Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari!
Kila mtu anaweza kufanya backup ya habari ya saa 20:00 tarehe 31, Mei 2024. Ni habari nambari 2 kama sijakosea.
Nilisikia Makamu wa Rais anawaomba wafanyabishara wapunguze bei ya gesi ili wananchi wengi waweze kumudu.
Kipi kilinipa shock?
Bidhaa ya gesi ni miongoni mwa bidhaa ziko chini ya mamlaka za udhibiti, ina maana bidhaa hii haina bei kikomo (bei elekezi)?
2. Je, suala la Kodi zote za bidhaa hii ya gesi sio sababu ya wafanyabishara kuuza kwa bei hizi?
Makamu wa Rais anapaswa kumshawishi Rais apunguze kodi kwenye bidhaa ya gesi ili bidhaa ishuke bei na si kuwaomba wafanyabishara wapunguze bei.
Kama wafanyabishara wanauza kinyume cha vibali vyao serikali ichukue hatua za kuwakamata wapelekwe mahakamani au wafutiwe vibali au wapigwe faini. Hii ya kuomba wafanyabishara wapunguze bei ilipaswa kufanywa na diwani au mwenyekiti wa serikali ya mtaa.