Nilipoagiza mzigo AliExpress nikakumbana na rungu la kodi

Hivi upangaji wa kodi na usafirishaji kuna chart imewekwa kuonyesha au watu wanalopoka tu na kama kuna utaratibu unaweza kunionyesha napataje
Chart ipo kwa Bandari na waagiza mizigo mikubwa, ila kina sie wa Airport na Posta ni kuropoka tu pale pale, na wakikuona mzembe mzembe wanakupiga bei kubwa ili mkutane katikati ama watengeneze mazingira ya Rushwa.

Cha muhimu hakikisha una invoice ya Aliexpress ama amazon ama uliponunulia mzigo inaepusha usumbufu.


Chart ya Kodi sina labda mwenye nayo anaweza kuiweka hapa
 
Duuh mbona napata hofu sasa kusumbuana na hawa watu asee
 

Chief ee, nahitaji kuagiza kitu from ali express, je! Utanifikiaje huo mzigo? Napatikana huku mkoani, je utanifikiaje? Asante mzee baba
 
Chief ee, nahitaji kuagiza kitu from ali express, je! Utanifikiaje huo mzigo? Napatikana huku mkoani, je utanifikiaje? Asante mzee baba
Kikawaida unakufikia kwa posta, kuna posta ya karibu hapo unapoishi? Pia ipo hii kampuni mpya ya speedaf japo sijajua kama wana matawi mikoa yote.
 
Ni Act au Regulation gani ya kodi inasema hivo.

Kama hutojali naomba u-cite hicho kifungu hata kama ni Income Tax Act (ITA-2004)au Revision zingine
Mkuu nenda ofisi ya TRA ilio karibu na wewe utapata maelezo vizuri kama ni mfanya biashara
 
Uliwaonesha invoince toka Aliexpress ama uliwaachia tu wakague na kutoa bei yao? Sijawahi kulipishwa zaidi ya 18%
Mkuu naomba msaada kujua ni kampuni gani naweza kuagiza electronics appliances kama air cooler, laptop nk na nipokee kwa haraka mpaka mkoani nilipo
 
Mkuu naomba msaada kujua ni kampuni gani naweza kuagiza electronics appliances kama air cooler, laptop nk na nipokee kwa haraka mpaka mkoani nilipo
Issue si kupokea haraka, issue ni Gharama. Kampuni kama Fedex, Dhl, etc zinaweza chukua hadi siku 3 mzigo kufika ila gharama ya kusafirisha laptop inaweza kuwa hadi laki 4. Ndio maana huoni watu wakitumia huo usafiri wa Haraka.

Pia uzito wa kitu unaongeza gharama pia, jinsi kitu kinavyokua kizito ndio jinsi gharama inavyoongezeka, mara nyingi vitu vizito watu wanatumia usafiri wa Meli ambao inafika mwezi.
 
Ok ahsante,
Ni kampuni gani ni rafiki kwa maelekezo hayo?
 
Hio Ni xiaomi?

Natamani agiza huko em nipe uzoefu inakuaje simu global maana yake Nini
Kuna xiaomi niliipenda na bei Ni nzuri

 
Product yyt toka nje yenye nembo ya R mana zipo tracked for VAT...hakikisha product zako hazina hio kitu. ..better nunua freeshipping ingawa kwa mzigo mkubwa inakua changamoto but hakikisha unaongea na agent km nizakodi sure la. .hii nikote..ebay alibaba or aliexpress
 
Mkuu asante kwa huu mchongo
 
kama unataka kununua bidhaa alibaba kwa jumla huna agent nitafute inbox nikupe agent wanaosafirisha mizgo ofisi zao zote zipo hapo k/koo

Na ukitaka ushauri zaidi karibu inbox
Tuwekee hapa,si anafanya biashara halali kabisa why pm tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…