Nilipokuwa mdogo niliona viongozi wakifurahi katika shughuli za kitaifa, kumbe wanafurahia posho sio uzalendo

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Aisee nilikuwa sipo sahihi, nilidhani viongozi wanapenda nchi yao Hadi nikawa inspired, toka nipo msingi shule tunaitwa na walimu tushiriki shughuli za viongozi, mama anawaandalia mihogo asubuhi nyumbani muende uwanjani kushiriki.

Nilichogundua kumbe wakubwa wanalipwa posho kubwa sana kushiriki hizi event ambazo wengine tulitoka jasho jukwaani, wengine njaa.

Nimekuja kugundua kumbe Kuna upper class wanaocheza na Kodi Kama posho na sisi wengine tunatumika kuonesha kwamba wakubwa wanakubalika Ili waendelee kutunyonya.

Hakuna mzalendo nchii hii mzalendo ni posho, hata Mdee amekuwa msaliti kwa sababu ya posho.

Watanzania ni Masikini sana, ni Masikini hakuna mfano. Ni shimo tulimo ndani , sio ccm Wala chadema wakututoa huku ni KIFO tu.

Asanteni wanajamvini
 
Mkuu upo sahihi.Njaa mbaya sana.Wanasema haina baunsa.
 
Ila bado upo mdogo kifikra na kiakili.

Nilichogundua kwako vijana wavivu na wasiopenda kujishughulisha Wana lawama Sana. Unakuta mtu anasema wakubwa hawatakiwi kupata posho kubwa kwa Sababu kazi zinafanywa na chini yao lakini wanasahau kubwa hao wakubwa wa Sasa walikuwa wadogo wa zamani na walikuwa wanalipwa kidogo na wanacholipwa Sasa ni matokeo ya juhudi zao kufika walipo.

Kijana anamaliza chuo anabahatika kupata ajira na hapohapo anatamani kulipwa sawa na yule aliyemkuta miaka 20 kazini bila kuonesha juhudi. jamani vijana tubadilike msione vyaelea vimeundwa
 
Point tupu pumnzika umeumiza kichwa kuandika viwafaavyo vijana
 
Huo ndio ukweli. Pambana na wewe uingie kwenye upper class
 
Kuna kijana mmoja aliyekuwa amemaliza University, siku moja alitoa malalamiko kwa baba yake, na baba yake akampa ufafanuzi ambao mpaka leo hii(ni mkuu fulani katika shirika fulani) anawaheshimu sana wastaafu.

Pale nyumbani palikuwa na punda mzee, lakini baba yake alimpenda sana huyo punda.

Malalamiko ya kijana: "Baba, sasa huyu punda ana faida gani, hivi sasa hafanyi kazi yoyote, kutwa kalala. Unamhangaikia wee, kumkatia nyasi, kumpa maji, kumwogesha, naona usumbufu mtupu! Si bora umpige risasi afe! Ni kifo kisicho na maumivu!

Baba kwa mtoto: " Mwanangu, unakumbuka tulikotoka?(baba alikuwa mkulima na mfanya biashara ya kuuza mpunga)?

Mtoto: "Ndiyo baba"
Baba: Ni nani alikuwa anabeba magunia ya mpunga toka shamba mpaka hapa nyumbani?
Mtoto: "Ni huyo punda baba!
Baba: " Ni nani alikuwa anabeba magunia ya mpunga toka nyumbani mpaka sokoni?
Mtoto: Ni huyo punda baba!
Baba: "Umesomeshwa na hela iliyotoka wapi?
Mtoto: Kutokana na mauzo ya mpunga baba!
Baba: Aliyeubeba nani?
Mtoto: Ni huyo punda baba!"
Baba: (kwa sauti kubwa) "Kwa hiyo fadhila zako kwa punda leo ni kumpiga risasi afe? Kweli?, kweli?, kweli? (baba akatoa leso akajifuta machozi, akaingia ndani)
Mtoto: (akakaa chini ardhini akimuangalia punda kwa huzuni na shukrani kubwa, akaanza kulia).
 
Kwa hiyo huyo Punda akamwezesha kupata kazi ya ukuu fulani kwenye hiyo kampuni fulani?
 
Back
Top Bottom