Nilipoona tu Jana Filimbi ya Mpira kuanza na Mpira Kupigwa Nje Makusudi nilijua Rivers United FC wameshakufa

Nilipoona tu Jana Filimbi ya Mpira kuanza na Mpira Kupigwa Nje Makusudi nilijua Rivers United FC wameshakufa

Kwa wale tu mliocheza Mpira ngazi za Ligi za chini, kati na hata Kubwa na mliokuwa / mlioko Ligi Kuu sasa mtakubaliana nami kuwa aina hii ya Uchawi umetumika na unatumika mno Mipirani.

Kitu pekee tu ninachokijua katika aina hii ya Uchawi ni kwamba Ukitumika Timu iliyoutumia kwa 100% hushinda hiyo Mechi.

Na hata Mechi ya Simba SC ya Jumamosi kuna Uchawi mwingine Ulitumika wakati Timu zikisalimiana na aliyekuwa Kinara katika Kuutekeleza ni Mchezaji Mmoja Muhimu wa Kiungo ambaye Namhifadhi.

Uchawi upo na Unafanyika mno.
Popoma
 
Nyinyi mbona kabla ya kucheza na Raja pale kwa Mkapa dereva wa basi lenu alirudi kinyumenyume na bado mkapasuka au ilikuwa mbinu ya kupunguza magoli ? Na vipi kule South Africa mwaka Jana dhidi mlivyowasha Moto uwanjani na bado mkapasuka au mhanga wenu aliwaambia mpunguze magoli kwa kuwasha moto uwanjani ? Dunduka NI dunduka Tu
 
Ifike mahali tukubali ubora wa Yanga. Uchawi hauchezi mpira!

Timu ya Congo wakati huo ikiitwa Zaire iliingia World cup na wachawi 100 na ikapigwa za uso!

Tunasubiri ijumaa Simba watakandwa week (7-0) na Wydad na hasira za kukosa kombe hata moja msimu huu zitawaangukia Mo, makocha, Onyango na Rage aliewaita wanasimba wote ni mbumbumbu! Mashabiki wa mikia fc mtasema wote waondoke!

Huko Yanga kwasasa ni furaha tu ya kucheza nusu fainali Shirikisho na kubeba NBC league cup!

Ijumaa inshallah sio mbali!
 
Back
Top Bottom