Nilipoteza Kazi kipindi ambacho niliihitaji kuliko nyakati yoyote

Nilipoteza Kazi kipindi ambacho niliihitaji kuliko nyakati yoyote

Take that risk mzee kwea pipa ma agent wapo kazi zipo ni wewe tu utayari wako. Mtumikie kafiri uishi vyema. Miaak 28 na una familia na ujatoboa bila kufanya maamuzi magumu ya haraka mzee unapoteana
Chief Nakuelewa Vyema Na Ushauri Wako Ni Babkubwa, Uzuri Ni Kuwa MI Ni Muumini Wa Kusafiri Na Nimeshafanya Attempts Kadhaa , Sina Sababu Hata Ya Kutafuta Agent 2022 Niliwahi Kufanya Kazi Na Agency Moja Hapa Dar Ya Kusaidia Watu Kusepa So At Least Nipo Na Uelewa Mkubwa Sana Juu Ya Opportunities Zipatikanazo Nje Ya Nchi Na Sijachoka Kujaribu🙏🏻🙏🏻Nimeshaaply Tourist Visa Ya USA 2 Times Nikaangukia Pua Though Nitajaribu Tena This Year Kwa CANADA na New Zeland Nashukuru Sana Kaka
 
Shukrani Sana Mkuu🙏🏻
Jiunge humu uangalie namna ya kujitetea
 
Kama upo Dar kazi za sales and marketing nyingi sana, kama vipi nenda pale makumbusho mwanga Tower, ghorofa ya 17 Kuna Kampuni ya kusambaza dawa za mbu hua wanatafuta watu wa masoko, peleka CV yako huwezi jua lolote likawa poa, pia usiache kufuatilia job sites, LinkedIn, na sehemu mbalimbali utaiona Nuru mkuu soon, nakuombea Mungu akufanyie wepesi.
Asants Sana Kaka, Nitalifanyia Kazi Hili🙏🏻
 
Mimi NI Kijana, Umri Miaka 28 Mkazi Wa Dar Es Salaam!

Wakuu Mtoto Wa Kiume Akikiri Hadharani Kuwa Mambo Ni Magumu Ujue Kweli Ni Magumu, Na Hii Ikiwa Ni Mara Yangu Ya Kwanza Kuandika Chapisho Langu Humu Jamiiforums Licha Ya Kuwa Member Kwa KipindI Kirefu Kidogo

Nilipoteza Ajira Yangu November 2024 Baada Ya Kampuni Niliyokuwa Nikifanyia Kazi Kufilisika , Nyakati Ambazo Mke Wangu Alikua Amekaribia Kujifungua Na Kodi Ya Nyumba Ilikua Ipo Nyakati Za Mwisho, Kiukweli Nilichanganyikiwa Ila Namshkuru Sana Mungu Mke Wangu Alijifungua Salama Na Mtoto Ana Miezi Mitano Sasa Pia Kodi Niliungaunga Na Nikalipa, Akiba Niliyokua Nayo Nilifungua Biashara Ya Gaming Plus Shisha Lounge Ambayo Ndani Ya Miezi Mitatu Ilikufa Baada Ya Kuibiwa Kila Kitu Kwenye ile Ofisi Yangu, Hapo Ndo Kizaazaa Kilipoanza Maana Ilifika Kipindi HadI Diapers Za Mtoto Nikawa Nahama Maduka Tu Kukopa

Kinachonisibu Hivi Sasa Ni Namna Ya Kuendesha Hii Familia Nzuri Isiyo Na Hatia Yoyote Na Inayostahili Malezi Bora Ya Baba Na Mume Kwani Wamenivumiia Kwa Kipindi Kirefu Sana Maisha Yakiwa Magumu Mno🙏🏻🙏🏻

Nduzu Zangu Kwa Yeyote Atayesikia Nafasi Yoyote Ya Kazi Tafadhali Mnikumbuke Ndugu Yenu

Nina Shahada Ya Kwanza Ya Uhusiano Wa Umma Na Masoko Kutoka Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Augustino, Mwanza Main Campus

Mungu Awabariki Sana🙏🏻
Muombe Mungu akukutanishe na watu sahihi
 
Badili mbinu kotokana na elimu yako ni ya makaratasi, fanyia kazi elimu ya akili, kuna kazi za ujenzi, kuchimba mtaro, kuondoka mjini kurudi kijijini pia gharama za maisha ya hapo nyumbani upunguze n.k
 
Ushauri Mzuri Sana Ndugu Yangu Idonyee🙏🏻
 
Chochote ukipatacho ikumbuke familia kwanza Mambo yatakaa sawa tuu endelea kupambana
 
Mwambie wife aende kwao, ili ujipange vizuri, tafuta hata boda ya mkataba , ingia mtaani
 
Kaka ushauri mzuri, changamoto ni kuwa wife wangu hakulelewa na wazazi bali na bibi ambae nae kwa sasa umri umeshaenda sana na amechukuliwa na watoto wake wanamlea so kiukweli wife hana pa kwenda ingawa ni mpambanaji mnooo nae alipoteza kazi baada ya kupata ujauzito ila kabla ya hapo wote tulikua tunaleta mkate nyumbani na maisha yalikuwa comfortable sana ,things has changed very fast hadi kuna muda siamini🙏🏻
Nenda Kawe boss wangu kwa Mwamposa utaniambia utakayoyakuta,ni ushauli wangu tu,au sikiliza Rise and shine kupitia TV au redio
 
Mwambie wife aende kwao, ili ujipange vizuri, tafuta hata boda ya mkataba , ingia mtaani
Kaka ushauri mzuri, changamoto ni kuwa wife wangu hakulelewa na wazazi bali na bibi ambae nae kwa saaa umeri umeshaenda sana na amechukuliwa na watoto wake wanamlea so kiukweli wife hana pa kwenda ingawa ni mpambanaji mnooo nae alipoteza kazi baada ya kupata ujauzito ila kabla ya hapo wote tulikua tunaleta mkate nyumbani na maisha yalikuwa comfortable sana ,things has changed very fast hadi kuna muda siamini🙏🏻
 
Kipindi cha amani ndicho kipindi cha kujiandaa na vita. Kwa sasa nadhan uko vitani you hapo inachtakiwa familia ile kwanza. Kuna option nyingine huwez kuzichukua mna familia iko nyuma yako. Skill za mitaa kama uwinga unazo?
 
Back
Top Bottom