Castle_Lite
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 4,646
- 10,442
Daah! Watu mna nguvu nyingi mme-take for granted 🙄
Sina tena . Labda itarud nikiamua kwa dhati na kupunguza mambo ya kidunia.
Daah! Watu mna nguvu nyingi mme-take for granted 🙄
Hapo ndipo nguvu zako zilipolala, usingestrugle ikiwa ungezitumia ki usahihi....just wishing n booomSina tena . Labda itarud nikiamua kwa dhati na kupunguza mambo ya kidunia.
Umetokea kwenye familia ya kichifu?Hii ni story yangu na nitatoa na mifano ya vitu nilivyowahi kufanya. Watu wengi hawakujua, lakini kuna matukio kadhaa yaliyotokea nikiwa mtoto ambayo hayakuwa ya kawaida kabisa. Haikuwa mara moja ilikuwa vitu ambavyo vilitokea mbele ya watu wengine pia.
Mfano wa kwanza ulikuwa mvua.
Kuna siku anga lilikuwa wazi kabisa. Hakukuwa na dalili ya mvua hata kidogo. Nilisimama nje nikaangalia juu halafu nikasema tu mvua inyeshe. Baada ya muda mfupi, mawingu yakaanza kukusanyika polepole, upepo ukabadilika, halafu mvua ikanesa. Watu walishangaa lakini hawakujua nini kilitokea dakika chache kabla.
Mfano wa pili ulitokea nyumbani.
Kuna siku taa ya chumbani ilikuwa imeharibika kabisa, haikuwaka hata kidogo. Watu walijaribu kuigusa mara kadhaa bila mafanikio. Nilishika tu swichi nikasema iwake, na ghafla taa ikawaka kama kawaida.
Watu walikaa kimya kwa muda.
Mfano wa tatu ulitokea nilipokuwa nje nacheza.
Kulikuwa na kitu kidogo nilichokuwa nacho mkononi kama sarafu. Niliitupa juu halafu kwa sekunde chache ilikaa hewani bila kuanguka mara moja. Ilikuwa kama imesimama kidogo hewani kabla haijarudi chini. Watu wawili waliokuwa karibu waliona hilo.
Walishangaa sana.
Mfano wa nne ndio uliwashangaza zaidi watu wazima.
Kulikuwa na glasi iliyoanguka na kuvunjika vipande vipande. Nilivikusanya vile vipande nikaviweka pamoja, nikavishika kwa mikono yangu kwa sekunde chache… halafu vile vipande vilikaa pamoja tena kama havikuvunjika kabisa.
Watu waliokuwa pale hawakuongea kwa muda.
Na mfano wa tano ndio ulionifanya nijue uwezo huo ulikuwa wa kweli.
Nikikia na uwezo wa kufungua madirisha au milango kwa kuiangalia tu kwa macho na kuifikiria ikiwa inafunguka au kufunga nayo inafanya hivyohivyo kama nilivyoifikiria akilini.
Baada ya hapo, mambo hayo yalianza kupungua polepole kadri nilivyokuwa nakua.
Mpaka sasa ni nadra naona kama yamepotea.
Lakini ukweli ni kuwa…
nilipokua mdogo miujiza ilikuwa inatokea mbele yangu, na wakati mwingine mikononi mwangu kabisa.
Kakukosea nini huyu jamaa boss
Haya mambo kila mmoja anaweza kutafsiri kivyake kutokana na misingi yake ya kiimani au mtazamo wake na experience yake, wapo wenye kuamini kwamba kila binaadamu huwa na spirit guide wake ndio hutupa hizo taarifa kupitia hisia, ndoto na njia zengine.Hivi hizo hisia ndo roho mtakatifu
Mazoezi ni yapiHaya mambo kila mmoja anaweza kutafsiri kivyake kutokana na misingi yake ya kiimani au mtazamo wake na experience yake, wapo wenye kuamini kwamba kila binaadamu huwa na spirit guide wake ndio hutupa hizo taarifa kupitia hisia, ndoto na njia zengine.
Muhimu ni kwamba hiyo ni intuition na hivyo kila mtu anakuwa nayo ila hutofautiana uwezo wake na aina zake, ndio maana wenzetu huwa wanafanya mazoezi ya kuimprove intuition.
Dogo naona ulishiba chai na magimbi ukaanza kukumbuka ndoto zako za utotonisijui ni nini natafuta njia ya kurudisha ili niweze tena
Na wewe yako ni ipi,weka hapa maana at least nacheka kuondoa stressHaya mambo kila mmoja anaweza kutafsiri kivyake kutokana na misingi yake ya kiimani au mtazamo wake na experience yake, wapo wenye kuamini kwamba kila binaadamu huwa na spirit guide wake ndio hutupa hizo taarifa kupitia hisia, ndoto na njia zengine.
Muhimu ni kwamba hiyo ni intuition na hivyo kila mtu anakuwa nayo ila hutofautiana uwezo wake na aina zake, ndio maana wenzetu huwa wanafanya mazoezi ya kuimprove intuition.
Nimesoma kichwa cha uzi nikaanza kucheka, hadi sasa sijasoma uzi na sisomi 🤣🤣
Ni kweli mkuu, nina tatizo kubwa la kiimani na limeanza nikiwa na miaka 13 kwahiyo mimi hizi bado naendelea kuona ni chai-tea.Unaogopa nini 😂😂😂 soma.
Hii ni kama wale wanaoamini Mungu , Uganga au Uchawi na wasioamini.
Kama haijawah kukutokea hauwez kuamini.
Utu uzima una mambo mengi, pesa zenyewe kwa asilimia kubwa tunazipata kwa njia za utatanishi.Kwa hiyo umeukataa u-clean n pure?
Exactly.Mambo ya kushangaza huwa yanawatokea wengi nikiwemo,lakini hakuna unaloweza kuilezea jamii ikakuelewa ama kuamini,best way ni kukaa kimya tu
Mara nyingi huwa ni husda ndo inaua hiyo nguvu… wachawi wana nguvu ya kuona kitu ndani yako bila wewe mwenyewe kujua, sipingi unayoyasema wala anayoyasema mleta mada. Ni ukweli kabisa! Ndo maana ya ule msemo kwamba kila mtoto huzaliwa na nguvu au karama yake.Nazingatia hapo kwenye "Clean and Pure".
chai ya rangi , mim Nakuamini except mfano wako wa nne .(mgumu sana😎😎😎)
Mm pia nilikuwa nina kanguvu fulan.
Mfano nilikuwa naweza kuota ndoto na zikatokea kweli,. Watu wa karibu kabla ya kufa nilikuwa naona wiki 2 au 3 kabla. Awe anaumwa au kufa gafla au ajali. Nikiota na nikimwambia Mama alikuwa anaanza kulia. Na wiki za mbele msiba unatokea kweli.
Nadhan Misiba inaweza fika 10+ kidogo niliyoiona.
pia Hiyo ya Mvua nilikuwa naweza. Na wingu likitanda nikinuia jua liwake linawaka kali ndan ya sekunde chache tu.
Kufungua milango nilikuwa naweza pia.
Kunuia kitu na kikatokea nilikuwa naweza pia.
nakumbuka form 4 niligombana na washkaj kadhaa (walikuwa wananionea bwenini na kunichezea rafu uwanjan) na nikanuia wapate zero na wote walipata. Watu kama 5 hiv 😎😎😎😎.
Na mengne meng nilinuia na yakatokea.
Na hapa sio kwamba ni dini au uchawi. Hapana. Nasema tu "Mungu naomba hivi na hivi" then unatulia na ukikumbuka unaomba tena, na baadae kinatokea.
Too Bad nimepoteza hiyo Nguvu kwa miaka Mingi sasa.
So nakuamin Bro. Hivyo vitu viko.
Ukijua utachanganyikiwa ndugu, we ishi tu 😁Niote nitakufa lini🤣
tatizo la kiimani naweza kukusaidia kama unataka. lakini jua kitu kimoja cha msingi ambacho kinakubalika kiimani na kisayansi kwamba asilimia kubwa ya vitu vilivyopo havionekani kwa macho, havisikiki, havishikikiNi kweli mkuu, nina tatizo kubwa la kiimani na limeanza nikiwa na miaka 13 kwahiyo mimi hizi bado naendelea kuona ni chai-tea.