Niliogopa nilipoanza kusikiliza wimbo mpya wa Roma 'Mimi ni Nani?

Niliogopa nilipoanza kusikiliza wimbo mpya wa Roma 'Mimi ni Nani?

yaani hapa nimejaribu kuirudia mara mbili tatu ili nimjue yeye ni nani ila nimeambulia patupu,,namkubali sana ROMA MKATOLIKI tangu anaanza MZIKI sijawahi kukosa kumsikiliza akipika ngoma mm napakua chap,leo nimekutana na FUMBO.
 
atakuw anazingumzia yeye ni chama🤣

mnaumiza akili Bure tu
 
Kwa maoni yangu Roma ni Natural Being
Kwa huu wimbo amezungumzia kwa upande wa uhai na kifo. Amejikita kwenye uhai na kifo. Kwamba hatma ya uhai ni kifo na kinaweza kuwa na mazingira tofauti lakini mapokeo yake ni ya aina moja. Na hutokea sio kama adhabu bali ni jambo asili linatokea kwa mazingira yoyote iwe mhusika achukue taahadhari au laah!! (Asili hujishughulisha na mambo jumla). Hivyo wanadamu tusijisahau sana. Ameamua kutumia wasanii, wanasiasa/Viongozi na matajiri kwa sababu ni watu maarufu na tunawafahamu na kwa sisi watu wa kawaida huwafikiria kama kifo(mambo asili) sio haki yao. Kwa wimbo huu nimejifunza mambo matatu ambayo sisi binadamu na viumbe wengine tunavimiliki.
1. Kuzaliwa/Kumea
2. Kuishi
3. Kufa.

NB:
All Organisms are Equal before the natural being.
 
Nilivousikiliza kwa Mara ya kwanza nilitaka kupata TAHARUKI,[emoji119]
Screenshot_20230616-142507.jpg
 
Back
Top Bottom