Nilishaeleza kwanini hatupaswi kuona ni kosa kwa Tanzania kukopa fedha za miradi kutoka nje, kwa kuwa tusipokopa athari zake ni hizi hapa

Sawa nimekuelewa point yako ni kua hutaki watu waikosoe serikali kwa kuvuna mikopo kila uchao! Ila bado nina swali vp hii mikopo tunayokopa je haina madhara kabisa hapo baadae ikiwa haitatumika kwa uwekezaji unaotakiwa?
Mkuu, mbona unauliza maswali mepesi sana katika thread nzito sana? Mikopo tunayokopa itaachaje kuwa na madhara ikiwa haitatumika kwa uwekezaji unaotakiwa? Hilo ni swali la kuuliza kweli ikiwa nilishasema tunahitaji mikopo kwa ajili ya capital (development) expenditure, na kuonyesha kwamba hata kutumia mikopo kwenye recurrent expenditure ni kosa?
 
Kama huoni 'contradiction' ya signature hiyo na uliyoandika kumhusu unayemsifia hapa, basi wewe utakuwa ni mmoja wa hao wenye akili ndogo sana.
Sio sioni contradiction, wewe huelewi filosofia katika signature yangu, kwa hiyo tatizo liko kwako - uwezo mdogo wa elimu na kuelewa philosophical statements
 
Mkuu, mbona unauliza maswali mepesi sana katika thread nzito sana? Mikopo tunayokopa itaachaje kuwa na madhara ikiwa haitatumika kwa uwekezaji unaotakiwa? Hilo ni swali la kuuliza kweli ikiwa nilishasema tunahitaji mikopo kwa ajili ya capital (development) expenditure, na kuonyesha kwamba hata kutumia mikopo kwenye recurrent expenditure ni kosa?
Sasa kumbe watu tunaikosoa serikali kukopa hovyo wakati hawawezi kusimamia hio mikopo itumike vema kwaajili ya maendeleo na sio ufisadi! Hivo basi hakuna haja ya kutupigia izo kelele zenu za kukopa wakati hatuna matumaini yoyote kwa io mikopo kuleta tija! YAANI HAINA HAJA YA KUKOPA KWA AJILI YA WATU WACHACHE KUJINEEMESHA!! Asante kwa mada nzuri.
 
Hapana Mkuu, hatukopi ili kulipa madeni. Tunakopa kwa ajili ya capital au development expenditure ili kujiongezea uwezo wa national revenue ili tuwe na uwezo zaidi wa kuongeza pato la taifa na in turn kuongeza uwezo wa kulipa madeni ya nyuma kutokana na increased national revenue
Ndio maana nakwambia hii elimu ya public finance Kwa watz ipo chini Sana, nenda mtandaoni kaangalie budget ya nchi miaka 5 nyuma kuanzia budget hii ya 22/23 angalia data ya total loans internal+external then angalia total debts paid internal+external ndo utakuja uelewe kumbe kimantiki we get fresh loan to pay old debts.
 
Sasa kumbe watu tunaikosoa serikali kukopa hovyo wakati hawawezi kusimamia hio mikopo itumike vema kwaajili ya maendeleo na sio ufisadi! Hivo basi hakuna haja ya kutupigia izo kelele zenu za kukopa wakati hatuna matumaini yoyote kwa io mikopo kuleta tija! YAANI HAINA HAJA YA KUKOPA KWA AJILI YA WATU WACHACHE KUJINEEMESHA!! Asante kwa mada nzuri.
Kama mnaikosoa serikali katika kukopa wakati tatizo ni matumizi mabaya ya mikopo basi hamna akili sawasawa. Kwa nini msiikemee serikali kwenye matumizi mabaya ya mikopo, ambalo ndio tatizo?

Ni sawa na kusema namlaumu baba kununua gari la familia kwa sababu mama na kaka yetu mkubwa huwa mara nyingine wanaendesha gari wakiwa wamelewa na kuligonga
 
Ndio maana nakwambia hii elimu ya public finance Kwa watz ipo chini Sana, nenda mtandaoni kaangalie budget ya nchi miaka 5 nyuma kuanzia budget hii ya 22/23 angalia data ya total loans internal+external then angalia total debts paid internal+external ndo utakuja uelewe kumbe kimantiki we get fresh loan to pay old debts.
Mkuu King Nkondo, una uzalendo ila huzielewi siasa za Tanzania. Vitu unavyovisema tatizo lake sio mikopo, bali utawala wa nchi ambao hauna kitu tunaita check and balance. Yaani hata mambo ya hovyo yakiletwa bungeni au yakipendekezwa na watendaji kama mawaziri yatapita tu, bora liende
 
Kama mnaikosoa serikali katika kukopa wakati tatizo ni matumizi mabaya ya mikopo basi hamna akili sawasawa. Kwa nini msiikemee serikali kwenye matumizi mabaya ya mikopo, ambalo ndio tatizo?

Ni sawa na kusema namlaumu baba kununua gari la familia kwa sababu mama na kaka yetu mkubwa huwa mara nyingine wanaendesha gari wakiwa wamelewa na kuligonga
Tunaikosoa kukopa sababu mkuu wa nchi alishabariki upigaji 'kuleni kwa urefu wa kamba', kwaio wasipokopa watatucha watanzania tukiwa na deni dogo na dhiki zetu! Ama watajiongeza wapunguze kula fedha za umma kwa kiwango ambacho walau tunaweza ona tija katika miradi inayoanzishwa kutokana na mikopo hio.
 
Basi mkosoeni Raisi Samia kwa kuwa very permissive kwa watu kufanya ufisadi. Na mbona nilishasema hapo juu, kuwa nakiri kwamba Samia hajawa mkali hata kidogo kwenye kukemea na kuchukua hatua dhidi ya ufisadi ambao unakua kwa kasi sana siku hadi siku
 
Ndio tunamkosoa kwa style hii. Yaani kama vile Ukitaka kuondoa mti, unaanza kuukata shina halafu baadae unaondoa kisiki na mizizi!! Hatua kwa hatua mzee!
 
Mkuu, naungana nawe kwamba ikiwa Samia ataruhusu hali ambapo tunakopa halafu fedha tulizokopa zinafanyiwa ufisadi, basi hata mie nitakuwa wa kwamza kuokota jiwe ili nimpige. Lakini kukopa na ufisadi ni mambo mawili tofauti. Lawama nyingi zimeelekezwa kwa Samia kwenye suala la kukopa. Kina Ndugai hawakusema nchi itapigwa mnada kwa sababu ya ufisadi wa fedha za mikopo bali kwa sababu ya kukopa.

Na ni kweli Samia hajawa makini sana kwenye kudhibiti ufisadi unaoendelea kukua kila siku tangu kifo cha Magufuli. Pamoja na ubaya wote na matumizi ya hovyo ya Magufuli kwenye fedha za serikali, aliweza kuweka hofu ya kufanya ufisadi nchini, ambapo chini ya Samia hofu hiyo inatoweka taratibu.

Samia anahitaji kuwa mkali kwenye ufisadi, watu wamemsoma na kuona hana ukali katika sehemu hii. Sijawahi kumsikia Samia anakemea ufisadi kwa nguvu zote au kuchukua hatua na kutangaza hadharani kuwawajibisha watu kwa sababu ya ufisadi. Sijui kama anaogopa au na yeye yuko compromised, yaani kaambiwa ukitumwagia ugali wetu tutamwaga mboga
Angekuwa smart basi angeeza na kuufumua mfumo mzima wa uongozi na kusuka upya. Baada ya hapo ndiyo angeanza kukopa. Ndoo kama inavuja kitu cha kwanza ni kuuziba kabla ya kuweka maji. Ufisadi siyo kukemea tu ila tunatakiwa kubadili mfumo ASAP. Hata huyo Magufuli pamoja na kujifanya kuwa mkali kwenye uzembe na ufisadi lakini hakuweza kubadili chochote ndiyo maana leo umefufuka kwa nguvu kubwa. Tutengeneze mfumo kabla ya chochote.
 
Sielewe hoja yako nini, kwa kuzingatia uliyoyaandika hapo ambayo unadai magufuli aliyafanya nahisi ndio njia nzuri ya kuilinda hiyo mikopo ikafanya KAZI ilivyokusudiwa...

Sasa we unataka tukope hapo hapo watu waende Safari zisizo na tija ulaya, unataka tukope hapo hapo unataka watu walipwe for nothing...hiyo mikopo unachukua kwa ajili ya kutumia Kula Raha Tu badala ya kujenga nchi!?

Mikopo mingi aliyoichukua magufuli ilikuwa ya kibiashara, unakopa kwa riba kubwa kama wanavyodai wachumi..laini pia kwa upande wa pili tija yake iliylonekanika kwa haraka na kwa.muda mfupi...

Na kingine...sijui huu ujinga watz tutautoa vipi kwenye akili zetu..tunataka maendeleo lakini hatutaki kuyatesekea hayo maendeleo...unavyoona ulaya na marekani ziko vile ni kwamba mababu zao miaka 100 iloyopita walipotia aina ya uchumi huu wa kujenga ambao bwana magufuli alikuwa akiutkelekeza hapa tz...

Huwezi kutenga bajet ukasema robo Tatu ya bajeti ni kulipana mishahara na posho alafu iliyobaki ndio unaingiza kwenye miradi ya maendeleo kama wafanyavyo huko bungeni..

Ni lazima unapotaka maendeleo lazima ujifunge mkanda kweli kweli lasivyo watz na waafrika tutaishia kukimbilia ulaya na marekani ambapo wao wako kwenye stage ingine kabisa ya maendeleo ambayo Sisi tunaitaka kwa Kuota ndotni na sio kufanya KAZI.

Binafsi sioni hoja na mantiki katika nondoo zako hapo juu , hivi mfano ukiweza kucontro mfumuko WA bei , kuna haja Gani ya kupandisha mishahara kwa danganya toto ya tsh 10000!?

Umeongelea vitambulisho vya wamachinga, ndugu ule ni ubunifu ambao ukileta tija kilichokosewa ni kuutengenezea mfumo Tu, lakini ilikuwa njia nzuri ya kuwa na chanzo kingine cha Kodi za halmashauri zetu...

Kiukweli andiko lako nalipa 2/10
 
Mkuu, ukikopa kwa ajili ya capital expenditure sio rahisi kuona fedha mitaani, ila ukikopa kwa ajili ya recurrent expenditure, jambo ambalo sio zuri, utaiona fedha mitaani, lakini baadae utapata maumivu sana.

Kukopa kwa ajili ya recurrent expenditure kunaleta athari kubwa ya inflation, na unaweza kujikuta inafikia unanunua fungu la nyanya kwa elfu kumi.
Nadhani hatujaelewana, shida inakuja kwamba ili tukope ina maana pesa za ndani zifanye mzunguko ili wananchi maisha yao yaboleke na waweze kulipa Kodi na hiyo pesa ikalejeshe hiyo mikopo
Sasa kilichop ni kwamba hizo pesa za ndani hazionekani na watu hali zao zinakua mbaya na wanashindwa kulipa hata Kodi, sasa hapo unategemea hiyo ni akili?
Watu wanakonda na hawawezi kula Milo mitatu bado serikari inaona raha kukopa ili hali walipa Kodi wanakonda?

Nimekuelewa. Lakini sasa kwa tatizo unaloeleza, unafikiri suluhisho ni kutokopa?
 
Sielewe hoja yako nini, kwa kuzingatia uliyoyaandika hapo ambayo unadai magufuli aliyafanya nahisi ndio njia nzuri ya kuilinda hiyo mikopo ikafanya KAZI ilivyokusudiwa...

Sasa we unataka tukope hapo hapo watu waende Safari zisizo na tija ulaya, unataka tukope hapo hapo unataka watu walipwe for nothing...hiyo mikopo unachukua kwa ajili ya kutumia Kula Raha Tu badala ya kujenga nchi!?

Mikopo mingi aliyoichukua magufuli ilikuwa ya kibiashara, unakopa kwa riba kubwa kama wanavyodai wachumi..laini pia kwa upande wa pili tija yake iliylonekanika kwa haraka na kwa.muda mfupi...

Na kingine...sijui huu ujinga watz tutautoa vipi kwenye akili zetu..tunataka maendeleo lakini hatutaki kuyatesekea hayo maendeleo...unavyoona ulaya na marekani ziko vile ni kwamba mababu zao miaka 100 iloyopita walipotia aina ya uchumi huu wa kujenga ambao bwana magufuli alikuwa akiutkelekeza hapa tz...

Huwezi kutenga bajet ukasema robo Tatu ya bajeti ni kulipana mishahara na posho alafu iliyobaki ndio unaingiza kwenye miradi ya maendeleo kama wafanyavyo huko bungeni..

Ni lazima unapotaka maendeleo lazima ujifunge mkanda kweli kweli lasivyo watz na waafrika tutaishia kukimbilia ulaya na marekani ambapo wao wako kwenye stage ingine kabisa ya maendeleo ambayo Sisi tunaitaka kwa Kuota ndotni na sio kufanya KAZI.

Binafsi sioni hoja na mantiki katika nondoo zako hapo juu , hivi mfano ukiweza kucontro mfumuko WA bei , kuna haja Gani ya kupandisha mishahara kwa danganya toto ya tsh 10000!?

Umeongelea vitambulisho vya wamachinga, ndugu ule ni ubunifu ambao ukileta tija kilichokosewa ni kuutengenezea mfumo Tu, lakini ilikuwa njia nzuri ya kuwa na chanzo kingine cha Kodi za halmashauri zetu...

Kiukweli andiko lako nalipa 2/10
Naona wewe ndio huelewi haya mambo, na kwa uliyosema hata kujaribu kukuelimisha itakuwa ni kupoteza muda wangu. Unahitaji shule ya muda mrefu sana
 
Angekuwa smart basi angeeza na kuufumua mfumo mzima wa uongozi na kusuka upya. Baada ya hapo ndiyo angeanza kukopa. Ndoo kama inavuja kitu cha kwanza ni kuuziba kabla ya kuweka maji. Ufisadi siyo kukemea tu ila tunatakiwa kubadili mfumo ASAP. Hata huyo Magufuli pamoja na kujifanya kuwa mkali kwenye uzembe na ufisadi lakini hakuweza kubadili chochote ndiyo maana leo umefufuka kwa nguvu kubwa. Tutengeneze mfumo kabla ya chochote.
Ufisadi sio lazima tatizo liwe mfumo - ni tabia (culture) ya watu.

Leo tukisema tuwe kama China, ukifisadi fedha za umma unahukumiwa kifo, na tukanyonga watu wawili watatu, unafikri kuna mtu atadiriki kufanya ufisadi? Nyerere yeye alichapa viboko 24, na watu waliogopa, na hata waliapa "Rushwa kwangu mwiko, sitatoa wala kupokea rushwa" na alifanikiwa.

Ethiopia hawakubadili mfumo enzi za Zanawi. Zanawi alimfunga jela miaka mitano tu ambaye alikuwa deputy wake wakati wa vita, akasema ikiwa nimefunga jela rafiki yangu kipenzi kwa ajili ya rushwa, sasa jaribu wewe mtu baki. Ufisadi ukafa. Nenda kwa Kagame Rwanda ufanye ufisadi uone utakavyokiona cha mtema kuni.

Kwa hiyo inahitaji kuwa na sheria kali tu, kwa kuwa kwa mtu mweusi ufisadi uko kwenye damu, ni adhabu tu ndio itamwogopesha sio mfumo
 
Watanzania wengi hawaelewi kwamba suala la kutekeleza miradi mikubwa nchini kwa kutumia fedha yetu ya ndani sio suala la kujivunia wala kujisifia hata kidogo. limetuletea maumivu makali katika karibu kila sehemu ya uchumi, hasa wakati wa Magufuli.

Miradi ya Magufuli aliyojivunia kutumia fedha za ndani ni kutia ndani ununuzi ndege, Reli ya SGR, Umeme wa Stiegler, daraja la baharini, Uwanja wa Chato, kuhamia Dodoma, nk.

Tanzania ni nchi masikini, sasa jiulize ikiwa fedha za miradi mikubwa kama hii sehemu yake kubwa ni fedha za ndani, fedha hizo zitatoka wapi? Katika nchi zote ambazo hazina vyanzo vikubwa vya fedha kama mafuta, miradi mikubwa kama hii hutekelezwa kwa fedha za mikopo ya nje na ndani.

Ili kupata fedha za ndani kwa wingi, Magufuli alifanya yafuatayo hapa chini, hatua ambazo zilituumiza sana. Ni kweli kuna mambo yanayotuumiza Samia ameyarithi toka kwa Magufuli, lakini si kwa kiwango kile cha wakati wa Magufuli.
  1. Wananchi na biashara zao kubanwa kodi kwa kila namna, kiasi kwamba hata biashara nyingine kufa kutokana na mzigo wa kodi
  2. Kutafuta vyanzo visivyo rasmi vya fedha kama vitambulisho vya wamamchinga ili kuongeza pato la serikali
  3. Kuanzisha kodi ya miamala ya simu kama Mpesa na vifurushi
  4. Kuanzisha kodi za kuchukua fedha ATM za benki
  5. Kutoa agizo kwa polisi kwamba wafanye kila namna kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa njia ya faini za barabarani
  6. Kubana nyongeza za mishahara ya wafanyakazi serikalini na maruurupu mengine ya wafanya kazi ili fedha ziende kwenye kutekeleza miradi mikubwa
  7. Kuondoa sherehe za kitaifa hata za matukio muhimu katika historia ya nchi
  8. Kupunguza kwa kiasi kikubwa bajeti za maendeleo ya serikali za mitaa - hii ni kutia ndani bajeti za miradi midogo midogo katika miji na majiji kiasi kwamba kunakuwa na athari mbaya ya mzunguko wa fedha na kila mtu anaanza kulia hali mbaya
  9. Kubana mikopo ya elimu ya juu ya wanafunzi, kwa mfano kusema wale waliosoma shule fulani hawastahili mikopo
  10. Kubana misaada ya Watanzania walioathirika na majanga kama matetemeko na kupunguza bajeti ya majanga ya kitaifa na hata kuwaambia wananchi wakipatwa na majanga watajijua
  11. Kutopunguza bei ya mafuta hata pale ambapo bei ya mafuta katika soko la dunia imeshuka kwa kiwango kikubwa ili sehemu kubwa ya faida katika biashara ya mafuta ya magari ilirudi serikalini
  12. Kubana safari za kikazi za wafanyakazi kwa kisingizio cha kubaki kazini ili kuwajibika
  13. Kubambikia kesi za uhujumu uchumi wafanya biashara wakubwa na kuwaambia kwamba wakitaka wasifungwe basi inabidi watoe malipo ya "makubaliano" ambapo ni kama kusema waihonge serikali
  14. Kunyang'anga mamlaka ya Bunge kupanga matumizi ya fedha za serikali na kuiweka chini ya uamuzi wa raisi
  15. Kupandisha ushuru wa bidhaa zinazoagizwa na wananchi toka nje kama magari kwa kisingizio cha "price uplift" ili fedha zaidi ziingie serikalini
  16. Nk, nk, nk

Hivyo basi, Watanzania tunapaswa kuamka na kutambua kwamba, unapokopa leo, ukalipa baadae, unalipa wakati uchumi wako umekua kutokana na mkopo uliochukua, na maumivu ya kurejesha mkopo taratibu yanakuwa si makubwa ukilinganisha na kama ungewakamua wananchi fedha za ndani.

Kwa hiyo si vibaya kwa Samia kukopa ili kutekeleza miradi mikubwa kwa manufaa ya maendeleo ya taifa. Kama kuna lawama tunapaswa kumtupia raisi Samia ni pale atakapokuwa akikopa kwa ajili ya matumizi ya kawaida (recurrent expenditure) na sio matumizi ya miradi yenye kuinua uchumi (capital expenditure).
Kukopa sio jambo baya. Nchi karibia zote duniani zinakopa kasoro Hong Kong (ni mojawapo ya nchi zisizo na madeni), ambayo uchumi wake Una kiwango cha Chini kabisa cha Deni kwa ulinganifu na pato Kuu. HongiKongi ndiyo Jumuiya ya watu pekee duniani ambayo ni almost haina deni. Hapo zingatia neno ALMOST. Ina hazina
ya kutosha na kubwa ya ukwasi wa kigeni na Sheria imara za kifedha. Pato lao la Taifa ni kubwa pasina mfano, huyo USA tu hagusii,

OVA

Mlomo lufyeto
 
Ufisadi sio lazima tatizo liwe mfumo - ni tabia (culture) ya watu.

Leo tukisema tuwe kama China, ukifisadi fedha za umma unahukumiwa kifo, na tukanyonga watu wawili watatu, unafikri kuna mtu atadiriki kufanya ufisadi? Nyerere yeye alichapa viboko 24, na watu waliogopa, na hata waliapa "Rushwa kwangu mwiko, sitatoa wala kupokea rushwa" na alifanikiwa.

Ethiopia hawakubadili mfumo enzi za Zanawi. Zanawi alimfunga jela miaka mitano tu ambaye alikuwa deputy wake wakati wa vita, akasema ikiwa nimefunga jela rafiki yangu kipenzi kwa ajili ya rushwa, sasa jaribu wewe mtu baki. Ufisadi ukafa. Nenda kwa Kagame Rwanda ufanye ufisadi uone utakavyokiona cha mtema kuni.

Kwa hiyo inahitaji kuwa na sheria kali tu, kwa kuwa kwa mtu mweusi ufisadi uko kwenye damu, ni adhabu tu ndio itamwogopesha sio mfumo
Sasa ukiwa unayajua haya, mbona akili yako inakuwa fyatu unapoanzisha mada za kichawa chawa kama uliyoweka hapa?
Watu wengine sijui mmeumbwa vipi, kwa kujichanganyachanganya katika kila jambo ili mradi mkidhi mahitaji yenu binafsi.
 
Ufisadi sio lazima tatizo liwe mfumo - ni tabia (culture) ya watu.

Leo tukisema tuwe kama China, ukifisadi fedha za umma unahukumiwa kifo, na tukanyonga watu wawili watatu, unafikri kuna mtu atadiriki kufanya ufisadi? Nyerere yeye alichapa viboko 24, na watu waliogopa, na hata waliapa "Rushwa kwangu mwiko, sitatoa wala kupokea rushwa" na alifanikiwa.

Ethiopia hawakubadili mfumo enzi za Zanawi. Zanawi alimfunga jela miaka mitano tu ambaye alikuwa deputy wake wakati wa vita, akasema ikiwa nimefunga jela rafiki yangu kipenzi kwa ajili ya rushwa, sasa jaribu wewe mtu baki. Ufisadi ukafa. Nenda kwa Kagame Rwanda ufanye ufisadi uone utakavyokiona cha mtema kuni.

Kwa hiyo inahitaji kuwa na sheria kali tu, kwa kuwa kwa mtu mweusi ufisadi uko kwenye damu, ni adhabu tu ndio itamwogopesha sio mfumo
Sasa hiyo tabia utaiondoa bila kutengeneza mfumo mzuri? Hili halihitaji usomi wowote kulielewa. Mfumo wetu mbovu ndiyo umefanya watu wengi wajenge tabia ya ufisadi. Kwa taarifa yako Tanzania sheria za ufisadi ni nzuri tu wala hazina walakini. Tatizo ni kuwa wanaofanya ufisadi wanazikwepa kwa sababu ya mfumo mbovu. Huhitaji kunyonga watu ili kumaliza ufisadi. Tubadili mfumo, tuwe na uwezo wa kupata viongozi wawajibikaji na pioa tuwe na uwezo wa kuondoa viongozi wenye elements za ufisadi. Tanzania kuna kulindana kwa viongozi na hili ni tatizo la mfumo na siyo sheria.
 
Back
Top Bottom