Betting haizalishi chochote hivyo haiwezi kukupa utajiri yenyewe kama yenyewe. Utajiri upo katika kuwahudumia watu wengi zaidi. So siku nyingine ukipata huo 'mtaji' ndio uutumie sasa kujenga UTAJIRI.
Yaani utajiri halisi ni pale watu wengi wanapokutegemea kuikweli katika kuishi kwao.
Wafalme walikuwa matajiri - Sababu akili zao zilipelekea mafanikio ya watu wote kiulinzi na maisha
Mo na Bhakhresa ni matajiri jumla - Sababu wanalisha watu weeengi.
Utajiri sio kuwa na mihela mingi, kwa hiyo ndugu kama unataka kuendelea kuwa tajiri kweli siku nyingine ukipata pesa wekeza kwenye kuanzisha kitu chenye msaada wa kweli kwa maisha ya jamii nzima sio wewe binafsi tu kupata raha.
Furaha yako ipo kwenye furaha ya watu wako
Utajiri halisi ni ule ambao hata ikipigwa EMP hapa bado wewe unabakia tajiri. Namaanisha unamiliki asset halisi na unazalisha bidhaa halisi na kutoa huduma halisi. Mwenye ngombe wengi ana asset halisi, mwenye kazi/ujuzi ana asset halisi. Sio kuwa na pesa mingi benki tu.
Sasa reply zangu zinakuwa ndeeefu zaidi ya uzi tena😥😥. Tuishie hapa. Ngoja tumsikie na huyu mwamba alichokisema kuhusu ukuu and it will remain forever true;
............anayetaka kuwa mkubwa kati yenu, sharti awe mtumishi wenu. Anayetaka kuwa wa kwanza, sharti awe mtumishi wa wote. Maana Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, ila kutumikia, na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi - Jesus himself.