Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hongera kwa kuwa na moyo wa kutaka kupunguza uzito. Unene na uzito uliopita kiasi sio mzuri.Nimeanza kuongezeka nilikuwa na mwili wangu mzuri,miaka enda rudi nina kg zangu 60 ajabu nikaona nguo zinanibana, mmmmh mara nazipeleka kwa fundi kuziongeza mmh juzi napima nina kg 70 hapana
Watu wako busy kunisifia nimenenepa naona kerooo.
Mazoezi nayo nafanya ila sio kiviiiile.nafanya kupitia tv Dstv 198 jmosi asubuhi Big brother naija wanafanya mazoezi sana nafanya nao ila sioni mabadiliko.
Huu ndo mlo wangu nibadilishe wapi?
1.Kila siku nakunywa lita moja na nusu ya maziwa fresh( hii ni lazima) mimi sinywi pombe lazima every day nipate maziwa.
2: asubuhi nakunywa maziwa na mkate
3: saa nne asubuhi sahani ya matunda saa 9 wali au chips mazingira ya kazini hivi ndo vyakula vinavyopatikana ( siku moja moja na mchana sili kabisa)
4. Jion sili chakula, nakula maziwa na mkate au tambi au kabichi.
5: j2 tu ndo nakula ugali samaki na mboga.mboga.
Hii diet imekaaje wajuzi wa kutengeneza mwili?
Dah asante sana nashukuru, ila ni kazi kweli kweli, yaan najikuta sina muda wa kufanya haya yote.ofisini natoka saa 2.5 usiku nafika home saa 3 usiku nimechoka mbaya muda wa mazoezi nautoa wapi?Hongera kwa kuwa na moyo wa kutaka kupunguza uzito. Unene na uzito uliopita kiasi sio mzuri.
Mimi sio daktari, au dietitian, lakini nimekuwa mtu wa mazoezi kwa miaka mingi, na nimekuwa kwenye upunguzaji na udhibiti uzito kwa miaka minne sasa. So, nitaeleza kutokana na uzoefu wangu.
Kanuni ya kupunguza uzito inafanana na mfumo wa hesabu zako za benki. Ukitaka kupunguza kiwango cha fedha kwenye akaunti yako, kuna njia mbili. Moja ni kuacha kabisa kuweka, unakua unatoa tu. Pili, kutoa kiwango kikubwa zaidi ya unachokiweka. Lakini kwenye mwili wa mwanadamu, njia ya pili ndio inatumika.
Kwenye mwili wa mwanadamu ili uzito upungue, unahitaji uhakikishe kiwango cha Calories (nishati inayotumika kuuwezesha kufanya shughuli mbalimbali) unachokiingiza mwilini (kupitia vyakula) ni lazima kiwe kidogo kuliko kile kinachopotezwa (kupitia shughuli mbalimbali).
Sasa ili ufanikishe kupunguza uzito. Ni lazima ufanye haya.
1. Hakikisha unakula vyakula kidogo vyenye wanga, vyakula vya kusindikaa, na vinywaji vya kusindikwa kwani vina kiwango kikubwa cha calories, ambazo ndio zinaupa mwili uzito zaidi.
Tazama picha hizi.View attachment 1882754View attachment 1882755View attachment 1882756
Mfano, ukinywa soda ya Mls 350, unaupa mwili 140 Cal. Ili uziunguze hizi, inahitaji mfano utembee kwa muda wa nusu saa (sababu ukitembea Nusu saa mwendo wa utaenda wastani wa Km 2.4 na kawaida utaunguza Cal 135). Hivyo usipofanya shughuli yoyote, utaongeza hizo 140 Cal kwenye mwili wako.
2. Kula vyakula ambavyo vinasaidia kupunguza uzito.
Mfano, tumia zaidi nyama nyeupe; kula sana mboga za majani, achana na sukari kama unaweza na tumia asali nayo kwa kiwango kinachoshauriwa, maziwa yanatakiwa ¾ litre kwa siku. Kula sana mboga za majani, ambazo hazipikwa na mafuta kila siku.
3. MAJI, MAJI, MAJI. Maji ya kunywa ni muhimu sana. Walau lita 3 kwa siku katika interval. Ukiamka asubuhi saa 11 kabla hujasafisha kinywa, kunywa maji yasiwe ya baridi, walau glass 3, ukiweka na limao moja ni nzuri zaidi. Kaa nusu saa ndio safisha kinywa. Usinywe maji ndani ya nusu saa kabla au baada ya kula, unaathiri mmeng'enyo wa chakula, kwa kudilute kemikali zinazosaga chakula. Usinywe maji masaa mawili kabla ya kulala, utaathiri usingizi.
4. Mazoezi na kazi.
Fanya mazoezi maalumu na yenye kiwango sahihi. Unatakiwa uzingatie kanuni za muda wa mazoezi, muda wa kupumzika ndani ya wiki, ili kuupa muda mwili wa kurecover misuli ili kuhifadhi kile ulichopata kwenye mazoezi. Mfano, kama unafanya mazoezi makali, yapaswa kila baada ya masaa kumi ya mazoezi makali, basi uupe mwili masaa 48 hadi 72 ya kupumzika. Kama ni ya wastani, ni masaa 48, ila kama ni ya kawaida masaa 24 yanatosha kupumzika. Pia mazoezi inabidi uhakikishe unafanya mazoezi sasa kwa ratiba sahihi. I can recommend; YouTube kuna Channel inaitwa Body Project, na Roberta's Gym. Naamini zitakufaa. Ila sharti la mazoezi ni Consistent. Without consistent you can't Gain.
Pia, kama shughuli zako ni za misuli, basi inabidi uzingatie aina na kiwango cha chakula. Kama ni za kutumia akili, vyakula kama mikate, chapati (wanga) punguza kabisa.
5. Mfumo wa maisha.
Hapa ndipo ilipo changamoto kubwa zaidi. Unaweza ukafanya vyote lakini, usipungue uzito au usione matokeo.
[emoji95]Usingizi. Muda wa kutosha wa mwili kupumzika ni muhimu sana kwenye upungzaji uzito na afya ya akili kwa ujumla. Usipolala muda wa kutosha, itaathiri ufanyaji kazi au mazoezi. Hivyo lala masaa 7 hadi tisa kwa siku. Mimi binafsi, weekedays zote ninalala saa 4 na kuamka saa 11. Kasoro ijumaa na jumamosi, sababu siku zinazofuatia sifanya mazoezi. Na jumapili siku nzima ni ya kuupa mwili total rest.
Epuka kabisa kulala mchana na hasa baada ya kula. Kulala mchana kunaathiri protein ambazo zinadhibiti sukari ya mwili na mapigo ya moyo.
[emoji95] Hakikisha umekula masaa yasiyopungua mawili kabla ya kulala.
[emoji95] Tembea. Wakati hulazimiki kutumia usafiri tembea. Kutembea ni adventure nzuri sana, sababu unajiunganisha mwili na mazingira huku ukuupa mwili faida. Walking is the man's best medicine.
View attachment 1882844
[emoji95]Nunua baiskeli. Ukijizoesha kutumia baiskeli, itakufaa kwenye kuuweka mwili katika hali nzuri.
Kwa ufupi, Siri kubwa ya mwili kupunguza uzito na kuwa na afya njema, ni kuwa kuushughulisha mwili, kulala muda wa kutosha, kutokulala lala hovyo mchana, maji ya kutosha, epuka vyakula vya sukari, wanga au vya makopo.
Kuna kitabu hiki, kizuri sana juu ya jinsi ya kuishi kwa kuzingatia afya.
View attachment 1882845
Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
Asante.leo sukari naacha tatizo nina vidonda vya tumbo, nisipokula naumia. Yaani vidonda vyangu dawa yake ni kula.Maziwa hayana shida kabisa maziwa sababu ni protein. Kinachofanya uongezeke ni vyakula unavyokula pamoja na maziwa..haswa hio wanga ,mafuta kwenye chips na sukari vipunguze hivyo.
😍😍😍 nice one,Ndio unampenda mtu kwa traits zake ama nafsi yake tu. If you fall inlove with someones heart and soul yeye kuwa bonge au mwembamba havihusiani!
Not bad. Ni kweli mazingira ya kazi yanaathiri mfumo wa maisha ikiwemo mazoezi. Jaribu kutengeneza muda, hasa asubuhi upate japo dakika 10 tu za kufanya mazoezi, uwe na consistency.. Ingia YouTube then search 10 Minutes Full body workout. Zipo nyingi, ila nashauri tumia hii;Dah asante sana nashukuru, ila ni kazi kweli kweli, yaan najikuta sina muda wa kufanya haya yote.ofisini natoka saa 2.5 usiku nafika home saa 3 usiku nimechoka mbaya muda wa mazoezi nautoa wapi?
Nikifika home napika maziwa tu huku nacheke big brother au movie nusu saa nyingi nishasinzia.[emoji23][emoji23][emoji23]
Sema nashukuru kwenye vyakula nitajitahidi.mazingira ya kazini ni mabaya nikishindaga home sili ovyo.
Mimi sio mnene nina mwili wa kawaida ila naona naongezeka na kakitaambi kwambalii nakaona sijui haka nikaondoe vip tumbo langu sio flat kama zamani.
Nataka nirudishe tumbo langu la zamani sehemu zingine nibaki hivi hivi
Afu nilisikia mazoezi yanakomaza miguu akuh yasije niharibia guu langu.
Ntakuwa nafanya mazoezi kidogo ya kuzuia kitambia afu nakula vyakula
ulivyoniambia, hapo vipi?
Leo naacha sukari maana maziwa ninayotumia naweka sukari, najifunza kutumia asali kuanzia leo.
Maji kiasi gani unatumia kwa siku?Asante.leo sukari naacha tatizo nina vidonda vya tumbo, nisipokula naumia. Yaani vidonda vyangu dawa yake ni kula.
Nikiwa job naweza sema leo ninakula natunda tu, nikikojoa tu mara mbili tumbo hilo njaa,hapo lazima nile tho nakula kidogo. Tangu mwaka jana mwezi wa 11 niliacha kupika wali kwangu ,kwakuwa niko mwenyewe. ila kazini nalazimika kuula[emoji17]
Kama leo nimekula ka pilau kadogo na samaki mkavu. Ndo sili tena, usiku ni maziwa na matunda. Kesho nashida home ndo ntaweza andaa mboga mboga.
Asante kwa ushauri.
Pili achana na hizi white processed stuff zote zinazotokana na ngano kama chapati, mikate, maandazi, tambi etcUmesema haunywi pombe, that's good achana na fizzy drinks pia.
Pili achana na hizi white processed stuff zote zinazotokana na ngano kama chapati, mikate, maandazi, tambi etc
Ukiweza piga starch au carbs ambazo ni natural kama mihogo, magimbi, viazi vitamu na upunguze mastarch ya mawali na maugali.
Mboga za majani na matunda kwa wingi, protein kishkaji coz we ni mwanamke na hauhitaji kujenga muscles.
Ukishindwa mazoezi kabisa jitahidi kuruka kamba au evening walk kwa ajili ya kukaza mwili.
Nipe Namba yake ya simu ili nikupunguzie mzigo,hiyo kazi niachie mimi.Napenda sana slim girls ( English figure), nilipokutana nae alikua mwembamba sasa ananenepa, sipendi mwanamke mwenye mahips hips na mwili sana, i like models but inaonekana ana asili ya mwili. Nashindwa kuelewa, leaving someone for this reason seems to be ridiculous
Ni ujinga tu huwa unawasumbua.Huwa nawashangaa sana jamaa wa sampuli yako!
Kuna Mmoja hivyo hivyo akaoa kaslim.. kalivyozaa tu akawa Bonge jamaa masononeko mengi..
Love doesn't ask Why!
Kwa hiyo na wewe una vinyama nyama??.[emoji23][emoji23]
Ahsante Mungu wengine tumeshahakikishiwa zinapendwa 'nyama nyama' lasivyo, jizoooozi..!
Ukitaka kumuacha kwa Sababu ya ubonge nijulishe ili nikusaidie[emoji23][emoji23]Kumbe slims girls ni ugonjwa wa wengi, mi nimemwambia wife akithubutu kuwa kibonge ajue imekula kwake.
Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Kama huwezi kabisa, wanasema brown bread ni nzuri. Ila ni vyema kuachana navyo. Jambo nililojifunza, miili yetu ili tuwe na afya, haitaki ipewe luxury ya kupitiliza na pili haitaki vile vyakula ambavyo tunavichukulia kuwa ni 'vizuri', ila inataka vile ambavyo tunavyoviona 'vya hadhi ya chini', haitaki vile 'vitamu vitamu'[emoji3]Pili achana na hizi white processed stuff zote zinazotokana na ngano kama chapati, mikate, maandazi, tambi etc
Nitajitahidi maana nahisi natumia sana mkate almost kila usiku nakula vipande viwili vya mkate na vikombe viwil vya maziwa.
Asantee sana.
Dada asikudanganye mtu hakuna anayeweza kumpenda mtu bila Sababu.Hata wewe mwenyewe mtu unayempenda hujampenda tu, kuna Sababu iliyofanya umpende.Ukipenda mtu bila sababu haya yote hayawezi kuwa shida
Mwambie aanze diet na mazoezi
Well said. Kuruka kamba ni zoezi zuri sana. Na interesting thing ni kuwa unaweza fanyia hata chumbani. Na huhitaji kuwa na kamba yenye (kama huwezi ipata). Unaweza ruka tu vile unatumia kamba. Mazoezi ni starehe nzuri sana.Umesema haunywi pombe, that's good achana na fizzy drinks pia.
Pili achana na hizi white processed stuff zote zinazotokana na ngano kama chapati, mikate, maandazi, tambi etc
Ukiweza piga starch au carbs ambazo ni natural kama mihogo, magimbi, viazi vitamu na upunguze mastarch ya mawali na maugali.
Mboga za majani na matunda kwa wingi, protein kishkaji coz we ni mwanamke na hauhitaji kujenga muscles.
Ukishindwa mazoezi kabisa jitahidi kuruka kamba au evening walk kwa ajili ya kukaza mwili.
Niliyenae nampenda bila sababu...hakuna mtu aliyenidanganyaDada asikudanganye mtu hakuna anayeweza kumpenda mtu bila Sababu.Hata wewe mwenyewe mtu unayempenda hujampenda tu, kuna Sababu iliyofanya umpende.
Nikiamka saa 11 nakunywa nakunywa vikombe viwili uvugu vugu,,saa moja asubuhi wakati natoka nakunywa tena, kazini nina bili kilimanjaro moja kila siku mpaka natoka nakuwa nishaimaliza. Nikifika home nakunywa tena tho sipimi, na saa tano muda wa kulala nasikiaga kiu sana lazima jinywe tena.
Sio mbaya.Nikiamka saa 11 nakunywa nakunywa vikombe viwili uvugu vugu,,saa moja asubuhi wakati natoka nakunywa tena, kazini nina bili kilimanjaro moja kila siku mpaka natoka nakuwa nishaimaliza. Nikifika home nakunywa tena tho sipimi, na saa tano muda wa kulala nasikiaga kiu sana lazima jinywe tena.
Kwa ufupi siwezi jua natumia kiasi gani, ila hiyo 1.5l kazini ni lazima
Nadhamu muda wetu ndo hautoshi ila kuanzia kesho lazima kula vitu ulivyoniambia.yaani nataka hiki kitumbo kinachokuja kipotee sehemu nyingine niko sawa. AsanteKama huwezi kabisa, wanasema brown bread ni nzuri. Ila ni vyema kuachana navyo. Jambo nililojifunza, miili yetu ili tuwe na afya, haitaki ipewe luxury ya kupitiliza na pili haitaki vile vyakula ambavyo tunavichukulia kuwa ni 'vizuri', ila inataka vile ambavyo tunavyoviona 'vya hadhi ya chini', haitaki vile 'vitamu vitamu'[emoji3]
Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app