na mume kaajiriwa wakashirikiana kutafuta mali. Mfano, mume kaajiriwa mke mfanya biashara, wakashirikiana kutafuta maendeleo.

2. Majukumu ya nyumbani anayotimiza mke. 'Domestic Duties'. Hii iliwekwa hivi ili kulinda haki za wale wanawake ambao ni house wives, yaani mke hajaajiriwa bali ni mama wa nyumbani. Zile domestic duties anazozifanya nyumbani, kama vile kumfulia mume, kumpikia, kumliwaza, kumshauri, usafi wa nyumba, n.k..., zinakuwa considered as a 'contribution' towards kupatikana kwa mali za ndoa. So hata kama mke alikuwa ni totally mama wa nyumbani, na wakachuma mali, basi kwenye mgawanyo wa mali za ndoa anakuwa considered.

Mkuu City hunter j, natumai umepata mwanga japo kiasi fulani.

-Kaveli-
 
ahaahahahahahhahahhaha kwani mafungu ya rozari yanasema kuna kwadegesma?
hem acha mambo yako!
af nna libido ya kukuooooona,siku mingi sana chaaaa
Tena ufanye haraka kabla hizi nywele hazijaisha mpk kisogoni. Huu upara naona Mungu ananitafutia utajiri. Na hivi mwanaye alisema tajiri ni ngumu kuingia kwenye ufalme wa babaye, naona kama loho mtakavitu ananitega ...(ni zambi kumwambia loho ashindwe na kulegea??)

Maskini zangu wajameni...
 
Dai chako mkuu,huyo dingi haoni soo kulelewa ndani ya nyumba?
 
Jamaa amemsitiri mkeo uliemtelekeza na watoto.

Ulitaka wawe machokoraa?
Amemstiri wapi wewe Karucee? Alichofanya ni UTAPELI TU, kwa nini abadili jina liwe lake, nyumba yake hiyo? Kiufupi huyo mwanamke HANA AKILI, unabadili jina la nyumba unaandika la mwanaume asiyehusika hata chembe? Inamaana siku wakikorofishana hiyo nyumba WATAGAWANA, ambapo angeandika jina lake hiyo nyumba ni yake!
 
Mimi sio mwanasheria lakini utoro katika ndoa zaidi ya miaka mitatu huwa hakuna ndoa. Lakini pia lazima isibitishwe na mahakama. Kwa vyovyote vile nyumba imemilikiwa kinyume na sheria.
 
haujakosea kabisa although kuna mitazamo mingi hapo nyumba irudi kwa watoto tu ndo muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…