Nilionya kuhusu Katompa nikapuuzwa

Nilionya kuhusu Katompa nikapuuzwa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mabondia wengi wa Jeshini hawana uwezo ila wanabebwa tu , Kidunda hawezi kumpiga Katompa hata wakirudia game mara 10 .

Hii ndio maana Tanzania haifanyi lolote kwenye michuano ya Olympic au mashindano yoyote yale ambayo inapeleka mabondia wa jeshi.

Kila mwenye macho kaona mawe ya Katompa, hakuna cha Kidunda wala nini, ngumi ni Mazoezi na mbinu za kisasa, huwezi kuwa na nyumba ndogo 10 ukategemea ushindi , miguu itakosa nguvu na utapigwa mapema tu
 
Kidunda alikua captain wa Tanzania katika ngumi za ridhaa kwenye mashindano ya kimataifa, Amesha cheza Commonwealth games, Olimpic games sio bondia wa kubabaisha alikua mmoja wa mabondia tegeneo wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya ridhaa.

Mimi naona amechelewa kuingia ngumi za kulipwa. Ukiacha faulo ya kupiga kichwa aliyocheza katompa bado Kidunda alikua akiongoza kwa point.

Msimchukulie poa Kidunda.
 
Kwenye u captain wake ameleta medali ngapi?

angalia nafasi ya Kidunda kwenye viwango vya dunia , halafu muangalie Katompa , namba hazidanganyi
 
Lakini mbona kama ikionyeshwa vionjo vya kila raundi inaonyesha Kidunda alikua na point zaidi ya mcongo?....huyu mcongo aliguswa mara nyingi zaidi uso wake kabla ya ajali ya kugongana vichwa..nilivyoona mimi
 
Kwenye u captain wake ameleta medali ngapi ?
angalia nafasi ya Kidunda kwenye viwango vya dunia , halafu muangalie Katompa , namba hazidanganyi
Katika medali Sina hakika ni ngapi Ila ndiye bondia aliye wahi kuleta medali zaidi ya mara moja Ila sio dhahabu na ndiye bondia ambaye Kama taifa katika ngumi za ridhaa tulikua tukijvunia. Kidunda ameanza kucheza professional boxing juzi tu kwaiyo uwezi kukumkuta katika rank za juu Ila muda si mrefu atasogea.
 
Lakini mbona kama ikionyeshwa vionjo vya kila raundi inaonyesha Kidunda alikua na point zaidi ya mcongo?....huyu mcongo aliguswa mara nyingi zaidi uso wake kabla ya ajali ya kugongana vichwa..nilivyoona mimi
Hivi kwenye boxing wanaangalia uzito wa ngumi au kuguswa kwa mtu usoni?
 
Lakini mbona kama ikionyeshwa vionjo vya kila raundi inaonyesha Kidunda alikua na point zaidi ya mcongo?....huyu mcongo aliguswa mara nyingi zaidi uso wake kabla ya ajali ya kugongana vichwa..nilivyoona mimi
Nakuhakikishia kama game ingeendelea kidunda asingefika round ya 6
 
Angeangushwa wakati wowote
Mbona hajaangushwa sasa!!!..Katompa ni bondia mzuri tunajua hilo na yupo rank za juu (ingawa ranks sio uthibitisho sahihi wa ubora wa bondia maana kuna sababu nying sana za bondia kuwa juu katika ranks) lakini kwa kiasi chake kidunda jana alionekana kutawala mchezo jaribu kucheki hata highlights utaelewa namaanisha nini
 
Hii tabia ya Azam kurudia rudia mapambano yaliyopita siyo nzuri unaona sasa mtoa mada Anawaza pambano la Dullah Mbabe na Katompa badala ya mpambano wa Kidunda mtu mbaya!

Kifupi Kidunda alikuwa anatoa kichapo kizuri tu kwa Mkongo
 
Back
Top Bottom