Nilipoteza Tsh. Milioni 2 kwa kuchanganya Afrikana na Afrika Sana

Nilipoteza Tsh. Milioni 2 kwa kuchanganya Afrikana na Afrika Sana

Ali Nassor Px

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2022
Posts
2,384
Reaction score
3,926
Aya mambo mengine jamani yasikieni tu na kila siku tujitahidi kufanya ibada/ Maombi kwa sababu kuna muda tunapitia changamoto. ila sasa muda wengine tunapitia changamoto mfululizo yani haijamaliza changamoto hii inakuja nyingine.

Sasa naomba moja kwa moja kwenya mada.

Kutokana na tukio hili la kupoteza million 2 nilijifunza kama Dar es Salaam sio Mkuranga, ukitembea tembea ukiwa upo sawa kabisa kiakili.

Siku hiyo jobless nipo home nimelala mara ghafla Baba ananigongea mlango kuwa niamke kuna sehemu anataka kunituma kwa vile yule ni mzee wangu mimi ni nani mpaka nimpinge sasa.

Jobless nikaamka akanipa maelekezo kuwa nichukue pesa alinipa kama million 2 na nusu hivi kwenye bahasha ya kaki pia akanipa namba za simu za rafiki yake.

Akanipa maelekezo kuwa yeye anawasiliana na jamaa tutakutana sehemu nimpe hizo pesa milion 2 ni za ada ya chuo ya mdogo wangu wa mwisho na laki 5 ni za jamaa wana biashara zao wenyewe na Baba.

Huyo jamaa alikuwa anapewa hizo pesa kwa sababu hizo pesa zilitakiwa zikalipwe Bank na bank yenyewe ni PBZ BANK na huyo bank ipo Zanzibar na yeye ndo alikuwa anaenda huko Zanzibar.

Alitakiwa akazilipie huko kwa sababu hata mdogo wangu yeye ali apply chuo Zanzibar huko baada ya kukosa vyuo Dar.

Sasa bhana Mwamba wakati napewa maelezo nilikuwa nipo fresh tu. Nilikuwa namsiliza mzee kwa umakini mkubwa sana. Baada ya maelezo nikachukua kibag changu nikazitia zile pesa mzee akanipiga na mbuku 10 wa nauli tu, (baba yangu mara nyingi hanipi pesa ila kama akanituma mara nyingi unipa pesa kubwa ile inayobaki ndo inakuwa yangu yani sirudishi chenji).

Nikawahi stand fasta chukua gari ya ubungo. sasa wakati nipo kwenye gari nashangaa message ya mama mtu ananiambia kuwa ajisikii sawa. mwezi wa pili ajaona siku zake.

Yani hapo ndo alinivuruga na nilikasirika kwa sababu siku tunafanya yetu kweli sikutumia ndomu ila baada ya ile game nilimpa pesa nikamwambia kanunue dawa. ujilinde kinamna fulani kwa sababu kama akipata mimba na mimi nina safari ya kwenda jeshi na jeshi miaka 3 mtoto atapata tabu ya huduma na yeye atapata tabu pia maana wa kumsaidia majukumu pia atakuwa hayupo maana mzee wangu namjua wenyewe.

Sasa wakati nachat nae nikamuuliza yani inakuwaje kuwaje ajaona siku zake mwezi wa pili sasa na wakati siku zile nilimpa pesa akanunue dawa.

akanijibu kuwa yeye hakumeza dawa kwa sababu dawa zinamualibiaga mzunguko wake hataki hata kuziona .

Daaah yani pale nilikuwa nipo ndani ya gari ila kama yule demu ningekuwa ndani ya gari ningempiga migumi ya roho alafu ningemtupa nje ya gari MAE ZAKE!

Katika chat chat si bando nalo likakata bhana na nikitazama umbali bado mrefu balaa na mda uo gari nazo haziendi (Foleni) na jamaa nae ananipigia simu umefika wapi dogo, yani hapo kichwani nilikuwa nina mawazo ya watu wawili.

likanijia wazo kama vipi nishuke kwenye gari nichukue boda au bajaji fasta inawaishe kwa jamaa lakini pia likanijia wazo nishuka ninunue vocha.

Nikashuka kwenye gari nikachukua vocha kama ya buku mbili hivi nikachukua na nikajiunga fresh kwanza nikampigia jamaa nikamwambia kuna foleni kwahiyo nimeshuka kwenye gari hapa nina mpango wa kuchukua usafiri wengine ili niwai.

iNkampigia sasa mama mtu wangu nikaomba anipe maelezo ya kunyooka nikaona anajing'ata ng'ata tu ndugu zangu siwadanganyi nilimtukana vibaya sana na nikamtoa akili sana yule demu maana niliona kama ananizingua hivi maana anajua hali halisi kama nimebakisha siku kadhaa tu hazizidi 10 nasepa Depo.

Mwamba nikakata simu fasta nikadandia bajaji kwenye bajaji nikakuta dereva bajaji kabeba abiria mmoja nikaona sio kesi nikaongea na wenye bajaji. nikamwambia anipeleke Africasana badala ya a
Africana.

jamaa mwanzo tulibishana kwa sababu alikuwa anaona safari ndefu ila dakika ya mwisho sasa akakubali fresh tu.

Kuzama ndani ya bajaji me nilikuwa busy na simu yangu tu mda uo nina mihasira balaa.

yule demu ananichanganya akili tu sijui hajui yeye afanyaje. sasa nikawa namuuliza haujui ufanyaje kivipi kwani wewe sikukupa pesa dawa au sasa nini kilikuchanganya mpaka ukala pesa baada ya kununua dawa ?

Wanangu ile nafika Africa sana nikashuka wenye bajaji akasepa mda uo kumbuka nipo bize na simu naongea na demu wangu anapiga simu analia mara analeta mambo

"Oooh basi nitajiua."

"Mara oooh mtoto nitalea wenyewe usiwe na wasiwasi maana haumtaki huyu kiumbe."

Yani ile akili ya kuwa nimepewa pesa ikinitoka kabisa nikawa namshughulikia mwanamke tu. mara ghafla nashangaa jamaa ananipigia simu Ooooh dogo upo wapi mbona mda unaenda sana nikampanga nishafika mbona ila ndo nilitaka kukupigia ila umeniwahi hapa.

Akaniuliza upo sehemu gani sasa nikampanga aaah me nipo hapa africana mbele yangu naona Bar kubwa hapa.

Jamaa akaniuliza kwa mshangao sana Bar kubwa wewe upo wapi kwani nikamwambia nipo hapa Africana kuna Bar na nikamtajia jina ya ile Bar jamaa akanipanga dogo ushapotea na hapo ulipo upo Africa sana na sio Africana.

Sasa kama kaakili nacho kakanirudia kichwani kutazama lile bag nilibeba pesa nalo sina yani siku ile niliona kama ndoto hivi inaendelea nikapata wazo nitakuwa nimeliacha kwenye bajaji ila sasa bajaji nampata wapi na jamaa wa bajaji wenyewe nimekutana nae njiani tu.

Siku huyo siwezi kuisahau kabisa kwa sababu nilikuwa nawaza nampataje bajaji au naenda kumuueleza nini mzee kuwa eti nimepoteza million 2 tena kwenye bajaji na sio daladala.

Ok, mzee ndo kanielewa kuwa pesa imepotea siku ya siku paah demu analeta mimba home yani mzee atanifikiria vipi nimempotezea pesa dogo alafu haijatosha nimemtia mimba mtoto wa mtu.

Nilipangawa vibaya sana nikaona solution cha kwanza nikazima simu nikatia mfukoni alafu safari sasa ni kurudi nyumbani ila nikaona nyumbani nako sio sehemu ya kwenda acha kwanza niende kwa baba mdogo nikaenda kwa baba mdogo nikamuelezea mchezo mzima .

Daah alisikitika sana maana hapo sijamlostisha mzee tu pia nishamuharibia mpaka mdogo wangu.

Baba mdogo akaniambia mimi nitabaki kwake mpaka siku ambayo nitasepa jeshi ila yeye ataenda kuongea na mzee baba mdogo akaenda kuongea na mzee sijui waliongea nini ila siku kadhaa mbili nikasikia dogo kashasepa chuo Zanzibar, na mimi ile ishu ya jeshi ikazingua sikwenda jeshi.

Siku nikipata muda nitawasimulia mkasa wa Mimba uliishia vipi ila kesi ilifika kwa mzee.
 
Shule zifunguliwe mapema.
Ameeeeen
1671115678813.jpg
 
Back
Top Bottom